settings icon
share icon
Swali

Je! Inamaanisha nini kwamba dhambi ni uasi?

Jibu


Waraka wa Kwanza wa Yohana 3:4 inasema, “Kila mtu atendaye dhambi anafanya uasi, kwa kuwa dhambi ni uasi.” Neno lililotafsiriwa “kuasi sheria” linatokana na neno la Kigiriki anomia, ambalo linamaanisha “kupuuza Mungu na sheria Zake.” Kutoka kwa neno hili la Kiyunani pia tunapata neno kinyume na sheria (antinomianism), ambayo ni imani kwamba hakuna sheria za maadili ambazo Mungu anatarajia Wakristo kutii. Kila dhambi ni uasi dhidi ya Mungu kwa sababu dhambi inakiuka kiwango chake cha maadili kwa wanadamu. Kwa kuwa Mungu alituumba (Mwanzo 1:27), ana haki ya kutuwekea mipaka. Ukuikaji wowote wa mipaka hiyo ni uvunjaji wa sheria yake, ambayo ina maana kwamba kila dhambi ni tendo la uasi.

Mfuasi wa Mungu ataepuka uasi-sheria. Mtu aliyebarikiwa anaelezewa kuwa “Bali huifurahia sheria ya Bwana, naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana” (Zaburi 1:2). “Ee Bwana, ninatamani wokovu wako, na sheria yako ni furaha yangu” (Zaburi 119:174). Tofauti kati ya kuasi sheria na upendo haingekuwa wazi zaidi: “Mioyo yao ni katili na migumu, bali mimi napendezwa na sheria yako” (Zaburi 119:70).

Maandiko yanatofautisha kati ya mtu anayetenda dhambi, kama vile sisi sote tunavyofanya (Warumi 3:10, 23; 1 Yohana 1:8), na mtu ambaye “anatenda uasi” (Mathayo 7:23; 13:41). Mtu asiyetii sheria, ni yule ambaye amejitoa kabisa katika maisha ya dhambi. Watu wasiotii sheria ama hawamwamini Mungu au wanakataa kukiri haki yake ya kutawala maisha yao (Zaburi 14:1). Hata wale wanaoishi katika uasi wa sheria wanaweza kupata msamaha ikiwa watageuka kutoka kwa dhambi zao na kupokea haki na wokovu wa Kristo (2 Wakorintho 5:21; Yohana 3:16-18).

Wale wanaodumu katika kuiasi sheria hawataurithi ufalme wa Mungu (1 Wakorintho 6:9-10; Wagalatia 5:20-21). Yesu alionya kwamba katika nyakati za mwisho uasi wa sheria utaongezeka na “upendo wa wengi utapoa” (Mathayo 24:12). Mtazamo wa uasi-sheria unapoenea angani, watu huanza kujiuliza juu ya mema na mabaya. Hawajui tena au hawajali kwamba viwango kamili vya maadili vipo. Watu wasio na sheria wanaweza kujiona kuwa watu wa kidini na wa kiroho sana, lakini wamemfafanua Mungu jinsi wanavyotamani awe, na si jinsi alivyo.

Mpinga Kristo ambaye ametabiriwa kutokea katika nyakati za mwisho anaelezewa kuwa ni “mtu wa kuasi” (2 Wathesalonike 2:3,8). Danieli anasema atakuwa mfalme ambaye “atafanya apendavyo” (Danieli 11:36). Mpinga Kristo atakuwa ni yule anayemjua Mungu ni nani lakini anajitangaza kuwa juu ya Mungu, kama vile Shetani alivyofanya (Isaya 14:14; 1 Yohana 2:22; 4:3; 2 Wathesalonike 2:4). Anaitwa “mwasi-sheria” kwa sababu atakataa mamlaka yote na kukabidhiwa dhambi. Wale wanaomfuata Mpinga Kristo wakati wa dhiki watamfuata katika uasi, kwa uharibifu wao wenyewe. Wale wanaopokea alama yake hawataweza kamwe kutubu na kupata msamaha, lakini watateswa milele katika ziwa la moto (Ufunuo 14:9-10).

Uasi huleta utamaduni unaokaidi (Mithali 29:18). wakati wa waamuzi ulikuwa wenye msukosuko kwa sababu, kwa sehemu, “kila mtu alifanya kile alichoona ni sawa machoni pake mwenyewe” (Waamuzi 21:25). Tunaona athari za kuasi sheria katika sehemu kubwa ya ulimwengu hii leo. Sheria za Mungu na hata sheria za jamii ya kilimwengu zimekataliwa kuwa zimepitwa na wakati, za kupita kiasi, au za kutiisha. Kila mtu ni sheria kwake mwenyewe, na matokeo ya aina hiyo ya uasi ni mchafuko na vurugu. Dhambi haipaswi kuhalalishwa kwa kupandishwa/kukunja mabega na kusema “sio ukamilifu wa mtu yeyote.” Kila tendo la dhambi ni kielelezo cha uasi wa sheria kwa sababu ni ukiukaji wa kiwango cha Mungu cha utakatifu na tabia yake kamilifu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Inamaanisha nini kwamba dhambi ni uasi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries