settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inasema nini kuhusu uongo? Je kusema uongo ni dhambi?

Jibu


Biblia iko wazi kwamba kusema uongo ni dhambi na haimpendezi Mungu. Dhambi ya kwanza katika ulimwengu huu ilihusisha uwongo alioambiwa Hawa. Amri kumi alizopewa Musa ni pamoja na: “Usimshuhudie jirani yako uongo” (Kutoka 20:16).

Katika kanisa la kwanza, Anania na Safira walidanganya kuhusu mchango wao ili wajifanye waonekane wakarimu ziadi kuliko walivyokuwa. Onyo la Petro ni kali: “Anania, mbona Shetani ameujaza moyo wako ili kumwambia uongo Roho Mtakatifu?” (Matendo 5:3). Hukumu ya Mungu ilikuwa kali zaidi: wenzi hao walikufa kwa sababu ya dhambi yao ya kusema uongo (Matendo 5:1-11).

Wakolosai 3:9 inasema, “Msiambiane uongo, kwa maana mmevua kabisa utu wenu wa kale pamoja na matendo yake.” Uongo umeorodheshwa katika 1 Timotheo 1:9-11 kama kitu kinachofanywa na waasi. Zaidi ya hayo, waongo watakuwa miongoni mwa wale watakaohukumiwa mwoshoni (Ufunuo 21:8). Kwa ulinganisho, Mungu hadanganyi kamwe (1:2). Yeye ndiye chanzo cha ukweli. Mungu hawezi kusema uongo (Hesabu 23:19).

Yesu alijitambulisha kuwa njia, kweli, na uzima (Yohana 14:6), na anatazamia wale wanaomfuata wawe watu wa ukweli. Ukweli unapaswa kuonyeshwa kupitia upendo (Waefeso 4:15), huku ukitoa tumaini kwa wale wanaotafuta ukombozi kutoka kwa uongo wa ulimwengu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inasema nini kuhusu uongo? Je kusema uongo ni dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries