settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu BDSM?

Jibu


BDSM inasimamia utumwa/nidhamu/ huzuni/ kujitia uchungu kwa aibu ili kutimiza haja ya ngono. Neno hili linaweza kurejelea utamaduni mdogo wa watu wanaopenda utawala/unyenyekevu na kujitia uchungu ili kutimiza haja ya ngono, au linaweza kurejelea kwa urahisi vitendo vya wanandoa ambao hujumuisha uigizaji-dhima wa kutawaliwa/utiivu kama sehemu ya uhusiano wao wa kimapenzi. Bila shaka, Biblia haitaji BDSM, iwe kama sehemu ya mahusiano ya ngono au jambo tofauti.

Kuhusiana na “kitanda cha ndoa” (Waebrania 13:4), Biblia haitoi vizuizi vingi kwa yale ambayo wenzi wa ndoa wanaweza kufanya kingono wao wenyewe. Zaidi ya uzinzi (ngono ya watu watatu kwa mara moja, kubadilishana wenzi, n.k.) na kanda za ngono (ponografia), ambazo biblia inazitaja waziwazi na kwa uwazi kuwa dhambi, kanuni nzuri inaonekana kuwa “makubaliano ya pande zote mbili” yanayotajwa katika 1 Wakorintho 7:5. Ikiwa mume na mke wanapatana kikamilifu, bila yeyote kulazimishwa au kushawishiwa, Mungu amewapa wanandoa uhuru kuhusiana na mambo yanayotukia katika “kitanda cha ndoa.” Je, uhuru huu unaweza kujumuisha mavazi ya ngozi nyeusi, utumwa usio na vurugu, na kuigiza? Hakuna kitu katika Biblia kinachozuia waziwazi shughuli hizo.

Hata hivyo, kuna mambo ya giza katika BDSM ambayo Mkristo hapaswi kuhusika nayo. Kupokea raha ya ngono kupitia kutoa au kupokea maumivu hakupatani na kile ambacho Biblia inasema kuhusu ngono. Ngono inapaswa kuwa onyesho la upendo, mapenzi, shauku, upole, kutokuwa na ubinafsi, na kujitolea. Ngono inapaswa kuwa kielelezo halisi/kimwili cha wanandoa kuwa “mwili mmoja” (Mwanzo 2:24). Kuleta maumivu, udhalilishaji, au fedheha katika uhusiano wa kimapenzi kunapotosha jinsi inavyopaswa kuwa, hata kama kuna makubaliano ya vitendo kama hivyo. Vipengele vilivyokithiri zaidi vya BDSM vinahusiana na Ushetani/upagani na kwa hakika havina kumcha Mungu na vimepotoka.

Kuhusiana na utamaduni wa BDSM, hitaji la kutawala na/ua kutawaliwa katika uhusiano, iwe wa ngono au sio ngono, inaweza kufichua hali ya akili inayohitaji kukombolewa na Mungu kupitia Yesu Kristo. Yesu Kristo alikufa ili kutuweka huru kutokana na dhambi na matokeo yake (Luka 4:18; Wagalatia 5:1). Yesu Kristo daima alionyesha uongozi wa mtumishi, si utawala, katika mahusiano yake na wengine (Yohana 13). Haja ya kutawala na kutamani kutawaliwa haina afya kiroho. Hata kama baadhi ya vipengele “visio na hatia” au vya kufurahisha vya BDSM vinaruhusiwa katika muktadha wa ndoa, idadi kubwa ya kile kinachofanyika katika BDSM si cha Kikristo au kama Kristo kwa maana yoyote.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu BDSM?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries