settings icon
share icon
Swali

Je Je! ngono ni dhambi?

Jibu


Katika muktadha sahihi, ngono sio dhambi. Kwa kweli ngono ni wazo la Mungu. Katika Mathayo 19:4-6, Yesu anasema kwa mamlaka ya kiungu, “Hapo mwanzo Muumba aliwaumba mwanaume na mwanamke, naye akasema, ‘Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja’? Hivyo si wawili tena, bali mwili mmoja. Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.” Tukio la uumbaji basi ndilo msingi wa taasisi ya ndoa, ambayo ilihalalishwa na Muumba Mwenyewe na kuanzishwa kuwa muungano wa kudumu kati ya mume mmoja na mke mmoja.

Ukweli kwamba Mungu aliumba binadamu kuwa “mwanamume na mwanamke” unaonyeshesha kwamba tumeumbwa kama viumbe vya ngono. Na amri ya Mungu ya “kuzaa na kuongezeka” haiwezi kutumizwa bila ngono (Mwanzo 1:28). Ngono ni agizo kutoka kwa Mungu, kwa hivyo ngono sio dhambi ikiwa inafanywa na mwenzio wa ndoa ambaye ni jinsia tofauti.

Neno ngono halipatakani katika Biblia. Kutajwa mara nyingi kwa neno hilo katika jamii, na mazoea ya ulimwengu ya kidhihaki, yamelipa neno hilo kiwango fulani cha sifa mbaya. Lakini Mungu kamwe hakukusudia liwe neno chafu.

Wimbo Ulio Bora hufuatilia uhusiano wa kimapenzi kati ya mume na mke wake katika kipindi cha uchumba, usiku wa arusi, na baadaye. Ufafanuzi wa raha ya mume na mke katika mlango wa 4 ni makinifu na ilhali hauna makosa katika maana yake. Ufafanuzi huo unafuata katika 5:1 kwa kibali cha Mungu: “Kuleni enyi marafiki, kunyweni; kunyweni sana wapendwa wangu.”

Ni katika nje ya ndoa tu ambapo ngono ni dhambi. Mungu aliiweka wazi kwamba malazi ya ndoa ni lazima yawe safi (Waebrania 13:4). Matendo ya ngono nje ya ndoa yanaitwa usherati. Wakorintho wa Kwanza 6:9-10 inasema, “Je, hamjui kwamba wasio haki hawataurithi Ufalme wa Mungu? Msidanganyike: Waasherati, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wahanithi, wala walawiti, wala wezi, wala wenye tamaa mbaya, wala walevi, wala wanaodhihaki, wala wanyangʼanyi hawataurithi Ufalme wa Mungu.” Kushiriki katika ngono bila ndoa ni kukosa maadili, na “Mapenzi ya Mungu ni kwamba ninyi mtakaswe, ili kwamba mjiepushe na zinaa” (1 Wathesalonike 4:3; linganisha 1 Wakorintho 6:18).

Ikiwa ujumbe wa Biblia kuhusu kujiepusha na ngono hadi wakati wa ndoa ungekubaliwa, kungekuwa na magonjwa machache sana ya zinaa, upungufu wa uavyaji mimba, mimba zisizotakikana, na watoto wachache sana wanaokua bila wazazi wote wawili maishani mwao. Kujizuia kunaokoa maisha, kunawakinga watoto, kunaupa uhusiano wa ngono kuwa na dhamani sahihi, na la muhimu zaidi humheshimu Mungu.

Kwa vyovyote vile ngono kati ya mume na mke sio dhambi. Badala yake ni dhihirisho la upendo, uaminifu, ushirika, na umoja. Ngono ni zawadi ya Mungu kwa wanandoa ya raha na kuzaa.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je Je! ngono ni dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries