settings icon
share icon
Swali

Dhambi kuu ni gani?

Jibu


Ukatoliki wa Kirumi unafundisha kwamba dhambi kuu ndio shina na chanzo cha dhambi nyingine zote. Kitangulizi cha kwanza cha fundisho hili kiliandikwa katika karne ya nne na mtawa anayeitwa Evagrius Ponticus, ambaye hapo awali aliorodhesha “mawazo mabaya” manane: ulafi, tamaa ua usherati, ubahili/tamaa ya mali, sikitiko au huzuni, hasira, kukata tamaa au kutokuwa na msimamo, majivuno, na kiburi. Baadaye kikundi hicho cha mambo manane kilipunguzwa hadi vitu saba na Papa Gregory Mkuu katika karne ya sita. Gregory aliorodhesha majivuno kuwa pamoja na kiburi na kukata tamaa kuwa huzuni, na kuongeza wivu, hivyo kuunda orodha iliyojumuisha “dhambi kuu” kuwa saba au “dhambi mbaya.” Leo hii, orodha ya dhambi kuu ni kama ifuatavyo: kiburi, uchoyo, tamaa, husuda, ulafi, hasira, na wivu.

Dhambi kuu hutokana na neno la Kilatini caput ambalo linamaanisha ”kichwa.” Thomas Aquinas baadaye hakuziita “dhambi,” bali “maovu.” Aquinas alitangaza kwamba uovu kuu ni ule ambao una mwisho wa kutamanika ili, kwa hamu yake, mtu afanya dhambi nyingi. Dhambi zote zinaweza kufuatiliwa hadi kwenye uovu fulani kama chanzo kikuu. Kwa mfano, ikiwa mwanamume anamtamani mke wa jirani yake, uovu huo unaweza kumfanya afanye uzinzi, kusema uongo kwa watu wengi, kupuuza au kuacha familia yake, na labda hata kuwaumiza watu kimwili. Dhambi zinazoongezeka kwa mtu huyo hushawishiwa na dhambi kuu ya tamaa ya hapo mwanzo.

Ni kweli kwamba kiburi, uhcoyo, tamaa, husuda, ulafi, hasira, na uvivu ni dhambi, na ni kweli kwamba tamaa hizo mbaya moyoni zinaweza kusababisha dhambi nyingine (soma Mathayo 15:19). Lakini ingekuwa kosa kufikiria dhambi saba kuu, au dhambi saba mbaya zaidi, kuwa mbaya zaidi machoni pake Mungu kuliko dhambi zingine. Dhambi zote machoni pa Mungu ziko sawa; zote, “zimekosa kiwango chake.” Kuiba sio dhambi mbaya kuliko kiburi, na uchoyo sio mbaya zaidi kuliko kusema uongo; hakuna dhambi ndogo au dhambi kubwa, kwa sababu dhambi zote ni chukizo sawa kwa Mungu wetu mtakatifu na mwadilifu. Mungu hawezi na kamwe hataweza kuiruhusu dhambi yoyote katika uwepo wake mtakatifu (Habakuki 1:13).

Dhambi kuu, au dhambi mbaya, hazijatajwa kama kundi katika Biblia; hata hivyo, Bwana anataja baadhi ya mambo ambayo Anachukia na hata kuorodhesha hayo: “Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana, naam, viko saba vilivyo chukizo kwake: macho ya kiburi, ulimi udanganyao, mikono imwagayo damu isiyo na hatia, moyo uwazao mipango miovu, miguu iliyo myepesi kukimbilia uovu, shahidi wa uongo ambaye humwaga uongo,na mtu ambaye huchochea fitina kati ya ndugu” (Mithali 6:16-19). Dhambi zote husababisha kifo (Warumi 6:23). Mungu asifiwe kwamba, kupitia damu ya Yesu Kristo, dhambi zetu zote zinaweza kusamehewa-hata “dhambi kuu.”

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Dhambi kuu ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries