settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu hofu?

Jibu


Biblia inataja aina mbili maalum ya hofu. Aina ya kwanza ni ya manufaa na inahimizwa sana. Aina ya pili ni ya hasara na inapaswa kushinda. Aina ya kwanza ya hofu ni hofu ya Bwana. Aina hii ya hofu haimaanishi kuwa na hofu ya kitu fulani. Badala yake, ni hofu ya kumcha Mungu; heshima kwa nguvu zake na utukufu. Hata hivyo, pia ni heshima sahihi kwa ajili ya ghadhabu yake na hasira. Kwa maneno mengine, hofu ya Bwana ni kukiri kwa jumla ya yote Mungu aliye, ambayo huja kwa njia ya kumjua Yeye na sifa zake.

Hofu ya Bwana huleta pamoja nayo baraka nyingi na faida. Ni mwanzo wa hekima na inaongoza kwa uelewa mzuri (Zaburi 111: 10). Wajinga tu hudharau hekima na adabu (Mithali 1: 7). Zaidi ya hayo, hofu ya Bwana inaongoza kwa maisha, pumziko, amani, na ridhaa (Mithali 19:23). Ni chemchemi ya maisha (Mithali 14:27) na hutoa usalama na mahali pa usalama kwa ajili yetu (Mithali 14:26).

Hivyo, mtu anaweza kuona jinsi kumcha Mungu lazima kuhimizwe. Hata hivyo, aina ya pili ya hofu iliotajwa katika Biblia haina faida wakati wote. Hii ni "roho ya woga" iliyotajwa katika 2 Timotheo 1: 7: "Kwa maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi." Roho ya ya woga hautoki kwa Mungu.

Hata hivyo, wakati mwingine sisi uhofu, wakati mwingine hii "roho ya woga"inatulemea, na kuishinda tunapaswa kumwamini na kumpenda Mungu kabisa . "Hakuna hofu katika upendo. Lakini upendo kamili unatoa nje hofu, kwa maana hofu inatumika na adhabu. Mtu mwenye woga hajafanywa mkamilifu katika upendo "(1 Yohana 4:18). Hakuna mtu mkamili, na Mungu anajua hilo.Ndio maana amenyunyiza wazi motisha dhidi woga kwa Bibilia nzima.Kuanzia kwenye kitabu cha mwanzo kuendelea hadi kitabu cha ufunuo ,Mungu anatukumbusha "Msiogope."

Kwa mfano, Isaya 41:10 inatuhimiza, "Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifahdaike, kwa maana mimi ni Mungu wako, nitakutia nguvu, maana nitakusaidia, naam nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu." Mara nyingi tunaogopa ya baadaye na ni nini kitafanyika kwetu. Lakini Yesu anatukumbusha kwamba Mungu anayewajali ndege wa angani, hivyo ni mara ngapi zaidi Yeye atawapa watoto wake? "Msiogope basi, bora niny kuliko mashomoro wengi" (Mathayo 10:31). Aya hizi chache tu hufunika aina nyingi za hofu. Mungu anatueleza kuwa tusiwe na hofu ya kuwa peke yetu, ya kuwa dhaifu mno, ya kutosikika, na kutokana na kukosa mahitaji ya kimwili. Funzo hili linaendelea katika Biblia, likiangazia mambo mengi tofauti ya "roho wa woga."

Katika Zaburi 56:11 mtunzi anaandika, "Nimemtumaini Mungu sitaogopa, mwanadamu atanitenda nini?" Huu ni ushahidi wa kushangaza kwa nguvu ya kumtegemea Mungu. Bila kujali kitakacho tokea, mwana zaburi atamtumainia Mungu kwa sababu yeye anajua na kuelewa nguvu ya Mungu. Ufunguo wa kushinda hofu, basi, ni kuweka matumaini kwa jumla na kamili katika Mungu. Kumtumaini Mungu ni kukataa kujisalimisha kwa hofu. Ni hatua ya kugeuka kwa Mungu hata katika nyakati ngumu na kumwamini kwa kufanya mambo ya haki. Imani hii inatokana na kumjua Mungu na kujua kwamba Yeye ni mzuri. Kama Ayubu alisema alipokuwa akipitia baadhi ya majaribio mangumu sana kumbukumbu katika Biblia, "Tazama ataniua, sina tumaini, ila hata hivyo nitaithibitisha njia yangu mbele yake" (Ayubu 13:15).

Mara tu baada tumejifunza kuweka imani yetu katika Mungu, hatutakuwa tena wa hofu ya mambo ambayo hutujia. Sisi tutakuwa kama mtunga-zaburi aliyesema kwa kujiamini "... nao wote wanaokukimbilia watafurahi, watapiga daima kelele za furaha, kwa kuwa Wewe unawahifadhi, walipendao jina lako watakufurahia" (Zaburi 5:11).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu hofu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries