settings icon
share icon
Swali

Je! Mungu anakublia mume na mke kufanya mapenzi wakati mke yuko kwenye hedhi/akiwa katika siku zake za hedhi?

Jibu


Walawi 15:19 inasema, “Ikiwa mwanamke atatokwa na damu ya kawaida ya mwezi, atakuwa najisi kwa siku saba, na yeyote atakayemgusa atakuwa najisi mpaka jioni.” Vivyo hivyo, Walawi 15:24 yasema, “Ikiwa mwanaume atalala naye na ile damu ya mwezi ikamgusa, atakuwa najisi kwa siku saba; kitanda chochote atakachokilalia huyo mwanaume kitakuwa najisi.” Hatimaye, andiko la Walawi 20:18 linasema hivi: “Ikiwa mwanaume atalala na mwanamke aliye katika hedhi yake na kukutana naye kimwili, amefunua mtiririko wa hedhi yake, naye huyo mwanamke amejifunua uchi wake. Wote wawili lazima wakatiliwe mbali na watu wao.” Kwa sababu ya Maandiko hayo, wengine hushikilia kwamba wenzi wa ndoa hawapaswi kufanya ngono mke ako katika hedhi.

Tatizo la maoni hayo ni kwamba Maandiko yakitumiwa mfululizo, hata kumgusa mwanamke ambaye ana mtiririko wake wa hedhi kungekatazwa. Zaidi ya hayo, kulingana na Walawi 15:20-23, hata kugusa kitu ambacho mwanamke amekigusa kungekatazwa. Je, sheria hizi zinatumika kwetu hii leo? La, hasha. Ni kwa nini? Ni muhimu kukumbuka kusudi la sheria za Agano la Kale kuhusu damu. Katika mfumo wa dhabihu, damu ilikuwa takatifu (Walawi 17:11). “Uchafu” wa mwanamke wakti wa hedhi ulikuwa ishara ya thamani iliyowekwa kwenye damu. Kwa hiyo, kushiriki na mwanamke ambaye alikuwa katika kipindi cha hedhi kulikatazwa.

Wakristo hii leo hawako chini ya sheria ya sherehe za Agano la Kale (Warumi 10:4; Wagalatia 3:24-26; Waefeso 2:15). Hakuna tena mfumo wa dhabihu. Dhabihu ya damu ya Yesu ililipa ahdabu ya dhambi mara moja na kwa wakati wote. Sheria za sherehe za Walawi hazitumiki hii leo. Hakuna sababu ya kibiblia ni kwa nini wanandoa hawawezi kufanya ngono wakati wa kipindi cha hedhi kwa mke. Madaktari wengine hawapendekezi kufanya ngono wakati wa hedhi kwa sababu ya mtazamo wa matibabu, lakini hakuna “hatari” iliyothibitishwa ya kujamiiana wakati wa kipindi cha hedhi. Kawaida wanawake hawana hamu ya kufanya ngono wakati wa hedhi, kwa hivyo hilo ni jambo linguine la kuzingatia. Kimsingi, suala hili lazima liamuliewe na mume na mke katika roho ya “makubaliano ya pande zote mbili” kama vile 1 Wakorintho 7:5 inavyoeleza.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mungu anakublia mume na mke kufanya mapenzi wakati mke yuko kwenye hedhi/akiwa katika siku zake za hedhi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries