settings icon
share icon
Swali

Je! Dhambi tendaji ni gani?

Jibu


Kunazo njia mbili za kimsingi ambazo kwazo tunatenda dhambi: aidha kutenda bila kukusudia au kutenda kimakusudi. Dhambi za kutendwa bila kukusudia, ni aina ya zile dhambi ambazo tulijua tulipaswa kufanya jambo na hatukufanya chochote (Yakobo 4:17). Dhambi tendaji ni ile aina ya dhambi tunachukua hatua na kuitenda (dhambi ya makusudi), iwe ni kwa njia ya mawazo, maneno au matendo. Dhambi tendaji inaweza kuwa ya makusudi. Ufahamu wa kabla haujalishi. Ukitembelea nchi nyingine ambayo magari yanaendeshwa katika upande kushoto, na ukiendesha kwenye njia ya kulia, bado unavunja sheria iwe unaijua au la. Sheria ya Agano la Kale iliagiza dhabihu maalum kwa ajili ya dhambi ambazo hazikuwa za kukusudia, lakini hata hivyo zilikuwa dhambi (Hesabu 15:22-24; taz. Waebrania 9:7).

Dhambi ya kwanza ya mwanadamu ilikuwa ni dhambi ya kusudi. Mungu aliwakataza kula tunda fulani (Mwanzo 2:16-17). Adamu na Hawa walijua amri ya Mungu na bado wakaasi (Mwanzo 3:6). Walichukua hatua ya kutenda dhambi. Mfalme Daudi alipofanya uzinzi kisha akaamuru Uria auawe ili kuficha jambo hilo, zote zilikuwa dhambi za kukusudia (2 Samweli 11). Biblia haifichi maelezo machafu ya maisha ya watu ambao aliwapenda na kuwatumia. Kurasa zake zimejaa dhambi za makusudi za viongozi wakuu kama Ibrahimu (Mwanzo 20:2), Musa (Kutoka 2:11-12), Daudi (2 Samweli 12:13), Sulemani (Nehemia 13:26), Petro (Mathayo 26:74-75), na Paulo (Wagalatia 1:13).

Sisi sote tuna hatia ya dhambi za kukusudia. Sisi sote tunafanya dhambi kimakusudi kwa kuenenda njia ambazo Mungu amekataza. Pia tunafanya dhambi bila kukusudia kwa kutojua viwango vya Mungu (Matendo 3:17; 1 Petro 1:14; Walawi 4:13-14). Asili yetu ya dhambi hutuzuia tusiwe na ushirika na Mungu. Tunaweza kuwa na kiwango cha dhambi tunazofanya kwa uwazi, lakini hatuwezi kusafisha mioyo yetu. Yesu alisema “Lakini kitokacho kinywani hutoka moyoni, na hiki ndicho kimtiacho mtu unajisi. Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na masingizio” (Mathayo 15:18-19).

Ndio maana tunamwihitaji Yesu. Hatuwezi kujizuia kutenda dhambi, na kwa kutenda dhambi tunaondoa tumaini lolote la kuunganishwa na Mungu mtakatifu. Wakati tu tunaporuhusu kifo na ufufuo wa Kristo kuwa mbadala wetu ndipo dhambi yetu inaweza kufutwa (Wakolosai 2:14; Warumi 6:6). Wakorintho wa pili 5:21 inasema, “Kwa maana Mungu alimfanya yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu kwake yeye.” Yesu alizibeba dhambi zetu za makusudi na zile siziso za makusudi na akalipa deni tunalodaiwa na Mungu.

Zaburi 51 ni sala ambayo Daudi aliandika baada ya kukabiliwa na dhambi yake ya makusudi. Alikuwa ametenda dhambi sana, na kungekuwa na athari (2 Samueli 12:14-15). Lakini alijua jinsi ya kutubu. Na alikuwa na ujasiri kamili katika neema ya Mungu na kupasa sauti, “Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu. Usinitupe kutoka mbele zako wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu. Unirudishie tena furaha ya wokovu wako,

unipe roho ya utii, ili initegemeze” (Zaburi 51:10-12). Daudi anatupa mfano wa njia sahihi ya kukabiliana na dhambi zetu za makusudi. Wakati tunatambua dhambi yetu dhidi ya Mungu, tunaweza kumgeukia, kukiri dhambi hiyo, na kumwomba atutakase. Tunaweza kutumaini nguvu za damu ya Yesu iliyomwagika ili kufuta dhambi zetu. Mungu anaahidi kuturudisha katika ushirika na kututia nguvu ili tuishi kwa njia inayompendeza yeye (Wafilipi 4:13).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Dhambi tendaji ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries