settings icon
share icon
Swali

Dhambi iliyo ya mauti ni gani?

Jibu


Yohana wa Kwanza 5:16 ni mojapo ya mistari ngumu sana katika Agano JipyaNew Testament kutafsiri. "Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo." Kati ya tafsiri zote huko nje, hakuna inayoonekana kujibu maswali yote kuhusu mstari huu. Tafsiri bora inaweza kupatikana kwa kulinganisha aya hii kwa kile kilichotokea kwa Anania na Safira katika Matendo 5:1-10 (angalia pia 1 Wakorintho 11:30). "Dhambi ya mauti" ni kwa makusudi, makusudi, kuendelea, dhambi asiyoungamwa. Mungu, kwa neema yake, anaruhusu watoto wake kuendelea kufanya dhambi bila kuwaadhibu mara hiyo hiyo. Hata hivyo, kuna wakati unakuja Mungu krhataruhusu muumini kuendelea katika dhambi asiyoitubu. Wakati hatua hii imefikiwa, Mungu wakati mwingine anaamua kumwadhibu Mkristo, hata kufikia hatua ya kuchukua maisha yake.

Hicho ndicho alichofanya katika Matendo 5:1-10 na 1 Wakorintho 11:28-32. Hii ndio labda Paulo alieleza kanisa la Korintho katika 1 Wakorintho 5:1-5. Tunapaswa kuomba kwa ajili ya Wakristo ambao wanafanya dhambi. Hata hivyo, unakuja wakati ambapo Mungu hatasikiza sala ya muumini mwenyedhambi ambaye ameamua kwamba hukumu inamjia. Ni vigumu kutambua kuwa kuna wakati ni tumechelewa mno kuomba kwa ajili ya mtu. Mungu ni mwema na haki, na ni lazima tumruhusu kuamua ni wakati gani tutakuwa tumechelewa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Dhambi iliyo ya mauti ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries