settings icon
share icon
Swali

Je! inamaanisha nini kuwa Shetani ndiye baba wa uongo (Yohana 8:44)?

Jibu


Akisungumza na kikundi cha Wayahudi, Yesu alisema, “Ninyi ni watoto wa baba yenu ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya baba yenu. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli maana hamna kweli ndani yake. Asemapo uwongo yeye husema lugha yake asili kwa maana yeye ni mwongo na baba wa uongo” (Yohana 8:44).

Shetani ndiye “baba wa uongo” kwamba yeye ndiye mwongo wa awali. Yeye ndiye “baba” wa uongo kwa njia ile ile ambayo Martin Luther ndiye “baba” wa Mageuzi na Robert Goddard ni “baba” wa roketi za kisasa. Shetani alinena uwongo wa kwanza katika historia iliyonakiliwa kwa Hawa, katika bustani y a Edeni. Baada ya kupanda mbegu ya shaka katika akili ya Hawa kwa swali (Mwanzo 3:1), moja kwa moja anahitilafiana na Neno la Mungu kwa kumwambia Hawa, “Hakika hamtakufa” (Mwanzo 3:4). Kwa uongo huo, Shetani alimwongoza Hawa kwa kifo chake; Adamu alifuata, na hivyo sisi sote tumefuata.

Uwongo ndio silaha kuu ya Shetani dhidi ya watoto wa Mungu. Anatumia mbinu ya udanganyifu ili kuwatenga watu kutoka Baba yao wa mbinguni. Baadhi ya uwongo wake unaojulikana sana ni “hakuna Mungu,” “Mungu hakujali,” “Biblia haiwezi kuaminika,” na “matendo yako mema yatakufikisha mbinguni.” Mtume Paulo anatuambia kwamba Shetani “hujigeuza aonekane kama malaika wa nuru” (2 Wakorintho 11:14), ili kile anachokisema na kukitenda kionekane kuwa chema na cha manufaa. Lakini hio ni owongo tu.

Uwongo mwingi wa Shetani huwa unajiendeleza wenyewe. Hiki ndicho kilichotokea wakati Hawa alipomshawishi Adamu kuamini ule uwongo wa ibilisi pia. Leo hii, Shetani bado anawatumia watu kueneza udanganyifu kwa niaba yake. Mara nyingi, yeye hutumia watu wenye haiba lakini wapumbavu ili kueneza udanganyifu wake, kama vile ilivyo kwa dini na madhehbu ya uwongo,

Biblia ina majina mengi ya Shetani ya kuelezea asili yake kamili, hii inajumuisha “mtawala wa ulimwengu” (Yohana 12:310, “mungu wa dunia hii” (2 Wakorintho 4:4), “mjaribu” (1 Wathesalonike 3:5), “mdanganyifu” (Ufunuo 12:9), “Beelzebuli” (kihalisi, “bwana wa nzi,” mtawala wa mapepo, katika Mathayo 10:25), na “Beliali,” maana yake “mwovu” (2 Wakorintho 6:15).

Shetani amenena uwongo mwingi kwa watu wengi zaidi (na hata malaika) kuliko kiumbe chochote kilichowai kuumbwa. Mafanikio yake yanategemea vile watu wanaamini uwongo wake. Ametumia kila kitu kuanzia “uongo wa hadhara” hadi uwongo mkubwa unaodhihirika ili kuwadanganya watu. Adolph Hitler, mtu ambaye alijifunza jinsi ya kudanganya kwa mafanikio, wakati mmoja alisema, “ikiwa utasema uwongo mkubwa na kuurudia kila mara uwongo huo utaaminika.”

Iwe uongo ni mdogo au mkubwa hiyo sio hoja, uongo ni wa Shetani. Ikiwa umedanganya hata mara moja, basi iwapo hautatubu, hautaingia mbinguni. Biblia inafundisha waongo wote “mahali pao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili” (Ufunuo 21:8). Methali 19:9 pia inafundisha kwamba yeyote anayedanganya atahukumiwa.

Epuka hatima hii kwa kutii Marko 1:15: “Tubuni na kuiamini Habari Njema.” Yesu ndiye kweli (Yohana 14:6), na kwame hawezi kukudanganya. Wale ambao watakuja kwa Yesu kwa imani watapata kwamba “Ndipo mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! inamaanisha nini kuwa Shetani ndiye baba wa uongo (Yohana 8:44)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries