settings icon
share icon
Swali

Biblia inasemaje juu ya kuchoma maiti? Wakristo wanapaswa kuchomwa wakifa?

Jibu


Biblia haitoi mafundisho yoyote maalum kuhusu uchomaji maiti. Kuna matukio katika Agano la Kale ya watu kuchomwa kwa moto hadi kufa (1 Wafalme 16:18, 2 Wafalme 21:6) na mifupa ya binadamu kuchomwa moto (2 Wafalme 23:16-20), lakini haya hii mifano ya uchomaji wafu. Ni jambo la kuvutia kutambua kwamba katika 2 Wafalme 23:16-20, kuchoma mifupa ya binadamu juu ya madhabahu ni kuharibu madhabahuni. Wakati huo huo , katika sheria za Agano la Kale hakuna mahali inaamrisha kwamba mwili wa marehemu uchomwe, wala kuambatisha laana yo yote au hukumu juu ya mtu ambaye amechomwa.

Uchomaji wafu ulikuwa unatekelezwa katika nyakati za Biblia, lakini haikuwa kawaida mazoezi tamaduni kwa Waisraeli au kwa waumini wa Agano Jipya. Katika tamaduni za nyakati za Biblia, kuzikwa katika kaburi, pango, au katika ardhi ilikuwa njia ya kawaida ya kuondoa mwili wa binadamu (Mwanzo 23:19; 35:9; 2 Mambo ya Nyakati 16:14; Mathayo 27:60-66). Huku mazishi ikuwa jambo la kawaida, hakuna mahali Biblia inaamrisha kuzika kama njia ya kuuweka mwili.

Je! Uchomaji wafu ni jambo Mkristo anapazwa kufikiria? Tena , hakuna amri kuu ya maandiko dhidi ya kuchoma wafu. Baadhi ya waumini hupinga mazoea ya kuchoma wafu juu ya msingi kwamba haitambui kwamba siku moja Mungu ataifufua miili yetu na kuinganisha pamoja na nafsi zetu / roho (1 Wakorintho 15:35-58, 1 Wathesalonike 4:16). Hata hivyo, ukweli kwamba mwili ambao umechomwa hauifanyi kuwa vigumu zaidi kwa Mungu kuffufua mwili huo. Miili ya Wakristo ambayo ilikufa miaka elfu iliyopita, kwa sasa, imegeuka mavumbi. Hii kwa vyovyote haiwezi mzuia Mungu na kuwa na uwezo wa kuifufua miili yao. Yeye ndiye aliye waumba kwanza; Hatakua na ugumu wa kuiumba tana. Uchomaji wafu haufanyi chochote ila tu "kaharakisha" mchakato wa kuufanya mwili kubadilika na kuwa mavumbi. Mungu ana uwezo wa kufufua mabaki ya mtu ambayo yalikuwa yamechomwa jinsi Yeye ni mabaki ya mtu ambaye hakuwa amechomwa. Suala la kuzika au kuchoma liko ndani ya ulimwengu wa uhuru wa Kikristo. Mtu au familia inayozingatia suala hili wanapaswa kuomba kwa ajili ya hekima (Yakobo 1:5) na kufuata mvuta wa imani baada ya maombi.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasemaje juu ya kuchoma maiti? Wakristo wanapaswa kuchomwa wakifa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries