settings icon
share icon
Swali

Je! Hila za Shetani katika Waefeso 6:11 ni gani?

Jibu


Hila ni ujanja au ulaghai uliobuniwa ili kumdanganya mtu. Hila za Ibilisi ni zile mbinu za ulaghai zinazotumiwa na Shetani ili kutunasa kupitia majaribu, vitisho, au kuogofya. Waefeso 6:11 inatuonya kuwa “Vaeni silaha zote za Mungu ili kwamba mweze kuzipinga hila za ibilis.” Maandiko yanatupa ufahamu juu ya mbinu za adui yetu: “Kwa maana hatuachi kuzijua hila zake” (2 Wakorintho 2:11), na tuko makini kutii maonyo yake.

Hapa kuna baadhi ya hila za Shetani tunazoziona katika Maandiko:

1. Kupinga neno la Mungu. Mwanzo 3 inatupa mtazamo wa kina kwa mbinu hii ya adui yetu. Iiliwaongoza kwa dhambi ya kwanza ya mwanadamu, na Shetani bado anaitumia kwa sababu inafanya kazi vizuri sana. Maneno ya kwanza yaliyorekodiwa ya ibilisi, kupitia kwa nyoka, yalikuwa haya: “Ati kweli Mungu alisema?” (Mwanzo 3:1). Kwa maneno hayo, Ibilisi alimwomba mwanamke huyo afikirie upya yale ambayo alielewa kuwa Mungu alikuwa amesema. Kwa kuongezea ufafanuzi wake wa kibinadamu, alijisadisha kwamba Neno la Mungu likuwa na vizuizi vingi sana.

Kwa kupendekeza kwamba tunapaswa kuchunguza tena fundisho lililo wazi la Neno la Mungu, Shetani hutualika tuongeze tafsiri yetu wenyewe na hivyo kubatilisha mapenzi ya Mungu yaliyotajwa. Madhehebu yote ya kanisa yanaanguka kwa mitego ya hila hizi za Shetani. “Je, kweli Mungu alisema kwamba ngono ya watu wa jinsia moja ni makosa?” anafyoza makanisa yanaanguka. “Je, kweli Mungu alisema kuwa kuna jinsia mbili tu?” anaokeza kutualika sisi kuweka mwelekeo wetu wenyewe kwenye ukweli, tukijifanya mingu badala ya Bwana. Waefeso 6:11 inasema kwamba tunahitaji kuvaa silaha zote za Mungu ili kustahimili hila hizo.

2. Anaswali utambulisho wetu. Luka 4:1-13 inatoa ufahamu katika hila kadhaa za Shetani. Shetani alimjia Yesu ili amjaribu nyikani. Katika matukio mawili, Shetani alianza majaribu yake kwa maneno haya: “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu.” Shetani alijua kabisa Yesu alikuwa nani (Marko 1:34). Yesu alikuwa pale Shetani alipoanguka “kutoka mbinguni kama umeme wa radi” (Luka 10:18). Shetani alichagua wakati mwafaka ambapo Yesu alikuwa mdhaifu kimwili na mwenye njaa ili kujaribu utambulisho Wake.

Shetani hufanya vivyo hivyo kwetu. Ili kufanya hila zake kuwa na ufanisi zaidi anatupiga wakati wa shida au pambano la kiroho na kupendekeza, “Kama ungekuwa mtoto wa Mungu, hili lisingekutokea. Ikiwa kweli ungekuwa Mkristo, Mungu angekusaidia sasa hivi.” Pia, tunahitaji “chapeo ya wokovu” iliyo imara ili kustahimili mashambulizi haya dhidi ya utambulisho wetu na tabia ya Mungu (Waefeso 6:17).

3. Kuyageuza Maandiko. Ujanja mwingine Shetani aliutumia dhidi ya Yesu ni kunukuu Maandiko, lakini kwa kuyageuza. Katika Luka 4:10-11, Shetani anakukuu Zaburi 91:11-12 katika jitihada za kumshawishi Yesu kutenda katika mwili badala ya kumfuata Roho (ona Wagalatia 5:16, 25). Lakini Shetani alishindwa kukamilisha wazo la zaburi hiyo. Mstari unaofuata, Zaburi 91:13 unasema, “Utawakanyaga simba na nyoka wakali, simba mkubwa na nyoka utawaponda kwa miguu.” Marejeleo haya ya Wanyama ni mafumbo ya maadui wakali na hatari-ni Shetani anafananishwa na simba na nyoka katika Maandiko (Mwanzo 3:15; Ufunuo 20:2; 1 Petro 5:8; linanganisha Warumi 16:20). Maana ya kweli ya kifungu katika Zaburi 91 ni kwamba Mungu atawalinda na kuwatia nguvu watumishi Wake wanapomshinda adui, Shetani. Moja ya hila za Shetani ni kuacha sehemu muhimu za Maandiko ili kupotosha maana yake ili kukamilisha lengo lake.

Tunaona hila hizi za Shetani zikitenda kazi siku hizi, kama walimu wa mafanikio na manabii wa uongo wanavyonukuu Maandiko kwa njia za ubinafsi na za kupotosha. Wanatumia Neno la Mungu vya kutosha ili kusikika kuwa na mamlaka, lakini wanalipindisha ili kuambatana na ajenda zao za kibinafsi. Kutumia mistari nje ya muktadha au mistari hiyo tu inayothibitisha chochote tunachotaka kuamini au kufanya ni tatizo lililoenea, na kuwashiriki wengi hawajui kuwa wameanguka katika moja wapo ya hila za Shetani.

4. Kutoa njia mbadala inayojaribu badala ya utiivu. Mpango mwingine au hila ya Shetani iliyotumiwa katika jaribu la Yesu ilikuwa kupendekeza njia nyingine, kuepuka utii mkali kwa mapenzi ya Mungu. Kwa ujanja Shetani alijua vizuri zaidi kuliko kupendekeza kwamba Yesu asahau mpango mzima wa wokovu na arudi mbinguni. Badala yake, alitoa njia mbadala. Katika Luka 4:5-7, “Ibilisi akampeleka hadi juu ya mlima mrefu akamwonyesha milki zote za dunia kwa mara moja. Akamwambia, “Nitakupa mamlaka juu ya milki hizi na fahari zake zote, kwa maana zimekabidhiwa mkononi mwangu nami ninaweza kumpa yeyote ninayetaka. Hivyo ikiwa utanisujudia na kuniabudu, vyote vitakuwa vyako.” Jaribio hili lililenga ubinadamu wa Mwana wa Adamu. Sasa Yesu alijua jinsi mtu anavyohisi kuwa katika mwili. Alijua jinsi miiba ingehisi katika mikono na miguu Yake. Alijua kukataliwa na kudhihakiwa kungekuwaje wakati Alipovuliwa nguo na kupitishwa mbele ya umati. Shetani alikuwa anajaribu kumpa maafikiano. Je! ikiwa Yesu angewea “kuuokoa ulimwengu” bila kuteseka kwa kusulubiwa? Je! kama ikiwa angechukua njia ya mkato na kumiliki falme zote za ulimwnegu sasa?

Moja wapo ya hila laghai zaidi za Shetani inahusisha uwezo wake wa kutoa maafikiano yaliyochafuliwa na dini. Anajua hawezi kuja kwa waumini waliokomaa na mashambulizi ya moja kwa moja juu ya maadili na imani zao. Kwa hiyo anaingililia mlango wa nyuma, akijifanya kuwa rakiki mwenye njia mbadala inayofaa: “Naam, nidyo, huenda ikawa ni makosa kwa kuishi na mpenziwe, lakini unaweza kumhubiria vizuri zaidi anapokutazama jinsi unavyoishi katika imani yako.” Au hili: Huitaji kwenda kanisani ili uwe wa kiroho. Unaungana vyema na Mungu peke yake msituni. Hao watu wote ni wanafaiki, na nyinyi ni waadilifu mno kutoshirikiana nao.” Ni lazima tujihadhari na hila za Shetani anapotoa kitu kingine isipokuwa utiifu kamili kwa mapenzi ya Mungu.

Waandishi wa Agano Jipya mara nyingi walionyesha hila za Shetani kwa wale waliokuwa kanisani ambao walikuwa wakianguka kwa ajili yao, na tunapaswa kuzingatia. Kuwepo kwa manabii wa uongo (1 Timotheo 6:3-5), wachuuzi (1 Petro 4:15), wazinzi (1 Timotheo 1:9-10), na walaghai (Ufunuo 2:20) zote ni sehemu ya mpango mkuu wa Shetani kudhoofisha kanisa kutoka ndani.

Ili kupambana na hila za Shetani, wafuasi wa Kristo lazima wakae wakiwa wemevaa silaha za Mungu. Ni lazima tukae ndani ya Neno lake ili tutambue udanganyifu wowote. Na tunapotambua kuwa tumeshikwa na hila za Shetani, ni lazima tutubu upesi na kutafuta uwajibikaji wa kimungu. Zaburi 37:23-24 inawatia moyo wale wanaotamani kuishi maisha ya kimungu: “Kama Bwana akipendezwa na njia ya mtu, yeye huimarisha hatua zake, ajapojikwaa, hataanguka, kwa maana Bwana humtegemeza kwa mkono wake.” Wakati Bwana anatushika mkono, hila za Shetani haziwezi kutudhuru.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Hila za Shetani katika Waefeso 6:11 ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries