settings icon
share icon
Swali

Je, jina lako litukuzwe katika Sala ya Bwana inamaanisha nini?

Jibu


Sala ya Bwana, iliyoandikiwa katika Mathayo 6, huanza na “Baba yetu uliye mbinguni,

Jina lako litukuzwe” (Mathayo 6:9). Kutukuza kitu ni kukifanya kitakatifu au kukitenga au kukitakasa. Yesu aliwafundisha wafuasi Wake kusali kwamba jina la Mungu Baba ”litukuzwe.” Ombi pekee la maana huja kwanza. Ni la muhimu sana Mungu kutukuza jila Lake.

Ni kwa njia gani tunataka Mungu Atukuze jina Lake? Je, ni kwa njia gani jina lake linapaswa kutiwa wakfu au kufanywa takatifu? Mwandishi mmoja anaeleza kuwa ni ombi kwa mungu kutenda kwa njia ambayo inaonyesha wazi utakatifu na utukufu Wake (Albert Mohler In The Prayer that Turns the World Upside Down: The Lord’s Prayer as a Manifesto for Revolution, p. 61). Mungu anaonyesha utakatifu wake ulimwenguni kwa kuunda watu watakatifu ambao wataliitia jina lake, kutangaza injili, na kukamilisha kazi nzuri (Waefeso 2:10).

Hakuna mtu anayependa jina lake lisahaulike, liandikwe vibaya au kutamkwa vibaya. Majina yetu ni sehemu ya utambulisho wetu na thamani ya mtu binafsi. Tunathamini kuwa na “jina njema,” yaani sifa isiyo na lawama. Vivyo hivyo, jina la Mungu huzungumza juu ya utambulisho Wake, tabia Yake, na matendo Yake. Daudi alisema, “hunihuisha nafsi yangu. Huniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake” (Zaburi 23:3; tazama Isaya 48:9-11 na Ezekieli 20:14). Jina la Mungu-tabia na sifa Yake-lazima zitengwe kuwa takatifu katika ulimwengu huu, na hivyo ndivyo Yesu anatufundisha tusali kwa ajili yake.

Ombi “Jina lako litukuzwe” linakuja kwanza katika Sala ya Bwana. Papo hapo, Yesu anaondoa lengo kutoka kwetu na kuelekeza fikira zetu kwa Mungu. Inamhusu Yeye, utakatifu Wake, na kazi Yake ulimwenguni. Yesu alitufundisha kuanza sala zetu kwa kumtambua Mungu ambaye tunamuomba. Yeye ni Baba mwenye upendo ambaye hutualika katika uwepo Wake. Anatujali kwa kweli. Mungu ni mtakatifu na anastahili heshima yote, na kipaumbele chetu cha kwanza ni kuomba ili ulimweng uone jinsi alivyo mtakatifu na mtukufu.

Katika tukio tofauti, Yesu alisali hivi kwa ajili ya wafuasi Wake: “Siombi kwamba uwaondoe ulimwenguni, bali uwalinde dhidi ya yule mwovu. Wao si wa ulimwengu huu, kama vile mimi nisivyo wa ulimwengu. Uwatakase kwa ile kweli, neno lako ndilo kweli. Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami nawatuma vivyo hivyo. Kwa ajili yao najiweka wakfu ili wao nao wapate kutakaswa katika ile kweli” (Yohana 17:15-19). Neno kutakasa katika Sala ya Yesu ya Kuhani Mkuu ni tafsiri ya neno lile lile la Kigiriki linalotafsiriwa “kutukuzwa” katika Mathayo 6:9). Yesu aliomba sala hii mahsusi kwa ajili ya wanafunzi Wake, lakini pia kwa wale ambao wangemwamini kupitia ujumbe wao-kumaanisha wale wote ambao wameweka imani yao katika Yesu Kristo (Yohana 17:20). Kama watoto wa Mungu (Yohana 1:12), tumeitwa kuwa watakatifu kama yeye alivyo mtakatifu (1 Petro 1:16).

Waraka wa kwanza wa Petro 3:15 inatuambia “Bali mtakaseni Kristo kuwa Bwana mioyoni mwenu.” Kutakasa katika kifungu hiki ni tafsiri nyingine ya neno la Kigiriki la “kutukuza.” Mojawapo ya njia ambazo tunamtambua Yesu kama Bwana na kuishi maisha yetu kwa kumheshimu Mungu. Tunaelekeza mioyo yetu Kwake, kuweka tumaini letu Kwake, kumtii, na kushiriki na wengine kumhusu. Na tufuate sala ya Yesu kama kielelezo cha maombi na “jina lako litukuzwe” iwe ndio haja ya mioyo yetu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, jina lako litukuzwe katika Sala ya Bwana inamaanisha nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries