settings icon
share icon
Swali

Eskatolojia ya Kikristo ni nini?

Jibu


Eskatolojia ni utafiti wa kile ambacho Biblia inasema kitatokea nyakati za mwisho. Wengi wanachukulia Eskatolojia kama eneo la theolojia linalopaswa kuepukwa. Kwa kweli, Eskatolojia sio muhimu sana kama fundisho la Sifa za Kristo, au fundisho la wokovu. Hata hivyo, hii haimaanishi kwamba sio muhimu kwa mtazamo wa Kibliblia. Jinsi tunavyoelewa Eskatolojia ina athari ya jinsi tunapaswa kuishi maisha yetu na kile tunachotarajia kufanyika kwa mpango wa Mungu. Mambo muhimu katika Eskatolojia ni:

Je! Ni nini maana unyakuo? Neno "nyakua" haliko katika Biblia. Ijapokuwa dhana hiyo ya Unyakuo inafunzwa katika Maandiko. Kunyakuliwa kwa kanisa ni tukio ambalo Mungu atawaondoa waumini wote kutoka duniani ili afanye njia ya hukumu yake ya haki imwagike duniani wakati wa kipindi cha dhiki.

Je, Unyakuo utatokea lini kuhusiana na Dhiki? Je, Unyakuo utafanyika kabla ya Dhiki, katikati ya Dhiki au mwishoni wa Dhiki?

Kuja kwa Mara ya Pili ina maanisha nini na kuna umuhimu gani? Kwa nini kurudi kwa Yesu Kristo ni muhimu? Je, Yesu atarudi lini? Je, ishara za kurudi kwa Yesu zitakuwa nini?

Je! Milenia ni halisi au ni mfano tu? Utimilifu wa maagano na ahadi nyingi za Mungu inategemea ufalme halisi na wa baadaye. Hakuna msingi dhabiti wa kukana kuelewa halisi kwa ufalme wa milenia na muda wake ambao ni miaka 1,000.

Je, kizazi kilichoshuhudia kubadilika kwa Israeli kama taifa kitakuwa hai katika Ujio wa Pili? Sio sahihi Kimaandiko kufundisha kwamba kizazi kinachoona Israeli ikikuwa taifa pia kitaona Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Hii inaweza kuwa hivyo, lakini Maandiko hayasemi hivyo.

Biblia inaelezea kipindi kigumu cha dhiki katika Ufunuo mlango wa 6-18. Ikiwa unyakuo utatangulia dhiki hii, au itatamatishwa na unyakuo, au kwa hakika iwe imefanyika, mitazamo hii ina ushawishi wa kile tunapaswa kujitayarishia. Eskatolojia inatusaidia kuelewa vifungu vya unabii vya Biblia na jinsi ya kuishi maisha yetu tukitilia maanani kile ambacho Mungu atatenda katika nyakati za mwisho. Kuna mabishano mengi ya Eskatolojia, lakini hio haituondolei jukumu letu la kusoma na kuelewa kile Biblia inafunza kuhusu nyakati za mwisho. Kuelewa Eskatolojia kutandoa woga mwingi tulio nao kuhusu siku za usoni. Mungu wetu ni mkuu, ako na mpango, na mpango huo wote utadhihirika kulingana na mapenzi yake kamili na wakati wake. Hii ni ya kutia moyo ya kutosha kwa wale walio ndani ya Kristo!

Kifungu kuu juu ya Eskatolojia ni Tito 2:13, "huku tukilitazamia tumaini lenye baraka na ufunuo wa utukufu wa Mungu wetu Mkuu, aliye Mwokozi wetu Yesu Kristo."

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Eskatolojia ya Kikristo ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries