settings icon
share icon
Swali

Je, nichague dini ipi inifaayo?

Jibu


Hoteli yeyote inayouza vyakula vitamu-vitamu hutushawishi kwa kuturuhusu kuagiza chakula kile sisi tukipendacho. Baathi ya wauzaji kahawa wanawezajivunia juu ya mamia ya ladha tofauti za Kahawa walizonazo. Hata wakati tununuanapo nyumba au magari, huwa tunatafuta yale yenye sifa tofauti-tofauti ambazo tungetamani ziwepo. Hatuishi tu katika ulimwengu wa chocolate, vanilla au strawberry, kwani mwenye kuchangua ndiye mfalme! Waweza kujitafutia kitu chochote utakacho kulingana na mapenzi yako binafsi au mahitaji yako.

Lakini je, yawekana kupata dini inayoeneda sawa na mapenzi yako binafsi? Je, waonaje kuhusu dini isiyokemea maovu, isiyo weka mahitaji au vikwazo, na ambayo haijafungwa au kuzingirwa na usumbufu mwingi wa vihitajikavyo na visivyo hitajika kufanywa? Dini kama hizo zipo, kama jinsi nilivyo zielezea. Lakini je, dini ni kitu cha kuchagua kama ladha ya ice cream inayokupendeza?

Kunazo sauti nyingi zinazo shindania usikivu wetu, sasa kwa nini mtu amfikirie Yesu zaidi kuliko, sema Muhammad au Confucius (mwana filosofia mashuhuri wa china), Buddha, au Charles Taze Russell (mmoja wa waanzilishi wa mashahidi wa yehova), au Joseph Smith (mwanzilishi ya dini ya kimarekani inayoitwa mormonism)? Kwani si kuna msemo usemao njia zote zinaelekea Mbinguni? Kwani si dini zote ziko sawa? Lakini ukweli ni kwamba, dini zote hazielekei Mbinguni kama jinsi vile njia zote hazielekei Indiana (jimbo la kule Marekani).

Yesu pekee ndiye azungumzaye kwa mamlaka ya Mungu kwasababu ni Yesu pekee aliyeshinda mauti. Muhammad,Confucius, na wengine wote wanaendelea kubadilika kuwa mavumbi makaburini mwao mpaka leo hii. Lakini Yesu, kwa nguvu zake mwenyewe, alitoka kaburini siku tatu baada ya kufa juu ya msalaba wa warumi uliojaa dhiki. Mtu yeyote mwenye uwezo juu ya mauti, anastahili usikivu wetu. Mtu yeyote mwenye uwezo juu ya Mauti anastahili kusikizwa.

Ushuhuda uthibitishao ufufuo wa Yesu ni mwingi na usiopingika. Kwanza, palikuwa na mashahidi zaidi ya mia tano waliomwona Kristo aliyefufuka kwa macho yao wenyewe! Hao ni mashahidi wengi sana. Haiwezekani kupuuzia ushahidi wa watu mia tano. Pia kunalo jambo la kaburi lililokuwa tupu. Maadui zake Yesu wangefanikiwa kwa urahisi sana kuzima habari zote za ufufuo wake kwa kuonyesha mwili wake uliokufa na unao oza, lakini hawakuwa na mwili wowote wa kuonyesha! Kaburi lilikuwa tupu! Je, yawezekana kwa mitume kuuiba mwili wake? Ni vigumu sana, na ili kuhakikisha kuwa hilo halitokei, kaburi lake Yesu lilikuwa limelindwa vilivyo na Askari wenye silaha. Na zaidi, utaona wafuasi wake wa karibu walitawanyika kwa uoga baada ya kukamatwa kwake na kusulubishwa, haingelikuwa rahisi kwa wavuvi waliokuwa wamevunjika moyo na kutishika, kupambana ana kwa ana na askari walio funzwa,na wenye ujuzi. Ukweli wa mambo nikwamba ufufuo wa Yesu hauwezi kubatilishwa!

Niseme tena, yeyote aliye na mamlaka juu ya mauti anastahili kusikilizwa.Yesu alithibitisha nguvu zake juu ya mauti, kwahivyo, twahitaji kusikia kile asemacho. Yesu alidai kuwa yeye pekee ndiye njia ya uzimani (Yohana 14:6). Yeye si njia tu; Yeye si mmoja kati ya njia nyingi, lakini Yesu ndiye njia.

Na Yesu huyu asema hivi, “Njoni kwangu,ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha’’ (Mathayo 11:28, TMP). Huu ni ulimwengu usio na huruma na maisha ni magumu. Wengi wetu tumetendewa dhihaka, tumejeruhiwa, na tumetishika kivita, si kweli? Sasa, kikusaidiacho ni nini? Urejesho au dini zaidi? Mwokozi anayeishi au mmoja kati ya ‘Mitume’ wengi ambao wamekufa? Uhusiano wa maana au kafara za utupu? Yesu si chaguo tu, Yeye ndiye chaguo!

Yesu ndiye ‘dini’ ikufaayo kama unatafuta msamaha (Matendo 10:43). Yesu ndiye ‘dini’ ikufaayo kama unatafuta uhusiano wa maana na Mungu (Yohana 10:10). Yesu ndiye ‘dini’ ikufaayo kama unatafuta uzima wa milele Mbinguni (Yohana 3:16). Weka imani yako kwa Yesu kama Mwokozi wako-ni chaguo lisilo na majuto! Mwamini yeye kwa msamaha wa dhambi zako-hata kuangusha.

Kama ungelitaka kuwa na ‘uhusiano wa sawa’ na Mungu, tazama mfano huu wa maombi. Kumbuka ya kwamba, kwa kusema ombi hili au ombi lengine lolote lile haliwezi kukuokoa. Ni kwa kumwamini Kristo pekee ndiko kutakuokoa toka dhambini. Ombi hili ni njia ya kumweleza Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu, najua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate kusamehewa. Naweka imani yangu Kwako pekee ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu na kwa msamaha-zawadi ya uzima wa milele! Amina!”

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, nichague dini ipi inifaayo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries