settings icon
share icon
Swali

Je! Inamaanisha nini kuwa hata pepo wanaamini (Yakobo 2:19)?

Jibu


Yakobo 2:14 inaanza mjadala wa imani bila matendo na inajumuisha hoja wazi ya Yakobo kwamba hata pepo huamini na kutetemeka (Yakobo 2:19). “Imani” ya mapepo haina faida, hata kama wanatetemeka kwa kile wanakijua ni kweli. Watu wanaosema “wanamwamini” Mungu huku hawaonyeshi ushahidi wowote katika imani ina kiwango sawia na “itikadi” ya mapepo.

Yakobo anaonyesha manufaa ya matendo katika kuonyesha rehema (Yakobo 2:13) kwa kuuliza itafaa nini ikiwa mtu atadai kuwa na imani lakini hana matendo na kuuliza swali balagha kama hiyo imani yaweza kumwokoa (Yakobo2:14). Ikiwa imani haiambatanishwi na matendo, haiwezi kumkomboa mtu kutoka kwa mahitaji yake, hasa katika hali ya kaka au dada aneyehitaji chakula (Yakobo 2:15). Ikiwa mtu aliye na imani hatakidhi hitaji hilo, watu wenye hitaji watasalia na hitaji hilo (Yakobo 2:16). Imani hiyo yenyewe imekufa-haifai kumkomboa mtu kutoka katika hitaji (Yakobo 2:17).

Yakobo anatoa nadharia tete katika Yakobo 2:18: mtu anaweza kupendekeza kuwa watu wanaonyesha imani yao katika njia tofauti (wengine kwa matendo na wengine bila matendo). Yakobo anapinga dhana tete, akiwakumbusha wasomaji wake kwamba imani bila matendo haina maana (Yakobo 2:20). Kabla afanye kauli hiyo ya ubatili wa imani bila matendo, Yakobo anazungumza na wale walio na dhana tete katika mfano wake (hii inaonyeshwa kwa matumizi yake ya kiwakilishi nomino katika uchache, ingawa wakati anapohutubia wasomaji wake anakitumia katika hali ya wingi). Yakobo anawapa changamoto wale wanaoamini kwamba Mungu ni mmoja: hata mapepo wanaamini hivyo- na wanatetemeka (Yakobo 2:19). Mapepo hawabadilishi tabia yao-hawatimizi mahitaji au kuwa na huruma kwa wengine- licha ya ufahamu wao wa kuwa Mungu ni nani.

Katika kutaja kwamba hata mapepo wanasadiki baadhi ya mambo kumhusu Mungu, Yakobo anadokeza kwamba aliye na imani na haionyeshi kwa matendo katika hali ya vitendo hana manufaa zaidi kuliko yale ya mapepo. Imani ya mtu haiwezi wakomboa wengine kutokana na mahitaji yao, bali matendo hufanya hivyo(Yakobo 2:16). Imani ya mtu haitoi huruma kwa mtu, bali matendo hufanya hivyo (Yakobo 2:13). Yakobo anaendelea zaidi kuwakumbusha wasomaji wake, ambao tayari amewatambulisha kuwa ndugu walio na imani katika Kristo Yesu (Yakobo 2:1), kwamba Abrahamu alihesabiwa haki kwa matendo wakati alimtoa Isaka kama dhabihu (Yakobo 2:21), na kwamba wakati Abrahamu alichukua hatua hiyo, Maandiko yalitimizwa yaliyosema Abrahamu alihesabiwa haki kwa imani yake katika Mungu (Yakobo 2:23, ikinukuu Mwanzo 15:6).

Yakobo anafahamu vyema kwamba Abrahamu alikuwa amehesabiwa haki kwa imani (katika Mwanzo 15:6) zaidi ya muongo mmoja kabla amtoe Isaka kama dhabihu (Mwanzo 22). Abrahamu alikuwa ametangazwa kuwa mwadilifu na Mungu muda mrefu kabla ya tendo hilo la dhabihu, na Paulo anathibitisha kwamba Abrahamu alihesabiwa haki kwa imani yake (Warumi 3:28-5:1) na wala sio kwa matendo. Kwa hivyo, Yakobo anazungumza waziwazi kuhusu aina tofauti ya kuhesabiwa haki; wakati anarejelea dhana kwamba mapepo wanaamini na kutetemeka (Yakobo 2:19), Yakobo hazungumzii kuhusu kuhesabiwa haki mbele za Mungu (au Mungu kumtangaza mtu kuwa mwadilifu). Badala yake, anazungumzia juu ya haki iliyo dhahiri au uadilifu wa manufaa ambao watu waneza kuuona, uadilifu ambao unaonyesha rehema (Yakobo 2:13) na unatimiza mahitaji (Yakobo 2:16). Yakobo anazungumzia kuhusu kuhesabiwa haki mbele ya watu-akipendekeza kwamba mtu hawezi kuonyesha imani (kwa watu) bila matendo mema (Yakobo 2:18).

Yakobo anaongeza kuwa itakuwa ni upumbavu sana kufikiri kwamba mtu anaweza onyesha imani bila matendo (Yakobo 2:20). Ikiwa Yakobo anarejelea kuhesabiwa haki n Mungu badala ya kuhesabiwa haki mbele ya binadamu, basi yeye na Paulo wanapingana moja kwa moja (linganisha Yakobo 2:24 na Warumi 3:28). Muktadha wa Paulo unazingatia jinsi mtu anavyokuwa mwadilifu mbele za Mungu (Warumi 3:28), na Yakobo anajadili jinsi mtu anauweka uadilifu huo katika matendo. Tunaonyesha imani yetu kwa watu wengine kwa kuwaonyesha huruma (Yakobo 2:13) na kukidhi mahitaji yao (Yakobo 2:16).

Mapepo huamini na kutetemeka (Yakobo 2:19),ilhali hawaonyeshi watu huruma au kukidhi mahitaji yao-ufahamu wao wa Mungu hauonyeshi kuwa mtu amebadilika kitabia. Yakobo anatarajia mengi kutoka kwa wale ambao ni ndugu na wamemwamini Yesu Kristo (Yakobo 2:1).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Inamaanisha nini kuwa hata pepo wanaamini (Yakobo 2:19)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries