settings icon
share icon
Swali

Je! Mungu aliumba kuzimu?

Jibu


Kuzimu ni mahali pa mateso ambapo palitayarishwa na Mungu kwa ajili ya shetani na malaika zake (Mathayo 18:9; 25:41). Maneno kuzimu (Kigiriki) na sheol (Kiebrania) nyakati zingine huhusishwa na kuzimu. Hata hivyo, kuzimu/sheoli ni mahali au ulimwengu ambapo roho za watu hueanda wanapokufa (ona Mwanzo 37:35). Kuzimu/Sheoli sio mahali pa mateso hasa kwa sababu watu wa Mungu walisemekana kwenda huko pamoja na waovu. Katika Agano Jipya, tunaona kwamba kuzimu kwa njia Fulani “imegawanywa.” Hiyo ni, ulimwengu wa wafu umegawanywa katika mahali pa faraja na mahali pa mateso (Luka 16:19-31).

Kuna maneno mengine yanayohusiana na kuzimu katika Biblia kama vile Gehena na ziwa la moto. Ni wazi kwamba kuna mahali halisi ambapo roho za wasiookolewa huenda milele (Ufunuo 9:1; 20:15; Mathayo 23:33).

Kila kitu chochote kilichowahi kuwako au kilichopo au kitakachokuwako kimeumbwa na Mungu, pamoja na kuzimu (Wakolosai 1:16). Yohana 1:3 inasema, “Vitu vyote viliumbwa kwa yeye, wala pasipo yeye hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa.” Mungu pekee ndiye mwenye uwezo wa kumtupa mtu motoni (Luka 12:5). Yesu anazo funguo za mauti na kuzimu (Ufunuo 1:18).

Yesu alisema kwamba kuzimu “ilitayarishiwa” Shetani na pepo zake (Mathayo 25:41). Ni adhabu ya haki kwa mwovu. Jehanamu, au ziwa la moto, itakuwa pia hatima ya wale wanaomkataa Kristo (2 Petro 2:4-9). Habari njema ni kwamba watu wanaweza kuepuka kuzimu. Mungu, katika rehema na upendo wake usio na kikomo, amefanya njia ya wokovu kwa kila mtu anayemwamini Mwana wa Mungu, Yesu Kristo (Yohana 3:16, 36; 5:24).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mungu aliumba kuzimu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries