settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini ni na imani na dini iliyo na mpangilio?

Jibu


Elezo/maana ya Kamusi ya “dini” itakuwa kitu sawa na, “imani na Mungu au miungu yakuabudiwa, ambayo hudhihirishwa katika tabia na tamaduni; au mpangilio wowote wa imani, ibada na kadhalika, kila mara ambao wahuzisha maumbile. “Katika maana sawia, Bibilia yazungumzia dini zilizo na mpangilio, lakini matukio mengi, lengo na madhumuni ya “dini iliyo na mpangilio” si vitu ambavyo Mungu hufurahishwa navyo.

Katika Mwanzo 11, hata hivyo tukio la kwanza la dini ya mpangilio, uzao/kizazi cha Nuhu aliwaweka pamoja ili wajenge mnara wa Babeli badala ya kutii amri ya Mungu ya kuujaza ulimwengu. Waliamini kuwa umoja wao ni wa maana kuliko uhusiano wao na Mungu. Mungu akaingilia kati na kuwachanganyisha kwa lugha, na kuharibu hii dini iliyokuwa na mpangilio.

Katika Kutoka 6 na kuendelea, Mungu “aliipanga” dini kwa taifa la Israeli. Amri kumi, sheria kuhusu mahali pa kuabudu, na mpangilio wa dhabihu vyote viliwekwa na Mungu na ilikua ifuatwe na Waisraeli wote. Kusoma sana Agano Jipya yaeleza zaidi kwamba lengo la dini hii ilikua inaashiria hataji la mkombozi ambaye in masia (Wagalatia3; Warumi 7). Ingawa wengi wamelielewa vibaya swala hili na wameabudu sheria na tamaduni badala ya kumwabudu Mungu.

Katika historia ya Waisraeli yote, mfutano mwingi unaoshuhudiwa na Waisraeli ulihuzisha ule wa dini ilyo na mpangilio. Kwa mfano kuabudu sanamu (Waamuzi 6; 1 Wafalme 18), Dagoni (1 Samweli 5), na Moleki (2 Wafalme 23:10). Mungu aliwashinda wafuazi wa hizi dini, akionyesha uweza alio nao juu ya vitu vyote na uepo wake kila mahali.

Latika injili, Wafarisayo na Wasadukayo wameelezewa kuwakilisha hizi dini za mpangilio wakati wa Kristo. Yesu kila mara alikabiliana nao kuhusu mafunzo yao potovu na maisha yao ya utabeli. Katika barua kulikua na dini ambazo zilichanganyisha matimizo Fulani, matendo na tamaduni. Pia walitafuta kuwalazimisha wakristo kuasi imani yao na kukubali kuwa “Ukristo pamoja na” dini. Kitabu cha Wagalatia na Wakolosai vinatoa onyo kuhusu hizo dini. Katika kitabu cha Ufunuo dini za mpangilio zitakuwa na usemi katika dunia kama wapinga Kristo na kuunda dini moja ya dunia.

Mara nyingi mwisho wa hizi dini za tamaduni ni upotovu kutoka lile lengo Mungu alikua nalo. Ingawa Bibilia yazungumzia hizi dini za tamaduni ambazo ni baadhi ya mpango wake. Mungu anaviita hivi vikundi vya waumini “kanisa.” Maelezo kutoka kwa kitabu cha Matendo Ya Mitume na Barua zaonyesha kuwa kanisa lastahili kuwa na mpangili na kujisimamia lenyewe. Mpangilia waelekeza, uchungaji, ukuaji, na huduna za uinjilisti (Matendo ya Mitume 2:41-27). Kwa mjibu wa kanisa, ni afadhali uitwe “uhusiano wa mpangilio/utamaduni.”

Dini ni jaribio la mwanadamu kuwa na uhusiano na Mungu. Imani ya kikristo ni uhusiano na Mungu kwa sababu yale ametufanyia kupitia kwa kusulubiwa kwa Yesu Kristo. Hakuna mpango wa kumfikia Mungu (Yeye ametufikia Warumi 5:8). Hakuna kulipa mahari (yote tumeyapokea kwa neema- Waefeso 2:8-9). Kusiwe na mfutano wowote juu ya uongozi (Kristo ndiye kuchwa cha kanisa- Wakolosai 1:18). Kusiwe na upaguzi wowote (wote tu sawa katika Kristo- Wagalatia 3:28). Kuwa na mpangili si shida. Kuzifuata sheria na tamaduni za dini ndio shida.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini ni na imani na dini iliyo na mpangilio?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries