settings icon
share icon
Swali

Bibilia inasema nini kuhusu utumiaji mzuri wa pesa zako?

Jibu


Bibilia iko na mengi ya kusema kuhusu usimamizi wa pesa. Kuhusu kukopa, Bibilia kwa jumla inashauri kinyume. Angalia Methali 6: 1-5; 20:16; 22: 7, 26-27 (“Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.... Usiwe mmoja wao waeekao rahani; Au walio wadhamini kwa deni za watu; Kama huna ktiu cha kulipa; Kwani ukaondolee kitanda chao chini yako”). Mara na mara tena, Bibilia inatuonya kujiwekea utajiri na inatushauri kutafuta utajiri wa kiroho badala yake. Methali 28:20, “Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.” Angalia pia Methali 10:15; 11:4; 18:11; 23:5.

Methali 6:6-11 yapeana maarifa kuhusu uzembe na utumiaji mpya wa fedha ambao utatokea. Tumeambiwa tuwatizame mchwa vile walivyo na bidii ambayo wafanya kazi kuweka hakiba chakula. Ufahamu huo pia watuonya kulala wakati tunastahili kufanya kazi kwa kitu ambacho ni cha faida. “Mtu goigoi” ni mvivu, mtu mzembe ambaye atapumzika badala ya kufanya kazi. Hatima yake imeakikishwa – umaskini na hitaji. Kwa upande mwingine mwisho wa spektra ni mtu aliyejawa na nia ya kujiwekea utajiri. Mtu kama huyo kulingana na Mhubiri 5:10 hatawai kuwa na utajiri wa kuthosha wa kumridhitisha na ataendelea kunyakua zaidi na zaidi. Timotheo wa Kwanza 6:6-11 pia yatuonya kuhusu mitego ya kudhamani utajiri.

Badala ya kuthamani kujiwekea utajiri, mfano wa bibilia ni ule wa kutoa, sio kupokea. “Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama alivokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu” (2 Wakorintho 9:6-7). Pia tumetiwa moyo tuwe watunzaji wema wa kile ambacho Mungu ametupa. Katika Luka 16:1-13 yesu alipeana mfano wa mtu mtunzaji asiye mwaminifu na kutuonya juu ya utunzaji mpaya. Maadili ya hadhiti ni “Basi kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe?”(aya ya 11). Pia tumewajibika kuwatafutia risiki wale wa nyumba yetu, vile 1 Timotheo 5:8 yatukumbusha: “Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.”

Kwa ufupi, nini Bibilia yasema kuhusu utunzaji bora wa fedha? Jibu linaweza wekwa kwa mukhtasari kwa neno moja-maarifa. Tunastahili kuwa wa maarifa na fedha zetu. Tunastahili kuweka akiba fedha, bali si kuzivuja. Tunastahili kutumia fedha, lakini kwa mwelekeo na kadirio. Tunastahili kumpatia Mungu, kwa ukarimu na thabihu. Tunastahili kutumia fedha kuwazaidia wengine, lakini kwa utambuzi na uongozi wa Roho wa Mungu. Si mokosa kuwa tajiri, lakini ni makosa kupenda pesa. Si makosa kuwa maskini, lakini ni makosa kuvuja fedha kwa vitu visivyo na maana. Ujumbe wa Bibilia ambao waendelea kila wakati kuhusu utunzaji bora wa fedha ni kuwa wa maarifa.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Bibilia inasema nini kuhusu utumiaji mzuri wa pesa zako?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries