settings icon
share icon
Swali

Giza la kiroho ni nini?

Jibu


Giza la kiroho ni hali ya mtu ambaye anaishi mbalina Mungu. Kitabu cha Agano la Kale cha Isaya, katika kutoa unabii juu ya Masihi, cha zungumza juu ya giza zito la kiroho lililowafunika watu: “Watu wanaotembea katika giza wameona nuru kuu, wale wanaoishi katika nchi ya uvuli wa mauti, nuru imewazukia” (Isaya 9:2). Kifungu hiki kinaonekana tena katika Agano Jipya katika Mathayo 4:16, kutangaza kwamba wale ambao wamemjua Mungu wa Israeli kupitia Mwana wake Yesu Kristo ndio ambao wamekombolewa kutoka katika giza la kiroho na sasa wanatembea katika mwanga wa maisha ya Mungu.

Mtume Yohana alifundisha kwamba Mungu ni nuru: “Huu ndio ujumbe tuliosikia kutoka kwake na kuwatangazia ninyi: kwamba Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza lolote. Kama tukisema kwamba twashirikiana naye huku tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatutendi lililo kweli” (1 Yohana 1:5-6). Na Yesu alitangaza kwamba Yeye ni nuru ya ulimwengu: “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu yeyote akinifuata hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima” (Yohana 8:12).

Kwa hivyo, goza la kiroho linamaana ya kutokuwa na ushirika na Mungu kupitia uhusiano na Yesu Kristo. Giza la kutengwa na Mungu linashindwa kwa njia ya Kristo: “Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu. Nuru hungʼaa gizani nalo giza halikuishinda” (Yohana 1:4-5).

Tangu Adamu na Hawa walipotenda dhambi, wanadamu wameishi katika ulimwengu ulioanguka. Watu wote wanazaliwa katika hali ya kuanguka ya dhambi na kutengwa na Mungu. Mpaka mtu anapozaliwa upya kwa Roho wa Mungu, anaishi katika giza la kiroho. Dhambi huitia giza ufahamu wetu na kuharibu macho yetu ya kiroho, na kutufunika katika giza kubwa: “Lakini njia ya waovu ni kama giza nene; hawajui kinachowafanya wajikwae” (Mithali 4:19). Musa analinganisha hali hii ya dhambi na kutotii na kupapasa-papasa kama “kipofu gizani” (Kumbukumbu 28:29). Rafiki mmoja wa Ayubu asema hivi juu ya wale waliopotea katika giza la kiroho: “Giza huwapata wakati wa mchana; wakati wa adhuhuri hupapasa kama vile usiku” (Ayubu 5:14).

Kuishi katika uasi dhidi ya Mungu na mapenzi Yake ni sawa na kuishi katika giza la kiroho. Bwana alipomwagiza Paulo, alisema, “Nitakuokoa kutoka kwa watu wako na watu wa Mataifa ambao ninakutuma kwao, uyafumbue macho yao ili wageuke kutoka gizani waingie nuruni, na kutoka kwenye nguvu za Shetani wamgeukie Mungu, ili wapate msamaha wa dhambi na sehemu miongoni mwa wale waliotakaswa kwa kuniamini mimi” (Matendo 26:17-18).

Baada ya wokovu, waumini wanakuwa mianga ya nuru ya kiroho ya Kristo: “Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, lakini sasa ninyi ni nuru katika Bwana. Enendeni kama watoto wa nuru” (Waefeso 5:8). Wale ambao wako ndani ya Yesu Kristo wamekombolewa kutoka katika ufalme wa giza: “Kwa maana ametuokoa kutoka ufalme wa giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake mpendwa” (Wakolosai 1:13). Wale ambao wanamkataa Yesu wanakabiliwa na utengano wa milele kutoka kwa Mungu katika “giza jeuzi” (Yuda 1:4-13).

Katika Uyahudi, tabia ya ndani ya mtu na ubora wa maadili hueleweka kuwa zinaonyeshwa kupitia macho. Katika Mathayo 6:22-23, Yesu analinganisha hali ya kimaadili ya nafsi ambayo haizaliwa upya na giza: “Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni nyofu, mwili wako wote utajaa nuru. Lakini kama jicho lako ni ovu, mwili wako wote utajawa na giza. Kwa hiyo basi, kama nuru iliyomo ndani yako ni giza, hilo ni giza kuu namna gani!” wasikilizaji wa Yesu wangeelewa kwamba jicho lenye afya ni lile linalotoa nuru kama vile moyo wenye afya uliofanywa upya hutokeza nuru ya kiroho. Lakini jicho la mgonjwa au la dhambi (au moyo) hufunga mwanga, na kuacha roho katika giza la kiroho.

Mtume Paulo anawaelezea wale walio katika hali ya dhambi kabla ya kumjua Kristo kuwa wana akili iliyotiwa giza, iliyofungwa na mioyo migumu: “Watu hao akili zao zimetiwa giza na wametengwa mbali na uzima wa Mungu kwa sababu ya ujinga wao kutokana na ugumu wa mioyo yao” (Waefeso 4:18).

Wale ambao hawajaamini wanaishi katika giza la kiroho kwa sababu Shetani, mungu wa ulimwengu huu, amepofusha akili zao. Hawawezi kuona nuru tukufu ya injili: “Kwa habari yao, mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo, aliye sura ya Mungu” (2 Wakorintho 4:4).

Giza la kiroho linarejelea yote yaliyo kinyume na nuru ya upendo wa Mungu katika Kristo. Habari njeam ambayo Yesu analeta katika ulimwengu huu ni kwamba nuru Yake-Roho Wake atoaye uzima hufurikisha nuru na maisha katika giza la kiroho ndani ya moyo wa mwenye dhambi. Yule ambaye alifungua macho ya vipofu anaweza pia kututoa katika giza la kiroho. Haijalishi ni giza kiasi gani, nuru ya upendo na ukweli wa Mungu inashinda kila dhambi inayotutenganisha na Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Giza la kiroho ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries