settings icon
share icon
Swali

Je, mtu anaweza kuzaliwa na jinsia isiyo sahihi?

Jibu


Tunaishi katika ulimwengu uliochanganyikiwa na ulioanguka, na mkanganyiko huo unaenea kila mahali, hivi kwamba maswali ya msingi kama vile, “mimi ni jinsia gani?” inakuwa ngumu kwa baadhi ya watu kujibu. Watu wengine wanadai kuwa wana jinsia isiyo sahihi ya kuzaliwa, au mwili usio sahihi. Mwanaume anaweza kuamini kuwa yeye ni mwanamke, lakini nafsi yake “imekwama” katika mwili wa wa kiume. Madai kama haya yanaungwa mkono na wengine wanaotetea jamii ‘isiyo ya jinsia ya kiume wala kike.” Lakini wale wanaoona tofauti za kijinsia kuwa sio chochote zaidi ya majina ya kiholela tu au “sanduku” ya kuvunjwa basi wanapinga mpango wa Mungu wa uumbaji.

Jambo la msingi katika kuelewa kwetu kwa jinsia ya binadamu ni kwamba Mungu aliumba jinsia mbili pekee. Hivi sasa, ulimwengu unapenda kuzingatia jinsia (kulingana na muundo wa jamii) kama isiyo na uhusiano wowote wa hali ya kuwa kike au kiume, lakini Biblia hailete tofauti hizo. Biblia ina suluhu ya mkanganyiko huu wa dunia: “Mwanaume na mwanamke aliwaumba” (Mwanzo 1:27). Wazo lolote la siku hizi kuhusu jinsia nyingi -au pia “mwendelezo”wa jinsia na jinsia zisizo na kikomo -sio la kibliblia. Mtu anaweza kudai kwamba amebadilisha jinsia lakini hio haibadilishi muundo wa Mungu na kusudi lake la kumuumba.

Watoto wanaokua katika ulimwengu uliochanganyikiwa wanasongwa na jumbe za kukanganya. Wavulana wachanga wanaambiwa sio lazima wawe wavulana; wasichana nao wanaambiwa kwambwa wanaweza kuwa sio wasichana kweli. Chochote wanachohisi basi hivyo ndivyo walivyo -mvulana, msichana au mchanganyiko wa zote mbili. Ulimwengu unawaambia kwamba haijalishi. Mchanganyiko na sintofahamu hiyo inatekelezwa kwa njia nyingi: siku zisizoegemea jinsia shuleni, kupigwa marufuku

istilahi kama vile wavulana na wasichana darasani, kuenea kwa vyoo vinavyotumika na watu wa jinsia yoyote, mitaala inayokuza ndoa za jinsia moja, na kadhalika. Sio ajabu kwamba watu wanakua wakihangaika na utambulisho wao wa kijinsia. Lakini Bwana wetu alionya kuhusu kuwapotosha watoto: “Yesu akawaambia wanafunzi wake: Mambo yanayosababisha watu watende dhambi hayana budi kutukia. Lakini ole wake mtu yule anayeyasababisha. Ingekuwa heri kama mtu huyo angefungiwa jiwe la kusagia shingoni na kutoswa baharini, kuliko kumsababisha mmojawapo wa hawa wadogo kutenda dhambi. (Luke 17:1–2).

Watu wengine wadai kuwa “wamehisi kuwa wa jinsia tofauti tangu utotoni.” Lakini mtu angejuaje jambo hilo? Wanalinganisha hisia zao na nini haswa? Jinsi watu wanavyohisi ndivyo wanavyojua, kwa kila mtu, jinsi anavyohisi ni “kawaida” kwake. Ulinganisho wowote na hisia za watu wengine itakuwa ni dhana tu. Watu wengine wanaweza kushawishika kuwa “walihisi kuwa wa jinsia tofauti” wakati fulani katika maisha yao, lakini hawana ulinganisho wa kimsingi.

Kwa kuzingatia hulka ya kutosha, mtu yeyote anaweza kushawishika kuwa yeye niwa jinsia tofauti.

Mara nyingi baadhi ya watu wanachukuliwa kuwa wa jinsia tofauti kwa sababu ya ile tafauti yao ya asili kimaadili na vile wanavyoitikia, na watu hao, “huwaza nyuma” dhana kuwa hivyo ndivyo wamekuwa tangu utotoni.

Lakini huku kufikiria upya kwa utoto wa mtu ni tofauti na kutamani kuwa na jinsia tofauti. Mtu anaweza kutamani angekuwa na jinsia nyingine kwa sababu nyingi, lakini hiyo haimaanishi ndivyo ilivyo. Mzazi anaweza kutia tamaa hiyo ndani ya mtoto, au mtoto anaweza kuona faida ambazo jinsia tofauti inafurahia na kuzitamani. Mtoto huyo pia anaweza kutamani kuwa na urefu wa futi saba, lakini hiyo haibadilishi ukweli.

Biblia inasema kuwa Mungu aliwaumba “mwanamume na mwanamke” na kusema kwamba uumbaji wake ni “mzuri sana” (Mwanzo 1:27, 31). Mpango wa Mungu ulikuwa mkamilifu, lakini kama ilivyo kwa vitu vinginevyo katika nyanja ya ulimwengu, hali ya ukamilifu iliharibiwa na dhambi. Dhambi iliathiri vibaya uumbaji wote, na kuumiza sio tu uhusiano wa binadamu na Mungu bali uhusiano kati ya binadamu na mpangilio mwingine wa uumbaji pia. Ulimwengu wetu umeanguka na madhara ya dhambi yameenea katika kila kitu. Magonjwa, kasoro za kusaliwa, majanga ya asili, matendo ya dhambi na matokeo ya dhambi za watu wengine na pia dhambi zetu, yote haya ni kwa sababu ya ulimwengu ulioanguka. Wakati mwingine madhara haya yaweza kutokea kwa njia ya hitilafu za kiasili; wakati mwingine yanaweza kuwa ni kwa sababu ya dhambi mahususi. Je, wakati mwingine hitilafu inaweza kufanyika katika jinsia, kimwilia au kiakili? Tunatambua kwamba mtu anaweza kuzaliwa akiwa na viungo vya kike na kiume – ingawa jinsia ya kibaolojia ya mtu inaweza kutambuliwa na vipimo vya matibabu.

Tunajua kwamba tunahusika katika vita vya kiroho vya nafsi zetu. Ulimwengu unatafuta kutufananisha na mfano wake, na ndiyo sababu tunapaswa kugeuzwa kwa kufanywa upya nia zetu (Warumi 12:1-2). Shetani anajaribu kutudanganya na kutuhimiza kuhoji mpango wa Mungu. Mojawapo ya hila za shetani ni kutufanya tusiridhike na jinsi Mungu alivyotuumba. Yeye ananong’onea wengine, “wewe ni mnono na hupendezi.” Na kwa wengine, “wewe ni mpumbavu na ovyo.” Na pia kwa wengine, “unaonekana kama mvulana, lakini kwa kweli wewe ni msichana.” Katika kila kisa ujumbe wa msingi ni ule ule: “Mungu aliburuga.”

Hii pia tunajua, kwamba viumbe wote wanalia kwa maumivu ili wapate kuwekwa huru kutoka kwa laana na uharibifu wa dhambi. (Warumi 8:20-22). Uharibifu anaoletwa na dhambi unatolewa kwa njia ya ukombozi wa Kristo. Kupitia wokovu, Yesu Kristo hutupa msamaha wa dhambi, hubadilisha matokeo ya uchaguzi wetu mbaya, na kufidia udhaifu wetu.

Kila mmoja wetu hukabiliwa na vita tofauti. Yesu Kristo hutuweka kwenye njia ya ushindi. Waebrania 12:1-2 inasema, “ mani a tuweke kando kila kitu kinachotuzuia na ile dhambi inayotuzinga kwa urahisi, nasi tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa kwa ajili yetu. mani a tumtazame sana Yesu mwanzilishi na mkamilishaji wa mani yetu, yeye ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake alistahimili msalaba, bila kujali aibu ya huo msalaba, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.” Msalaba ni muhimu. Yesu alianzisha imani yetu, na ataikamilisha. Ushindi wake utakuwa wetu pia.

Wengine wanaweza kuwa wanapigana na majaribu ya jinsia tofauti, uchoyo, kiburi, hasira, au dhambi yoyote ile. Mwingine anaweza kukabiliana na mkanganyiko wa jinsia. Haijalishi vita tunavyopigana vya dhambi na uwongo wa shetani, swali tunalopaswa kujibu ni, “Je, Kristo na kazi yake ya ukombozi inatosha kwa vita vyetu?” Yesu kwa hakika anatosha kwa vita vyetu vyote, na anatamani kututakasa kupitia kwa Neno Lake la kweli (Yohana 17:17).

Kama watoto wa Mungu, tunapaswa kuridhika maishani (Wafilipi 4:11; 2 Wakorintho 12:10). Tunatambua kwamba sisi wote tuna upungufu, kimwili, kiakili, kihisia na kiroho. Lakini kupitia Kristo huo upungufu hautaingilia kati ya mpango Mungu alio nao kwetu sisi kumheshimu na kumtumikia.

“Msiogope enyi kundi dogo, kwa maana Baba yenu ameona vyema kuwapa ninyi Ufalme” (Luka 12:32).

Ikiwa mtu anahisi kuwa alizaliwa katika jinsia isiyo sahihi, suluhisho sio upasuaji wa kubadilisha jinsia, tiba ya homoni, kuvaa mavazi ya jinsia tofauti, na kadhalika. Hizo ni njia za dunia za kukubali uwongo wa shetani. “Upendo haufurahii mabaya bali hufurahi pamoja na kweli” (1 Wakorintho 13:6). Na Mungu hafanyi makosa. Yule ambaye anahisi mwamba alizaliwa katika mwili usiofaa, kwanza kabisa anafaa kupata nguvu ya mabadiliko ya Kristo. Wakati “tunapata kuwa washiriki wa asili ya uungu,” tunaepuka “upotovu ulioko duniani unaosababishwa na tamaa mbaya” (2 Petro 1:4).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, mtu anaweza kuzaliwa na jinsia isiyo sahihi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries