settings icon
share icon
Swali

Je ni nini huunda ndoa kulingana na Biblia?

Jibu


Hili ni swali ngumu kulijibu kwa sababu hamna Biblia inasema waziwazi ni katika hatua gani Mungu huwadhamini wanandoa. Kuna mitazamo tatu ya kawaida: 1) Mungu huwadhamini wanandoa wanapoana kisheria. 2) wanandoa wameoana mbele za macho ya Mungu wakati wao wamekamilisha baadhi ya aina ya sherehe rasmi ya harusi. 3) Mungu anawadhamini wanandoa kuolewa wakati wajamian katika ndoa. Hebu tuangalie katika kila moja ya mitazamo tatu na tuone ni nini umuhimu na udhaifu wa kila moja.

1) Mungu hudhamini ndoa ya wanandoa wakati wameoana kihalali. Uungwaji wa maandishi kawaida kulingana na mtazamo huu ni mistari ambayo huimiza kutii serikali (Warumi 13:1-7; 1 Petro 2:17). Hoja ikiwa kama serikali inahitaji baadhi ya "cheti" kukamilika kabla ya ndoa kutambuliwe, wanandoa wanapaswa kutii wenyewe mchakato wowote ambao serikali inahitaji. Dhahiri ni Kibiblia kwa wanandoa kuwa na utii kwa serikali ili muradi tu kama mahitaji hayo si kinyume na neno la Mungu na ni ya manufaa. Warumi 13:1-2 inatuambia, "Kila mtu lazima aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maan hakuna mamlaka isiyotika kwa Mungu; na ile iliyop umeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlakhushidnana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu."

Kuna baadhi ya udhaifu na matatizo ya uwezo kwa mtazamo huu. Kwanza, kulikuwa na ndoa kabla ya serikali yoyote iundwe. Kwa maelfu ya miaka, watu walikuwa wanafunga ndoa na hakuna kitu kama vile cheti cha ndoa. Pili, hata hii leo, kuna baadhi ya nchi ambazo hakuna utambuzi wa ndoa kiserikali, na hawana matakwa ya kisheria kwa ndoa. Tatu, kuna baadhi ya serikali ambazo zinaweka mahitaji yasiyo ya kibiblia kwa ndoa kabla itambuliwe kisheria. Kwa mfano, kuna nchi ambazo zinahitaji harusi kufanyika katika Kanisa la Katoliki, kwa mujibu wa mafundisho ya Kikatoliki, na kusimamiwa na padri wa Kikatoliki. Ni wazi, kwa wale ambao wana msimamo tofauti na Kanisa la Katoliki na ufahamu wa kikatoliki wa ndoa kama sakramenti, itakuwa si kibiblia kutii kwa kuoana ndani ya Kanisa la Katoliki.

2) Maharusi watakuwa wameoana katika macho ya Mungu wakati wao hukamilisha baadhi ya aina ya sherehe rasmi ya harusi. Sambamba na jinsi katika tamaduni nyingi, baba humpeana bintiye katika harusi, baadhi ya wakalimani huelewa Mungu kumleta Hawa Adamu (Mwanzo 2:22) kuwa Mungu Alisimamia harusi "sherehe" ya kwanza. Katika Yohana sura ya 2, Yesu alihudhuria sherehe ya harusi. Yesu hangeudhuria tukio kama hilo ikiwa hakuwa amelihidhinisha litokee. Yesu kuhudhuria sherehe ya harusi inaonyesha kwamba Mungu inahitaji sherehe ya harusi, lakini dhahiri zaidi haimaanishi kuwa sherehe ya harusi inakubalika mbele za Mungu. Karibu kila utamaduni katika historia ya binadamu umekuwa na baadhi ya aina rasmi ya sherehe ya harusi. Katika kila utamaduni kuna tukio, hatua, agano, au tangazo ambalo kwamba limetambuliwa kwa kutangaza mume na mke wameoana.

3) Mungu anawaona maharusi kuoana wakati ndoa imetimizwa kwa kujamiiana. Kuna baadhi ya watu wanaodai kwamba mume yeyote na mke kuwa na ngono, Mungu anawachukulia hao wawili kuwa maharusi. Msingi wa mtazamo huu ni dhana hii ni ukweli kwamba kujamiiana kati ya mume na mke ni utimilifu wa mwisho wa kanuni ya "mwili mmoja" (Mwanzo 2:24; Mathayo 19:5, Waefeso 5:31). Kwa mjibu huu, kujamiiana ni "muhuri" wa mwisho kwa agano la ndoa. Hata hivyo, kama wanaharusi wemeoana kisheria na kisherehe, lakini kwa sababu fulani hawawezi kushiriki katika ngono, maharusi hao bado wachukuliwa wanandoa.

sio Kibiblia kufikiria wanandoa ambao wamekuwa na ngono-lakini ngono hawajatimiza yoyote ya mambo mengine ya agano la ndoa, hawastahili kuoana. Maandiko kama vile 1 Wakorintho 7:2 zinaonyesha kwamba ngono kabla ya ndoa ni uasherati. Kama kujamiiana husababisha wanandoa kuwa ndoa, basi haiwezi kuchukuliwa kuwa uasherati, kwa vile wanandoa huchukuliwa kuwa ndoa wakati wao hushiriki katika ngono. Hakuna kabisa misingi wa kibiblia kwa maharusi kufanya ngono na kisha kujitangaza wenyewe kuwa wameoana, hivyo kutangaza baadaye mahusiano yote ya ngono kuwa halali na uheshimu Mungu.

Hivyo, ni nini huudna ndoa mbele ya macho za Mungu? Inaonekana kwamba kanuni zifuatazo zinapaswa kufuatwa: 1) Ikiwa mahitaji ni busara na si kinyume na Biblia, wanandoa wanapaswa kutafuta chochote hutambuliwa rasmi na kiserikali na kinapatikana. 2) wanandoa wanapaswa kufuata tamaduni lolote na desturi ya kifamilia ni kawaida wazinazotumika kutambua maharusi kama "ndoa rasmi." 3) Kama inawezekana, maharusi wanapaswa kutimiza ndoa kwa kujamiiana, kutimiza kanuni ya "mwili mmoja".

Je! Itakuaje ikiwa moja au zaidi ya kanuni hizi hazijatimizwa? Wanaharusi kama hao bado huchukuliwa ndoa mbele ya macho za Mungu? Hatimaye, hiyo ni kati ya maharusi na Mungu. Mungu anajua mioyo yetu (1 Yohana 3:20). Mungu anajua tofauti kati ya agano kwali la ndoa na jaribio la kuhalalisha uasherati.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je ni nini huunda ndoa kulingana na Biblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries