settings icon
share icon
Swali

Je! umuhimu wa hekalu la Ezekieli ni gani?

Jibu


Ezekieli alizaliwa katika ukoo wa ukuhani (Ezekieli 1:3), lakini alimtumikia Mungu kama nabii. Katika Ezekieli 40-48, Ezekieli anaona maono ya kina kuhusu hekalu kuu na tukufu. Maono haya pana yamekuwa mada ya kisio na tafsiri tofauti mbalimbali kwa miaka sasa.

Ezekieli alianza huduma yake ya unabii kabla ya Yerusalemu na hekalu kuharibiwa na Wababeli kitika mwaka wa 586 Kabla Kristo Azaliwe. Kabla ya kuharibiwa, manabii wengi wa uwongo waliwahakikishia watu kwamba Mungu alikuwa pamoja nao na kwamba hakuna jambo baya litawatendekea (Ezekieli 13:8-16). Manabii wa kweli kama Yeremia na Ezekieli waliwaonya watu kuwa hukumu ya Mungu ilikuwa inakuja (Ezekieli 2:3-8). Katika Ezekieli 8-11, nabii anaona utukufu wa Mungu ukiondoka hekalu.

Katika uhamishoni, aliwatia moyo Waisraeli kwamba hukumu haitadumu milele, na kwamba Mungu atarejesha Israeli na kuishi miongoni mwao mara nyingine tena. Katika Ezekieli 37 anasimulia ono la “Bonde la Mifupa Mikavu,” ambamo anaeleza kuunganishwa na kuhuishwa kwa Israeli iliyokufa. Katika sura ya 38-39, Ezekieli anatabiri vita vya Gogu na Magogu, ampapo maadui wa Israeli watashindwa. Kisha, katika sura za 40-48, Waisraeli wakiwa mwaka wa ishirini na tano uhamishoni, Ezekieli anaelezea hekalu kubwa sana (sura 40-42). Utukufu wa Mungu unarejea (sura 43), dhabihu zinarudiwa tena (sura 44-46), na nchi inarejeshwa kwa watu wa Israeli (47-48). Nyoyo za watu zitakuwa zimefanywa upya (Ezekieli 36:26-27), na hata watu wa Mataifa watakuwa na nafasi katika ufalme uliorejeshwa (Ezekieli 47:22). Nchi itatawaliwa na mwana wa Ufalme kama Daudi (Ezekieli 44:3; angalia pia 37:24-25; 34:23-24).

Katika maono yake ya hekalu, Ezekieli anachukuliwa hadi Israeli ambako anaona mlima na jiji. Anakutana na “mtu ambaye kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwa shaba” (Ezekieli 40:3). Huyu mtu anamwambia Ezekieli azingatie kwa uangalifu kwa kila jambo analoliona na kusikia na kuwaelezea yote kwa upana na urefu watu wa Mungu (aya ya 4). Kiwango cha jengo la hekalu linaangaziwa katika sura zinazofuata tatu za Ezekieli.

Swali ni, je! lini maono ya hekalu la Ezekieli yatatimia? Je! Tunastahili kuangalia utimilifu wake kihalisi? Ama, ono hili ni mfano wa uwepo kamili wa Mungu miongoni mwa watu wake? Je! Maono haya yametimia? Ama utimilifu wake utakua siku za usoni? Ikiwa hekalu la Ezekieli ni la usoni, je! Litatimizwa wakati wa kipindi cha kanisa, cha milenia, au katika hali ya milele? Majibu ya maswali haya yataamuliwa haswa na dhamira ya mfasiri kuhusiana na hali halisi au kiishara ya unabii na utimizo wake.

Majibishano ya kuunga mkono kuwa unabii wa hekalu la Ezekieli ushatimia ni utele wa maelezo ya maono ya Ezekieli na vipimo halisi vya hekalu. Ikiwa maono yanatimizwa kihalisi, basi utimilifu wake utakua usoni, kwa sababu hakuna jambo lolote kama lile ambalo limeelezewa katika Ezekieli 40-48 lishatoke hadi wakati huu. Vipimo vya hekalu la Ezekieli ni vikubwa mno kuliko vile vya hekalu la wakati wa Yesu, na kuwa hekalu hilo lilikuwa jengo kubwa sana.

Wengi wa wale wanaotarajia utimizo wa hasa wa hekalu la Ezekieli wanatarajia kwamba kusimamishwa kwa hekalu hili utakuwa wakati wa ufalme wa milenia, miaka 1000 ya kutawala kwa Kristo katika ulimwnguni. Wakati wa kipindi cha milenia, watakatifu watutukuka kutoka wakati wa sasa wataishi pamoja na mwanadamu wa kawaida ambaye bado atahitaji kufanya uamuzi kwa ajili ya Kristo ili waokolewe- na wengi watachagua kutomwamini Yeye. Mfumo wa dhabihu unaoelezewa katika Ezekieli hauwezi kuwa ule wa ondoleo la dhambi, kwa kuwa Kristo ashatimiza hilo mara moja na kwa ajili ya wote (Waebrania 10:1-4, 11-14). Mtazamo wa njia hii huwa unaona dhabihu kuwa ukumbusho wa kifo cha Kristo au kama ibada za utakaso katika hekalu, lakini sio kuwa ni njia ya msamaha wa dhambi.

Katika mtazamo wa kitamathali wa hekalu la Ezekieli, maono ya nabii huyo yanarudia kauli kwamba Mungu mara nyingine tena atadumu na watu wake katika uhusiano kamilifu. Uhusiano huu umeelezewa katika lugha ambayo watu wa siku zile (haswa Ezekieli kama kuhani) wangeelewa- hekalu la Kiyahudi tukufu kadri, kukiwa na dhabihu kamili za mara kwa mara, na Masihi akihudumu, na utukufu wa Mungu ukionekana ukiwa Dhahiri. Katika maono ya baadaye kwa nabii, Mungu alifunua zaidi jinsi atakavyo timiza haya, Yesu mweyewe akichukua nafsi ya hekalu, dhabihu na nchi. Uwepo wa Mungu kupitia kujazwa kwa Roho Mtakatifu utakuwa dhihiri kuliko hapo awali. Utimizo wa hekalu la Ezekieli basi utatimizwa katika wakati wa kanisa kwa kiwango fulani na katika wakati ujao, kwa ukamilifu.

Haijalishi ni mtazamo gani umechukilwa, maono ya hekalu la Ezekieli yasema kuwa Mungu hajawatekeleza watu wake na kwamba uhusiano Wake nao utarejeshwa na kuinuliwa kiwango ambacho utukufu na uhusiano wake havijawai tokea hapo mbeleni. Hali zilizoko sasa hazipaswi kamwe kumfanya mtu kutilia shauku ahadi za Mungu.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! umuhimu wa hekalu la Ezekieli ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries