settings icon
share icon
Swali

Je, Yesu alikua na kaka na dada (ndugu)

Jibu


ndugu wa Yesu yametajwa katika mistari kadhaa katika Biblia . Mathayo 12:46, Luka 8:19, na Marko 3:31 za sema kwamba mama na ndugu zake Yesu walikuja kumwona. Biblia inatuambia kwamba Yesu alikuwa na ndugu wanne: Yakobo, Yusufu, Simioni na Yuda (Mathayo 13:55). Biblia pia inatuambia kwamba Yesu alikuwa na dada, lakini wao hawajatajwa majina yao wala kuhesabiwa (Mathayo 13:56). Katika Yohana 7:1-10, ndugu zake wanaenda kwenye sikukuu hukui Yesu anabaki nyuma. Katika Matendo 1:14, ndugu zake na mama yake wameelezewa wakiomba pamoja na wanafunzi. Wagalatia 1:19 inataja kwamba Yakobo alikuwa ndugu yake Yesu. Hitimisho zaidi la asili ya vifungu hivi ni kutafsiri kwamba Yesu alikuwa na ndugu halisi wa damu.

Baadhi ya Wakatoliki wa Kirumi hudai kwamba hawa "ndugu" walikuwa kweli binamu zake Yesu. Hata hivyo, katika kila tukio, neno maalum la Kigiriki la "ndugu" limetumika. Wakati neno ambalo limetumika linaweza kutaja ndugu wengine, maana yake ya kawaida na halisi ni ndugu wa kimwili. Kulikuwa na neno la Kigiriki la "binamu," na halikutumika. Zaidi ya hayo, kama walikuwa binamuze Yesu, kwa nini mara nyingi wao hutajwa kuwa pamoja na Mariamu mamaye Yesu? Hakuna kitu katika mazingira ya mama yake na ndugu kuja kumwona kinatupa fununu kwamba walikuwa watu wengine zaidi ya wa ukoo halisi, husiana wa damu na nduguk wa kambo.

Jadala la pili la Katoliki ni kwamba ndugu na dada wa Yesu walikuwa wana wa Yusufu kutoka kwa ndoa iliyotangulia. Nadharia nzima ya Yusufu kuwa mkubwa kiasi kwa umri zaidi ya Mariamu, baada ya kupata jiko awali, na kuzaa watoto wengi, na kisha kuwa mjane kabla ya kuolewa na Mariamu ni tunio lilo tungwa bila msingi wowote wa Biblia. Tatizo liloko ni kwamba Biblia haina haidokezi kwamba Yosufu alikuwa ameolewa au alikuwa na watoto kabla ya kumuoa Mariamu. Kama Yusufu alikuwa na watoto angalau sita kabla ya kumwoa Mariamu, ni kwa nini hawajatajwa katika safari ya Yosufu na Mariamu kwenda Bethlehemu ( Luka 2:4-7 ) au safari yao ya Misri (Mathayo 2:13-15) au safari yao wakirudi Nazarethi (Mathayo 2:20-23) ?

Hakuna sababu ya kibiblia ya kuaminika kwamba hawa ndugu ni kitu kingine chochote zaidi ya watoto halisi wa Yusufu na Mariamu. Wale wanaopinga wazo kwamba Yesu alikuwa na ndugu na dada wa kambo hufanya hivyo, sio kutoka kwa kusoma Maandiko, lakini kutokana na dhana kable ya ubikira daima wa Mariamu, ambayo yenyewe kwa uwazi sio ya kibiblia: "Lakini yeye (Yusufu) alikuwa hakuwa na muungano wowote na (Mariamu) hadi alipojifungua mtoto wa kiume. Na yeye akampa jina Yesu "(Mathayo 1:25). Yesu alikuwa ndugu wa kambo, ambao walikuwa wana wa Yusufu na Mariamu. Hayo ni mafundisho yaliyo wazi na yasiokuwa na utata kwa neno la Mungu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Yesu alikua na kaka na dada (ndugu)
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries