settings icon
share icon
Swali

Hawara ni nani? Kwa nini Mungu aliruhusu wanaume wawe an masuria katika Biblia?

Jibu


Katika Biblia, suria ni mwanamke anayeishi na mwanamume kana kwamba ni mke, lakini bila kuwa na hadhi kamili za mke. Masuria katika enzi ya wazee wa ukoo na zaidi ya hapo walikuwa na cheo cha chini—walikuwa wake “wa pili.” Suria hakuweza kuolewa na bwana wake kwa sababu ya hali yake ya mtumwa, ingawa, kwake, uhusiano huo ulikuwa wa kipekee na unaendelea. Hapo kale, inaonekana kwamba masuria walitumiwa kuzaa watoto kwa wanaume ambao wake zao walikuwa tasa (ona Mwanzo 16:1-4). Baadaye, inaonekana kwamba masuria waliwekwa kwa ajili ya kujifurahisha tu kingono (ona 2 Mambo ya Nyakati 11:21). Masuria katika Israeli walikuwa na baadhi ya haki sawa na wake halali, bila heshima sawa.

Ingawa ni kweli hakuna mahali ambapo Biblia inashutumu usuria kwa uwazi, shutumu inonekana kwa njia isiyo wazi tangu mwanzo wa wakati. Kulingana na Mwanzo 2:21-24, nia ya awali ya Mungu ilikuwa ndoa iwe kati ya mwanamume mmoja na mwanamke mmoja, na hilo halijabadilika kamwe (Mwanzo 1:27). Kwa hakika, uchunguzi wa maisha ya wanaume kama Mfalme Daudi na Mfalme Sulemani (aliyekuwa na masuria 300; 1 Wafalme 11:3) unaonyesha kwamba matatizo yao mengi yalitokana na mahusiano ya mitala (2 Samweli 11:2-4).

Biblia haielezi kamwe kwa nini Mungu aliruhusu wanaume kuwa na Masuria. Aliruhusu talaka na mitala, pia, ingawa hakuna kati ya haya yalikuwa sehemu ya mpango Wake wa asili wa ndoa. Yesu alisema Mungu aliruhusu talaka kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya wanaume (Mathayo 19:8). Tunaweza kudhani ugumu uleule wa moyo ulisababisha kuoa wake wangi na masuria.

Tunaweza pia kukisia sababu kulingana na utamaduni wa siku hizo. Wanawake ambao hawajaolewa katika nyakati za kale walikuwa wakiwategemea kabisa wanafamilia zao, kama vile baba zao, kaka zao, n.k. Ikiwa kwa sababu fulani mwanamke hakuwa na wanafamilia au mume wake alikufa au kumtaliki, angeachwa na chaguzi chache kushi. Wanawake wengi katika nyakati za kale hawakuwa na elimu na ujuzi katika biashara. Kujiruzuku ilikuwa ngumu sana, na walikuwa hatarini kwa wale ambao wangewavamia. Kwa wanawake wengi walio katika hali mbaya, kuwa suria lilikuwa chaguo linalofaa zaidi kuliko ukahaba, ukosefu wa makao, au kifo. Angalau suria angepewa nyumba na kupewa utunzaji kiwango fulani.

Inaonekana kuwa Mungu aliruhusu dhambi ya suria, kwa sehemu, kuwaandalia wanawake wenye mahitaji, ingawa kwa hakika haikuwa hali nzuri. Dhambi haifai kamwe. Wakristo wanapaswa kukumbushwa kwamba, kwa sababu Mungu anaruhusu dhambi kwa muda fulani, haimaansihi kwamba Mungu anapendezwa nayo. Simulizi nyingi za Biblia zinafundisha kwamba Mungu anaweza kuchukua kile ambacho watu fulani wananuia kuwa uovu na kukitumia kwa wema (k.m., Mwanzo 50:20).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Hawara ni nani? Kwa nini Mungu aliruhusu wanaume wawe an masuria katika Biblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries