settings icon
share icon
Swali

Kama nimeokolewa na dhambi zangu zote zimesamehewa , kwa nini nisieendelee kutenda dhambi?

Jibu


Mtume Paulo alijibu swali sawia katika Warumi 6:1-2, "Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?" dhand kwamba mtu anaweza “kumwamini Kristo Yesu" kwa ajili ya wokovu na kisha kuendelea kuishi kama yeye alivyoishi mbeleni, ni wazo la kigeni kwa Biblia. Waumini katika Kristo ni viumbe vipya (2 Wakorintho 5:17). Roho Mtakatifu anatubadilisha kutoka kuzalisha matendo ya mwili (Wagalatia 5:19-21) hadi kuzaa matunda ya Roho (Wagalatia 5:22-23). Maisha ya Kikristo ni maisha yaliyobadilishwa kwa sababu Mkristo amebadilishwa.

Chenye kinatofautisha Ukristo kutoka dini zingine ni kwamba Ukristo hulingana na kile Mungu amekifanya kwa ajili yetu kwa njia ya Yesu –fanikio la kiungu. Kila dini zingine za dunia zinalingana na kile tunapaswa kufanya ili kupata kibali cha Mungu na kwa msamaha- mafanikio la kibinadamu. Kila dini nyingine hufundisha kwamba ni lazima kufanya mambo fulani na kuacha kufanya baadhi ya mambo mengine ili kupata upendo na huruma za Mungu. Ukristo, imani katika Kristo, hufundisha kwamba sisi tunafanya mambo fulani na kuacha kufanya mambo fulani kwa sababu ya kile ambacho Kristo amefanya kwa ajili yetu.

Jinsi gani mtu yeyote, baada ya kukombolewa toka kwa adhabu ya dhambi, milele katika moto wa Jehanamu, kurudi nyuma na kuishi maisha hayo ambyo yalimwekeza Jahannamu hapo mbeleni? Jinsi gani mtu yeyote, baada ya kufanywa safi kutokana na unajisi wa dhambi, na kuwa hamu ya kurudi katika rindi la uangamizo? Jinsi gani mtu yeyote, anayejua kile Kristo alichokifanya kwa niaba yetu, kuendelea kuishi kana kwamba Yeye si wa muhimu? Jinsi gani mtu yeyote, ambaye ametambua ni kiasi gani Kristo aliteseka kwa ajili ya dhambi zetu, kuendelea kutenda dhambi kana kwamba mateso hayo hayakuwa na maana?

Warumi 6:11-15 inasema, "Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu. Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake; wala dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki; kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema. Katika njia sawa, ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi bali hai kwa Mungu katika Kristo Yesu. Basi, msiruhusu dhambi itawale ndani ya miili yenu ambayo hufa, na hivyo kuzitii tamaa zake mbaya. Wala kutoa sehemu ya mwili wako kwa dhambi, kama vyombo vya uovu, bali jitoeni kwa Mungu , kama wale ambao wamekuwa kuletwa kutoka mauti hadi kwenye uzima ; msiendelni nini basi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chin ya sheria bali chini ya neama? Hasha!

Kwa mwongofu wa kweli, basi, kuendelea kuishi kwa dhambi si chaguo. Kwa sababu uongofu wetu ulisababisha asili mpya kabisa, nia yetu si kuishi tena katika dhambi. Naam, sisi bado twatenda dhambi, lakini badala ya kugaga ndani yake vile tulifanya wakati mmoja, sisi sasa tunaichukia na tunatamani kukombolewa kutoka humo. Wazo la "kuchukua faida " ya sadaka ya Kristo kwa niaba yetu kwa kuendelea kuishi kwa dhambi ni jambo lisiloweza fikirika. Kama mtu anaamini mwenyewe kuwa Mkristo na bado anataka kuishi maisha ya zamani ya dhambi, ana sababu kutia shaka wokovu wake. "Jijaribuni wenyewe kwamba katika imani; jithibitisheni weneyew. Au hamjijui weneyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu?"(2 Wakorintho 13:5).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kama nimeokolewa na dhambi zangu zote zimesamehewa , kwa nini nisieendelee kutenda dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries