settings icon
share icon
Swali

Je! inamaanisha nini kwamba ni bora kuoa kuliko kuwaka tamaa katika 1 Wakorintho 7:9?

Jibu


Wakorintho wa Kwanza 7:8-9 inasema, “Kwa wale wasiooa na kwa wajane, nasema hivi, ingekuwa vizuri wasioe. Lakini kama hawawezi kujizuia, basi waoe na kuolewa, kwa maana ni afadhali kuoa au kuolewa kuliko kuwaka tamaa.” Paulo anasema kwamba, ingawa useja ni kupendelea kwake, sio makosa kuoa. Kwa kweli, kwa wale walio na tamaa kali ya ngono, ni afadhali waoe kuliko kuchochewa na tamaa isiyotosheleka

Kauli ya Paulo kwamba ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa yanaunga mkono msimamo thabiti wa Biblia dhidi ya uasherati: ikiwa wenzi ambao hawajafunga ndoa wanawaka tamaa kwa wao wenyewe, wanahitaji kufunga ndoa, na wala sio kuanguka katika dhambi. Wengi hujaribu kutetea ngono kabla ya ndoa kwa visingizio kama vile “tumeposana” au “tunapendana.” Lakini Biblia hairuhusu mambo hayo. Katika 1 Wakorintho 7:1-2, Paulo anazungumzia tofuati kati ya waliofunga ndoa na wale ambao hawajaoa na kusema kwamba utimilifu wa ngono ni sababu kuu ya ndoa: “Basi kuhusu mambo yale mliyoyaandika: Ni vyema mwanaume asimguse mwanamke. Lakini ili kuepuka zinaa, kila mwanaume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.” Ndoa ni mpango wa Mungu wa kutimiza tamaa za ngono, na uhusiano wowote wa ngono nje ya ndoa ni dhambi (Waebrania 13:4).

Tamaa za ngono huchipuka wakati wa kubalehe na kuongezeka kadri mwili unavyokua. Tamaa za ngono zenyewe sio mbaya. Hizo ni sehemu ya kukua kuwa mwanaume au mwanamke mwenye afya. Tanachofanya kuhusu tamaa hizo huamua kama zinaongoza kwenye dhambi au la. Yakobo 1:13-15 inaeleza kuendelea kutoka kwa jaribio hadi kwa dhambi yenyewe: “Mtu anapojaribiwa asiseme, “Ninajaribiwa na Mungu.” Kwa maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu wala yeye hamjaribu mtu yeyote. Lakini kila mtu hujaribiwa wakati anapovutwa na kudanganywa na tamaa zake mwenyewe zilizo mbaya. Basi ile tamaa mbaya ikishachukua mimba, huzaa dhambi, nayo ile dhambi ikikomaa, huzaa mauti.”

Kwa dai lake kwamba ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa, Paulo anatoa onyo kwa wale walionaswa katika mwenendo wa dhambi. Uchumba wa muda mrefu, uchumba wa vijana, matukio ya “ngono” kati ya wale wanaochumbiana zote ni njia ambazo majaribu yanaweza kuanza “kuwaka” miongoni mwao. Wathesalonike wa Kwanza 4:3-7 pia inazungumzia haja ya kudhibiti tamaa zetu: “Mapenzi ya Mungu ni kwamba ninyi mtakaswe, ili kwamba mjiepushe na zinaa, ili kwamba kila mmoja wenu ajifunze kuutawala mwili wake mwenyewe katika utakatifu na heshima, si kwa tamaa mbaya kama watu wa Mataifa wasiomjua Mungu. Katika jambo hili mtu asimkosee ndugu yake wala kumlaghai. Kwa kuwa Bwana ni mlipiza kisasi katika mambo haya yote, kama vile tulivyokwisha kuwaambia mapema na kuwaonya vikali. Kwa maana Mungu hakutuitia uchafu, bali utakatifu.”

Tunapokataa kutawala miili yetu kwa njia ambazo ni takatifu na zenye heshima, tuko katika hatari ya kuruhusu msukumo wa asili wa ngono kugeuka kuwa tamaa— au kusababisha mtu mwingine kujazwa na tamaa. Hii ni kweli hasa wakati wa ujana wa ubalehe wa miaka ya mapema ya ishirini wakati homoni zinapokuwa na nguvu na miili yenye nguvu. Tamaa ya ngono iko kwenye kilele chake, na wapumbavu au wasiofundishwa mara nyingi huingia kwenye dhambi ya ngono kabla ya kutambua madhara ya muda mrefu. yote. Mpango wa Mungu ni kwa wale ambao “wanawaka” na hamu ya ngono kutafuta mwenzi wa ndoa kwa maombi na kudhibiti tamaa yao hadi usiku wa harusi. Wale wanaoweza kudumisha usafi wa kiadili hawapaswi kuhisi kulazimishwa kufunga ndoa. Useja ni mtindo wa maisha unaokubalika kabisa. Lakini, ikiwa mtu anaanza “kuwaka” kwa shauku, ni wakati wa kutafuta mwongozo wa Mungu katika kutafuta mwenzi.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! inamaanisha nini kwamba ni bora kuoa kuliko kuwaka tamaa katika 1 Wakorintho 7:9?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries