settings icon
share icon
Swali

Je! Mungu huitazama dhambi isiyokusudiwa kwa njia tofauti?

Jibu


Kitabu cha Walawi kilihitaji matoleo tofauti kulingana na ikiwa dhambi ilikuwa ya kukusudia au bila kukusudia. Je, hii inamaanisha kwamba Mungu huzitazama dhambi zisizokusudiwa kwa njia tofauti?

Sio hakika vile. Ni wazi kwamba Mungu aliweka tofauti kati ya dhambi za kukusudia na zisizokusudiwa katika suala la matoleo katika Agano la Kale. Walawi 4:2-3 inabainisha mfano huu: “Mtu yeyote afanyapo dhambi bila kukusudia na akatenda lile lililokatazwa katika amri yoyote ya Bwana: “‘Ikiwa kuhani aliyetiwa mafuta amefanya dhambi na kuwaletea watu hatia, lazima alete kwa Bwana fahali mchanga asiye na dosari, kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya dhambi aliyotenda.”

Dhana ya dhambi isiyo ya kukusudia katika Walawi 4 inahusiana na dhambi kwa kupotea au kwa bahati mbaya. Katika hali hii, sadaka inaweza kutolewa. Hata hivyo, hakukuwa na toleo lililopatikana kwa ajili ya mtu alipotenda dhambi kimakusudi. Hesabu 15:30-31 inasema, “Lakini yeyote ambaye amefanya dhambi kwa dharau awe mzawa au mgeni, anamkufuru Bwana, naye mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake. Kwa sababu amelidharau neno la Bwana na kuvunja amri zake, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali; hatia yake inabaki juu yake.” Wale walioasi katika kutenda dhambi kimakusudi walipaswa kukataliwa mbali au kutengwa na watu.

Ingawa kunaweza kuwa na tofauti katika suala la matokeo ya dhambi zisizokusudiwa na za kukusudia katika Agano la Kale, Biblia iko wazi wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu (Warumi 3:23). Matoleo ya Agano la Kale yalifananisha kutolewa kwa Yesu Kristo mwenyewe kama dhabihu msalabani kwa ajili ya dhambi zetu. Yesu ndiye kibadala cha kutosha cha msamaha na uzima wa milele.

Katika Yohana 14:6 Yesu anafundisha, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia kwangu.” Ingawa kila mtu amefanya dhambi (isipokuwa Yesu), tunayo fursa ya msamaha na ukombozi kutoka kwa dhambi kupitia dhabihu ya Yesu msalabani. Kwa imani katika Yeye, wokovu hupatikana (Waefeso 2:8-9). Hii ni kweli, haijalishi ikiwa dhambi ni za kukusudia au sio za kukusudia, iwe mtu anaamini kwamba amefanya dhambi kidogo au ametenda dhambi nyingi.

Maandiko yako wazi kwamba mwanadamu aliumbwa akiwa mzuri lakini yeye ni mwenye dhambi sasa kama matokeo ya Anguko (Mwanzo 3). Haijalishi aina au kiwango cha dhambi ambazo mtu ametenda, Yesu anatosha kusamehe na kutoa uzima wa milele. Wale wanaoikataa injili, bila kujali ni kiasi gani au ni dhambi ndogo kiasi gani wametenda, watatengwa na Mungu kwa umilele na watapata adhabu ya milele kwa ajili ya dhambi zao. Mungu anawaita watu wote waje kwake, kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbingu lililotolewa kwa wokovu (Matendo 4:12).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mungu huitazama dhambi isiyokusudiwa kwa njia tofauti?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries