settings icon
share icon
Swali

Dhambi ya kuhesabiwa ni nini?

Jibu


Katika bustani mwa Edeni, wakati Adamu alipofanya dhambi kwa kula tunda kutoka kwa Mti wa kujua Mema na Maovu, kitendo hicho cha uasi kilileta athari mbaya na ya aina mbili kwa wanadamu wote. Athari ya kwanza ilikuwa dhambi ya asili na ya pili dhambi ya kuhesabiwa.

Adamu, kama kiongozi wa kizazi cha wanadamu, alisababisha kila mtu baada yake kuzaliwa katika hali ya kuanguka au hali ya dhambi. Athari hii ya dhambi ya Adamu inajulikana kuwa dhambi ya asili na mara nyingi inajulikana kuwa dhambi ya kurithi. Wanadamu wote wamerithi asili ya dhambi kupitia tendo la awali la Adamu la kutotii (Warumi 5:12-14).

Fauka ya kupokea asili iliyoanguka, watu wote waliokuja baada ya Adamu wamehesabiwa kuwa na hatia ya dhambi ya Adamu (Warumi 5:18). Hiyo ndiyo maana ya kuhesabiwa dhambi. Kutuhumiwa ni kuhesabiwa au kuwajibishwa na kitu. Dhabi iliyohesabiwa ni hatia ya Adamu iliyohusishwa au kuhesabiwa kwetu. Wanadamu wote wanahesabiwa kuwa walifanya dhambi katika Adamu na hivyo kustahili adhabu sawa na ile ya Adamu. Dhambi iliyohesabiwa huathiri msimamo wetu mbele za Mungu (tuna hatia, tumehukumiwa), ambapo dhambi ya asili huathiri tabia zetu (tumeharibiwa kimaadili). Dhambi ya asili na iliyohesabiwa hutufanya tuwe chini ya hukumu ya Mungu.

Neno deni linatumika kisheria na kifedha na linamaanisha “kutaja kitendo, neno, au kitu chochote kama kilivyohesabiwa mtu mwingine.” Kibiblia, dhambi ya Adamu ilihesabiwa kwa wazao wake wote, nao wanapaswa kukabiliwa kama wenye hatia. Haimaanishi wao binafsi wana hatia ya dhambi ya Adamu, ila tu kwamba dhambi yake ilihesabiwa kwao, na hivyo kila mtu anashiriki katika hatia na adhabu ya kosa hilo la asili.

Adhabu ya dhambi ni mauti. Tuko chini ya kifo cha kiroho, au utengano kutoka kwa Mungu katika maisha haya ya sasa, kwa sababu ya dhambi inayohesabiwa: “Kwa habari zenu, mlikuwa wafu katika makosa na dhambi zenu, ambazo mlizitenda mlipofuatisha namna ya ulimwengu huu na za yule mtawala wa ufalme wa anga, yule roho atendaye kazi sasa ndani ya wale wasiotii. Sisi sote pia tuliishi katikati yao hapo zamani, tukitimiza tamaa za asili yetu ya dhambi na kufuata tamaa zake na mawazo yake. Nasi kwa asili tulikuwa wana wa ghadhabu, kama mtu mwingine yeyote” (Waefeso 2:1-3). Ikiwa tutadumu katika hali hii ya utengano na Mungu, matokeo yake ni kifo cha pili, ambacho ni cha milele (Ufunuo 20:11-15).

Kifo cha kimwili pia ni adhabu ya dhambi iliyohesabiwa: “Kwa hiyo kama vile dhambi ilivyoingia ulimwenguni kupitia kwa mtu mmoja, na kupitia dhambi hii mauti ikawafikia watu wote, kwa sababu wote wamefanya dhambi” (Warumi 5:12). Hatia ya dhambi ya Adamu moja kwa moja ilitwikwa na kuhesebiwa juu ya jamii yote ya wanadamu ili kwamba watu wote sasa wako chini ya kifo (Warumi 6:23).

Mtume Paulo anafundisha kuhesabiwa dhambi katika vifungu mbalimbali: “watu wengi walikufa kwa sababu ya kosa la mtu mmoja,” “kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta adhabu kwa watu wote,” “Kwa maana kama vile kwa kutokutii kwa yule mtu mmoja wengi walifanywa wenye dhambi” (Warumi 5:15,18,19). Na “Kwa maana kama vile katika Adamu watu wote wanakufa” (1 Wakorintho 15:22).

Habari njema kuhusu dhambi ya asili na kuhesabiwa ni kwamba Mungu tayari alikuwa na suluhu, mpango mkuu wa wokovu, hata kabla ya Adamu kufanya dhambi katika Bustani.

Suluhu ya dhambi iliyohesabiwa ni kazi ya upatanisho ya Yesu Kristo: “Kwa maana kama vile kwa kutokutii kwa yule mtu mmoja wengi walifanywa wenye dhambi, vivyo hivyo kwa kutii kwa mtu mmoja wengi watafanywa wenye haki” (Warumi 5:19). Pindi mwenye dhambi anapomwamini Yesu na kukubali karama Yake ya wokovu, atahesabiwa haki ya Kristo: “Kwa maana kama vile katika Adamu watu wote wanakufa, vivyo hivyo katika Kristo wote watafanywa hai” (1 Wakorintho 15:22). Waumini wanamiliki haki ya kuhesabiwa.

Kama vile watu wote walivyo ndani ya Adamu, vivyo hivyo waumini wote wako katika Kristo. Kuwa ndani ya Kristo maana yake ni kwamba haki yake sasa ni yetu. Kupitia kifo cha dhabihu cha Kristo msalabani, dhambi ya wanadamu ilihesabiwa kwa Kristo. Yesu alijitwika adhabu ya dhambi zetu: ” Alitolewa afe kwa ajili ya dhambi zetu, naye alifufuliwa kutoka mauti ili tuhesabiwe haki” (Warumi 4:25).

Waumini bado hawajakamilishwa katika haki. Hata hivyo wamevikwa haki iliyohesabiwa ya Kristo: “Kwa maana Mungu alimfanya yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu kwake yeye” (2 Wakorintho 5:21). Yesu alijibu madai ya haki kwa dhambi zetu na kukidhi matakwa ya Sheria (Warumi 3:25-26; Wakolosai 2:14).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Dhambi ya kuhesabiwa ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries