settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu haki za watoto?

Jibu


Hadi karne ya ishirini, dhana ya haki za watoto haikutiliwa maanani sana. Watoto walikuwa kimsingi mali ya wazazi, au wakati mwingine, walifikiriwa kuwa watu wazima na kutumwa kufanya kazi katika viwanda na katika mashamba. Mnamo 1924, Umoja wa Mataifa ulipitisha mkataba unaoitwa Azimio la Haki za Mtoto, na tangu wakati huo, majaribio mengi yamefanywa na mashirika ya ulimwenguni kote kama vile UNICEF, pamoja na mataifa binafsi, kufafanua na kudumisha haki za watoto.

Biblia haina mengi ya kusema kuhusu haki za watoto, badala yake inaelekeza maagizo kwa wazazi kuhusu malezi ya watoto wao. Waefeso 6:4 inasema, “Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana.” Haki nyingi za watoto zimewekwa ndani ya amri hiyo, lakini lengo lake sio kwa mtoto, bali kwa mzazi. Mungu huwapa wazazi amri kali kuhusu kuwalea watoto wao na huwapa wazazi wajibu wa kufuata amri hizo (Kumbukumbu 6:1-2). Hata watoto wanapokuwa wakubwa, Mungu anatazamia wazazi waweke mipaka ikiwa wanaweza kufanya hivyo. Katika 1 Samueli 3:13, Mungu alimkemea kuhani Eli kwa sababu wanawe watu wazima walikuwa waovu na walifanya mzaha katika nyumba ya Mungu. Eli alijua jambo hilo lakini hakuwazuia.

Ingawa wazo la haki za watoto kuwa dhamana inayolindwa kisheria linaweza kuwa zuri, jambo halisi linaweza kuwa mbaya. Ikiwa “haki za watoto” zinajumuisha haki ya kutofundishwa nidhamu, basi fedheha na aibu ziko pembeni: “Fimbo ya maonyo hutia hekima, bali mtoto aliyeachiwa bila maonyo humwaibisha mama yake” (Mithali 29:15). Watetezi wengi wa haki za watoto wanataka haki hizo kuchukua nafasi ya haki ya wazazi ya “kumlea mtoto katika njia impasayo” (Mithali 22:6). Matangozo mengi ya haki za watoto yanatupilia mbali haki ya wazazi waliyopewa na Mungu, yakivunja haki ya wazazi za kuwapa nidhamu vile wanaona inafaa, kutoa maagizo ya kidini kulingana na dhamiri, na hata kuelimisha mtoto jinsi wanavyoamini kuwa ni bora kwa mtoto huyo.

Kesi ni nyingi ambapo mahakama, kwa niaba ya mtoto mdogo, imewaadhibu wazazi kwa kutounga mkono upasuaji wa kubadili jinsia, tiba ya homoni, au taratibu zingine za ukeketaji kwa mtoto mdogo, ikitangaza “haki” ya mtoto ya kujiamulia. Ingawa kila mwanadamu lazima atendewe kwa hadhi na heshima kama mtu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:27), “haki” maalum zinazohusu watoto pekee zinapaswa kutazamwa kwa tahadhari.

Badala ya haki maalum, watoto wanapewa maagizo katika Biblia. Mungu anawaagiza watoto “Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa Bwana Mungu wako” (Kutoka 20:12). Katika Waefeso 6:1 na tena katika Wakolosai 3:20, watoto wanaambiwa kuwatii wazazi wao katika Bwana, kwa maana hii ni haki. Tunapaswa kutambua kwamba unyanyasaji wa aina yoyote kamwe haujadokezwa au kukubaliwa katika mamlaka yoyote ya kimaandiko.

Kwa kuwa Mungu ndiye aliyeumba familia na kuwakabidhi wazazi watoto, Anajua vyema ziadi jinsi ya kuwalea (Zaburi 12:3). Watoto wanapolelewa kwa roho ya utii na kufundishwa kuwaheshimu wazazi, wao pia wanakuwa watu wazima bora zaidi. Ni wazazi, sio serikali, ambao wanapaswa kuwajibika kwa watoto, isipokuwa katika hali mbaya ziadi. Mungu aliwapa akina mama na baba watoto, si serikali, haijalishi jinsi mfumo wa mahakama unavyoweza kuwa na nia njema.

Kwa kawaida watoto hawajui au kupendelea kile ambacho kinawafaa zaidi. Wala haiko katika uwezo wa mzazi kutoa “haki” hizi. Kulingana na hati fulani ya haki za watoto, watoto wanaweza kupewa “haki” ambazo haziwezekani. Kwa mfano, mjane nchini Sudan ambaye amepoteza makao yake kwa sababu ya magaidi huenda asiweze kuwapa watoto wake “haki” yao ya kula lishe bora na kitanda kizuri. Je, anavunja sheria kwa kuwapa maganda ya mkate huku wakilala kwenye sakafu ya udongo? Je, utekelezaji wa sheria hizi za haki za watoto una mipaka? Hayo ni maswali yanayostahili kuzingatiwa kwa uzito tunapojaribu kutunga sheria inayomhakikishia kila mtoto haki fulani mbali na wazazi. Biblia haionekani kuunga mkono sheria yoyote kama hiyo na badala yake inawashauri akina mama na akina baba wachukue kwa uzito jukumu lao la mzazi, kwa kuwa Mungu anawawajibisha kwa ajili ya hali njema ya watoto wao.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu haki za watoto?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries