settings icon
share icon
Swali

Je, Biblia inasema nini kuhusu kuwa na tabia za kiume na kike?

Jibu


Mtindo wa kuwa na tabia za kiume na kike, au kuwa na jinsia zote, hutia ukungu kwenye mipaka ya utambulisho wa kinjisia au kwa njia fulani unachanganya vipengele vya kiume na kike. Ili mtu binafsi, mtindo wa maisha, au nguo zichukuliwe kuwa ni za jinsia zote, lazima zikose utambulisho wa kijinsia unaotambulika. Mtu mwenye tabia za kiume na kike kweli hatambuliki kwa urahisi kama mvulana au msichana-na mkanganyiko huo unakusudiwa.

Ingawa mambo mengi si ya kiume wala ya kike (elimu, ajira, magari, n.k.), mtindo wa kuwa ta na tabia za kike na kiume huwa umekusudiwa. Watu wengi huchagua mtindo huo ili kutoa kauli la kisiasa au la kimaadili. Wanawake ambao hunyoa nywele zao kama wanaume, hufunga matiti yao, na kuvaa nguo kubwa za kiume, wanajaribu kuficha ujike wao. Vilevile, wanaume wanaotengeneza nywele zao kwa njia za kitamaduni za kike, huvaa mavazi ya kike, au kujipodoa wanajaribu kupinga mwonekano wa kijadi wa kiume. Idadi kubwa ya watu wanaochagua mtindo wa jinsia zote pia wanatatizika na masuala ya utambulisho wa kijinsia, hisia ya jinsia tofauti au ushoga. Lakini, ikiwa sura ya nje ya mtu ni suala la uamuzi wa kibinafsi, je, kuna mambo ya kiadili na kiroho ya kuzingatia? Je, biblia inasema lolote kuhusu mtindo wa kuwa na tabia ya kike na kiume?

Mungu aliumba hasa jinsia mbili tofauti kutumikia majukumu mawili tofauti katika uumbaji wake (Mwanzo 1:27). Mungu alimuumba Adamu katika tendo maalum la uumbaji (Mwanzo 2:7). Kisha akamuumba mwanamke, Hawa, kutoka kwa ubavu wa Adamu ili awe msaidizi wake (Mwanzo 2:20-22). Adamu na Hawa walikuwa na sifa tofauti kabisa. Walikuwa tofauti kwa sababu Mungu alikusudia wawe tafauti, na aliwapenda hivyo (Mwanzo 1:31). Mwanamume na mwanamke walikusudiwa kuzaana ili dunia ijae viumbe walio na sura ya Mungu (Mwanzo 1:28). Ni mwanamume na mwanamke tu wanapokutana wanaweza kuunda mwanadamu mpya, na inahitaji tofauti hizo za kijinsia kufanya hivyo.

Mungu alipowapa Waisraeli Sheria, aliweka makatazo dhidi ya kutia doa jinsia. Kumbukumbu 22:5 inasema, “Haimpasi mwanamke kuvaa nguo za kiume wala mwanaume kuvaa nguo za kike, kwa maana Bwana Mungu wenu anachukia yeyote ambaye hufanya hivi.” Hii hairejelei mwanamke anaye vaa suruari refu ili kusafisha vibanda au mwanamume anayevaa aproni ili kuchoma nyoma. Aya hii inarejelea mtindo unaozidi ongezeka hii leo: kuficha kimakusudi sifa za kiume au za kike ili kujaribu kukaidi jinsia ya mtu aliyopewa na Mungu.

Sheria za Mungu daima hulenga moyo. Anajali sana nia zetu na mitazamo ya moyo kuliko matokeo ya matendo yetu. Watu wanaokataa kwa makusudi jinsia Aliyowapa wanamkataa Yeye na mpango Wake. Kimsingi, mwanamke anayevaa nguo za kujionyesha kuwa ana uwezo wa kike na kiume anamwambia Mungu, “Ulifanya makosa.” Mwanamume anayevaa nguo za jinsia nyingine au kuvaa nguo zisizoeleweka anamwambia Mungu, “Huwezi kunitimizia mahitaji yangu. Hujui unachofanya.” Zote mbili ni njia za kukaidi haki ya Mungu ya kuwa Bwana juu ya maisha yetu. Kukataa jinsia yako mwenyewe au kuificha ni mojawapo ya njia za kukufuru tunaweza kukataa haki ya Mungu ya kututawala. Ikiwa hawezi hata kupata jinsia yetu sahihi, basi anawezaje kupata kitu kingine chochote sahihi?

Baadhi wanaweza kusema kwamba kwa kuonekana kuwa na tabia kike na kiume hawakatai jinsia yao, lakini maoni ya kijamii yanayohusiana na jinsia hiyo tu. Hata hivyo, hoaja hiyo ni dhaifu mno, kwa kuwa kuna njia nyingi mbadala za kukanusha fikra potovu huku tukisherehekea sifa zinazowafanya wanaume na wanawake kuwa wa kipekee. Wanawake hawahitaji kufuata mitindo ya kipuuzi, ya kuvutia, au ya kufichua miili yao kwa sababu tu utamaduni umeonyesha uanawake kwa njia hiyo. Na wanaume wana haki ya kupinga hulka ya kutokuwa na hisia, udume inayolazimishwa na marafiki wao. Lakini uanaume na uanauke vimejikita kwa undani ya nafsi zetu kuliko vile vinavyoakisiwa nje. Jinsia ndio msingi wetu kama watu binafsi.

Mwanamke anaweza kuwa rubani wa kivita, msimamizi wa ujenzi, au dereva wa lori huku akiendelea kusherehekea ujike wake jinsi anavyoonekana. Mwanamume anaweza kuwa baba wa kukaa nyumbani, tabibu, au katibu bila kuacha uume wake. Mtindo wa kuwa na tabia ya kike na kiune huchanganya suala hilo. Haiwezekani kujua kweli na kujulikana wakati sehemu ya msingi ya mtu, jinsia yake, imefichwa. Watu wanaochagua mwonekano wa jinsia ya kiume na kike huenda wasiweze kutambua ujumbe mseto wanaotuma. Wanaweza kuamini kuwa wanapuuza jinsia katika jaribio la kuzingatia ni nani wanajiamini kuwa kweli. Kwa kweli, wanaelekeza uangalifu usiofaa kwa jinsia kwa kuibua swali akilini mwa kila mpita-njia: “Je, jinsia ni nini?”

Utamaduni wa kisasa unaenda kinyume na jinsia, unatupilia mbali maarifa ya kawaida na ukweli katika jaribio lake la kuwa “werevu” na wenye “maendeleo.” Hali ya kutokuwa kike au kiume sasa inasherehekewa, na uhalisia wa kijinsia hutazamwa kwa dharau, lakini kusherehekea kitu hakukifanyi kuwa sahihi, na kudharua kitu hakukifanyi kuwa kibaya. Utumwa wakati mmoja ulisherehekewa; hiyo haikuifanya kuwa sawa. Ajira ya watoto inakubalika katika sehemu nyingi za dunia; hiyo haiifanyi kuwa jambo nzuri. Ukahaba na ulanguzi wa watoto umekithiri katika nchi nyingi; hiyo haizifanyi kuwa sawa. Na, ingawa mkanganyiko wa kijinsia, kubadili jinsia, na mtindo wa kuwa na tabia ya kike na kiume inazidi kuwa maarufu hii leo, hiyo haizifanyi kuwa sahihi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Biblia inasema nini kuhusu kuwa na tabia za kiume na kike?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries