settings icon
share icon
Swali

Guff ni nini?

Jibu


Guff ni neno ambalo kitabu cha sharia na maadili ya Kiyahudi (Talmud) hutumia kurejelea hazina ya nafsi zote ambazo hazijazaliwa. Talmud ni mafundisho ya Kiyahudi juu ya Torati au Agano la Kale, na hasa vitabu vya kwanza vitano vya Biblia vinavyojulikana kama Torati. Tamaduni za Kiyahudi zinasema kwamba Talmud ilianza kama mafundisho simulizi yaliyotolewa na Musa ambayo hatimaye yalikamilishwa wakati fulani kati ya karne ya nne na ya pili Kabla ya Kristo kuzaliwa.

Kwa halisi, neno guff linamaanisha “mwili.” Kimsingi Talmud inasema, “Masihi hatafika hadi wakati hakutakuwa na nafsi katika guff.” Talmud inasema kwamba kuna idadi fulani ya nafsi mbinguni ambazo zinangoja kuzaliwa. Zinangoja katika hazina ya mbinguni inayoitwa “guff”, hadi wakati zitakapozaliwa na Masihi hatafika hadi wakati kila moja ya nafsi hizi zitazaliwa katika ulimwengu wa kawaida.

Je, dhana ya guff ni ya kibliblia? Hapana. Maandiko ya Kiebrania wala Agano Jipya hayafundishi kwamba kuna hazina ya nafsi mbinguni. Biblia haifundishi kwamba nafsi zinangoja kuunganishwa na miili wakati wanapozaliwa. Biblia haielezi wazi kuhusu au jinsi nafsi za binadamu zinaumbwa lakini dhana ya guff haikubaliani na ile ambayo Biblia inafunza kuhusu asili ya nafsi. Ni jambo la kibiblia kushikilia kwamba Mungu huumba kila nafsi ya binadamu wakati wa mtungo mimba au nafsi ya binadamu unaundwa pamoja na nwili kupitia muungano wa kimwili na kiroho wa kutungwa mimba.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Guff ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries