settings icon
share icon
Swali

Je! Inamaanisha nini kuwa Bibilia ni pumzi ya Mungu?

Jibu


Wakati watu wanasema kuwa Bibilia ni pumzi ya Mungu, huwa wanarejelea dhana kuwa Mungu kwa uungu wote aliwashawishi uandishi wa Bibilia wa mwanadamu kwa njia ambayo kwamba chochote walichokiandika ni neno la Mungu. Kwa mjibu wa Bibilia, neno “pumzi” lamaanisha “Mungu aliwafanyia imla” pumzi yamaanisha kwamba Bibilia kweli ni neno la Mungu na inafanya Bibilia kuwa ya ajabu kati ya vitabu vyote.

Ingawa kunayo mitazamo kuwa ni kiwango gani Bibilia iko na pumzi ya Mungu, hakutakuwa na tashwishi yoyote, Bibilia yenyewe yasema kuwa kila neno la kila sehemu ya Bibilia lilitoka kwa Mungu (1 Wakorintho 2:12-13; 2 Timotheo 3:16-17). Huu mtazamo wa Bibilia huitwa pumzi ya “usemi wa nguvu” (Verbal plenary). Hiyo yamaanisha pumzi yafika hadi kwa maneno yenyewe. Si hoja pekee na kwamba pumzi yaenea sehemu zote za Bibilia na kila malengo makuu ya Bibilia. Watu wengine wanaamini kuwa sahemu za Bibilia pekee ndio ziko na pumzi au wazo pekee linalohusu mambo ya dini ndilo liko na pumzi. Lakini mtazamo huu wa pumzi unakosea vile Bibilia yajielezea yenyewe. Usemi wa nguvu pia ni kitambulisho muimu cha neno la Mungu.

Umbali wa pumzi waweza kuonekan katika 2 timotheo 3:16, “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki.” Hii aya yatwambia Mungu aliweke pumzi yake kwa Bibilia yote na ni ya manufaa kwetu. Si sehemu ya Bibilia ambayo yashughulikia imani za dini ambazo ziko na pumzi, bali ni kila neno kuanzia Mwanzo hadi Ufunuo. Kwa sababu ni la pumzi ya Mungu, Bibilia ina mamlaka yote ukifika wakati wa kuweka imani, na yatosha kufundisha mwanadamu jinsi ya kuwa na uhusiano mwema na Mungu. Bibilia yasema haina pumzi ya Mungu pekee, bali ina uwezo wa kutubadilisha na kutufanya tuwe “wakamilifu” Je! Tunaihitaji nini zaidi?

Aya nyingine ambayo inazungumzia vile Bibilia ina pumzi ya Mungu ni 2 Petero 1:21. Aya hii yatuzaidia kuelewa kuwa hata kama Mungu alitumia wanadamu kwa maumbile yao tofauti, na namna ya uandishi wao, Mungu kwa uungu alipumua lile neno waliloliandika. Yesu mweneywe alithibitisha pumzi ya usemi wa nguvu wa Bibilia wakati alisema, “Msidhani ya kuwa nalikuja kutangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amini, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wal nukta moja ya torait …..” (Mathayo 5:17-18). Katika aya hizi, Yesu anatilia nguvu ule ukamilifu wa Bibilia hata lile elezo dogo hata nukta, kwa sabau ni neno la Mungu.

Kwa sababu Bibilia ina pumzi ya Mungu, tunaweza malizia kwamba ni kamilifu na ina mamlaka yote. Mtazamo mzuri juu ya Mungu utatuelekeza kwa mtazamo mwema wa neno lake. Kwa sababu Mungu ni mwenye uwezo wote, anayejua mambo yote, na ni mkamilifu, neno lake litakua na maumbile yakee na kua na tabia zile zile. Aya hizo hizo zinazoweka msingi wa pumzi ya Bibilia pia ni kamilifu na ziko na mamlaka yote. Bila tashwishi yoyote, Bibilia iko kile yasema iko- mamlaka yasioweza kukanwa, neno la Mungu kwa wanadamu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Inamaanisha nini kuwa Bibilia ni pumzi ya Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries