settings icon
share icon
Swali

Je, Mungu aliumba ulimwengu?

Jibu


Fundisho la Maandiko kuhusu asili ya ulimwengu linapatikana katika Mwanzo 1:1, ambayo inasema kwamba, hapo mwanzo, Mungu aliumba mbingu na nchi. Steven Hawking anajaribu kuzuia ukweli huu (au, angali, katika jitiada zake, anamfanya Muumba aonekane kuwa amepita mipaka katika suala la mwanzo wa ulimwengu). Hata hivyo, dhana zake sio geni, bali ni matoleo ya hivi punde ya jaribio la juu sana la kuelezea jinsi ya kupata kitu (k.m., ulimwengu) kutoka kwa utupu.

Uungwajimkono wa kazi ya Hawking unatoka katika kuwepo kwa sheria ya mvuto. Wanafizikia wanajua kuwa nishati inayohusishwa na nguvu ya mvuto ni hasi, huku nishati inayohusishwa na vitu vingi vya kawaida (basiboli/aina ya mpira wa magongo, magari nk) ni chanya. Kuna uwezekano kuwa hizi nishati chanya na asi zinaweza kughairi, na hii kusababisa nishati sifuri. Hali mbili zilizo na nishati sawia (au tofauti ya nishati sifuri), ziko katika uhalisi na zinapendekezwa kuwa sawia. Mfano utakuwa mpira wa kandanda kwenye sakafuni jikoni au mezani bila kutaka kubingirika mahali popote. Hii ni kwa sababu katika kila nafasi mpira ulioko katika sakafu jikoni unaweza chukua utakua na nguvu sawia, kwa hivyo hamna kati ya hizo nafasi mbili inayoweza pendelewa kuliko nyingine.

Hawking anawazia asili ya ulimwengu katika njia hiyo hiyo. Kwa kuwa inawezekana kufikiria uumbaji wa ulimwengu kuwa na (nishati sifuri), Hawking adokeza kwamba hakuna haja ya kuelezea jinsi ilivyoumbwa. Lakini ufahamu huu hauko katika msingi wa fisikia, bali ni ufahamu wa dhamiri falsafa ya Hawking mwenyewe. Katika mfano wa mpira wa kandanda ukiwa sakafuni jikoni, inawezekana kufikiria mpira wa kandanda unaweza kukaa mahali popote sakafuni bila kuhitaji ufafanuzi wowote; hata hivyo ni jambo lingine toafuti kabisa kusema kwamba mpira wa kandanda na sakafu jikoni vilitoka utupu.

Majaribio ya Hawking ya kushughulikia tatitzo hili si mapya kwa njia yoyote kwa wanafalsafa; ni mojawapo ya masuala kongwe sana katika falsafa ya mateuzi: “ex nihilo nihil fit” (kihalisi, “hakuna kitu kinaweza kutoka mahali bila kitu”). Dhana ya Hawking inaweza thibitisha kwamba hali mbili za kimwili (ulimwengu uliopo dhidi ya usiokuwapo) kinishati ziko sawia, lakini hii haifanyi chochote kushughulikia suala la sababu na athari. Hakuna maelezo yanayohitajika kueleza kwa nini mpira unakaa karibu na jiko badala ya karibu na jokovu, lakini maelezo yanahitajika ikiwa mpira utasonga toka kwa kando ya jiko hadi juu ya jokovu. Katika fizikia, mabadiliko hayawezi fanyika bila maelezo; katika lugha ya kifalsafa, athari haiwezi fanyika bila sababu.

Mawazo ya Hawking hayafanyi chochote katika kushughulikia hili; suala la asili ya ulimwengu iko vile ilikuwa mbeleni. Haiwezekani kupata kitu kutoka utupu. Ni wazo la Muumba tu linaloweza elezea kikamilifu mahali ulimwengu ungeweza kutoka. Isitoshe, taarifa ya Hawking kwamba sayansi itashinda dini sikuzote “kwa sababu inafanya kazi” inaonyesha kutoelewa kwa msingi kwa falsafa ya sanyansi. Ukweli haumuliwi na “matendo,” bali ikiwa unapatana na ukweli unaotuzunguka. Wakati tunasema kuwa kauli fulani ni ya ”kweli,” tunasema kwamba maudhui ya kauli hiyo yanaelezea jinsi mambo yalivyo. Uhusiano huu kati ya kauli na ukweli inaouelezea inamtegemea mtu na akili yake. Kauli inaweza kuwa ya kweli au uongo, bila kujali kama inavyoonekana kwa mtu binafsi kuelezea hali sahihi ya mambo. Hiki ndicho tunamaanisha wakati tunasema kwamba ukweli hauna upendeleo; “thamani ya ukweli” ya kauli ni sifa ambayo inamiliki bila ufahamu wa mtu.

Ingawa, pindi tunapoanza kujaribu kuamua ikiwa kauli fulani ni ya kweli au ya uwongo (vile inavyofanyika katika sayansi na dini), njia pekee tunaweza kujua jinsi ya kuendelea ni kujaribu kuipa jaribio kauli “kuona kama inafanya kazi.” Kwa mfano tuseme tunataka kuamua ikiwa kauli, “paka wote ni wa rangi ya hudhurungi” ni ya kweli. Tunaweza kuanza uchunguzi wetu kwa kukusanya paka wote pamoja na kuwaangalia kila mmoja wao kuona ikiwa kuna yeyote ambaye haambatani na kauli inayochunguzwa, na hapo kuifanya kuwa ya uwongo. Tunahitaji tu kupata paka mmoja wa rangi ya kijivu ili kujua kwamba kauli ya awali ni ya uwongo: paka wote sio wa rangi ya hudhurungi.

Basi itakuaje ikiwa kila paka tuliyeweza kumpata kwa kweli alikuwa wa rangi ya hudhurungi? Ni wazi kwamba ulimwengu una paka wa aina nyingi na rangi tofauti. Katika kesi hii, ingawa kauli “inafanya kazi” (kutokana na uchunguzi wetu, paka wote wanaonekana kuwa na rangi ya hudhurungi), ni wazi kuwa hiyo sio kweli. Kwa hivyo, suala la kama sayansi au dini “zinafanya kazi” kwa hakika halihusiani kabisa na suala la ukweli katika kila moja ya taaluma hizi. Ingawa ukweli unaweza kugunduliwa kwa kutambua kile kinachofanya kazi, kwa sababu tu usemi huo unaonekana kufanya kazi haimaanishi kuwa ni kweli.

Kwa muhtasari, hoja ya Hawking inashindwa kwa misingi ya kifalsafa. Hawking anajaribu kumbadili Mungu na sheria fulani (mvutano). Hata hivyo, Hawking anashindwa kushughulikia suala muhimu lililopo-yaani, chanzo cha sheria ya fizikia. Sheria ya uvutano ilitoka wapi na kwa njia gani utupu unaeza zalisha kitu? Sheria ya kimwili sio utupu. Zaidi ya hayo, dhana ya Hawking ya wingi wa malimwengu yalikusanyika ili kuepuka hitimisho la urekebishaji mzuri haina mantiki kifalsafa, inachochewa kimetafizikia, na haina ubishi kuliko tafsiri ya wakanamungu.

Ni kwa nini wanadamu wanatafuta kumuondoa Mungu kutokana na kuhusika katika uumbaji wa ulimwengu? Jibu ni rahisi sana. Wanadamu humchukia Mungu na hawataki kuwa chini ya sheria ya Mungu, au kuwajibika kwa matendo yetu. Kama vile Paulo anaandika katika Warumi 1:21-23, “Kwa maana ingawa walimjua Mungu, hawakumtukuza yeye kama ndiye Mungu wala hawakumshukuru, bali fikira zao zimekuwa batili na mioyo yao ya ujinga ikatiwa giza. Ingawa walijidai kuwa wenye hekima, wakawa wajinga na kubadili utukufu wa Mungu aishiye milele kwa sanamu zilizofanywa zifanane na mwanadamu ambaye hufa, na mfano wa ndege, wanyama na viumbe vitambaavyo”.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Mungu aliumba ulimwengu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries