settings icon
share icon
Swali

Kipindi baada ya utawala wa miaka elf moja nini?

Jibu


Kipindi baada ya utawala wa miaka elf moja ni tafsiri ya Ufunuo sura ya 20 ambayo inaona kuja kwa Kristo mara ya pili kama utatokea baada ya "milenia," kipindi cha furaha au zama za mafanikio ya Mkristo na utawala. Hilo neno lajumlisha pamoja maoni kadhaa ya nyakati za mwisho, na ni tofauti na kipindi kabla ya miaka elfu moja (mtazamo kwamba kuja mara ya pili kwa Kristo kutatokea kabla ya ufalme wake wa milenia na kwamba ufalme wa milenia ni halisi miaka 1000 ya utawala) na kwa upunguvu kiasi, amilenia (hakuna milenia halisi).

Kipindi baada ya utawala wa miaka elf moja ni imani kwamba Kristo anarudi baada ya kipindi cha muda, lakini si lazima halisi miaka 1000. Wale wanaoshikilia mtazamo huu hawatafsiri unabii ambao haujatimia wakitumia mbinu ya kawaida, halisi. Wanaamini kwamba Ufunuo 20:4-6 haipaswi kuchukuliwa kama ilivyo. Wao wanaamini kwamba "miaka 1000" ina maana ya "kipindi cha muda mrefu." Aidha, kiambishi awali "baada ya" katika " postimilenia" inaashiria mtazamo kwamba Kristo atarudi baada ya Wakristo (si Kristo mwenyewe ) wameweka imara ufalme katika dunia hii.

Wale ambao wanashikilia postimilenia uhamini kuwa dunia hii itakuwa bora na bora bila ya kujali kinyume ya ushahidi wote - na dunia nzima hatimaye kufanywa "Wakristo." Baada ya hayo kutokea, Kristo atarudi. Hata hivyo, huku si kuitizamo dunia katika nyakati za mwisho ambayo maandiko yanawakilisha. Kutoka kitabu cha Ufunuo, ni rahisi kuona kwamba dunia itakuwa mahali pa kutisha wakati huo siku zijazo. Pia, katika 2 Timotheo 3:1-7, Paulo anaeleza siku za mwisho kama "nyakati za taabu."

Wale ambao wanashikilia postimilenia watumia njia isiyo halisi kutafsiri unabii ambao hajatimizwa, wakishirikisha maana yao wenyewe kwa maneno. Tatizo na hili ni kwamba wakati mtu anaanza kushirikisha maana kwa maneno mengine kuliko maana yao ya kawaida, mtu anaweza kuamua kwamba neno, maneno, au mstari ina maana yoyote yeye anataka umaanishe. Usawa wote unaohusu maana ya maneno utapotea. Wakati maneno yanapoteza maana yake, mawasiliano hukoma. Hata hivyo, hii sio jinsi Mungu ana nia kwa lugha na mawasiliano kuwa. Mungu anawasiliana nasi kwa njia ya neno lake lililoandikwa, kwa lengo maluum la maana ya maneno, ili joha na mawazo yaweza kuwasilishwa.

Kawaida, tafsiri halisi ya maandiko inakataa postimilenia na kushikilia tafsiri ya kawaida ya maandiko yote, ikiwa ni pamoja na unabii ambao haujatimizwa. Tuna mamia ya mifano katika maandiko ya unabii kutimia. Chukua, kwa mfano, unabii kuhusu Kristo katika Agano la Kale. Unabii huo ulitimizwa. Fikiria kuzaliwa na bikira kwa Kristo (Isaya 7:14; Mathayo 1:23) . Fikiria kifo chake kwa ajili ya dhambi zetu (Isaya 53:4-9, 1 Petro 2:24). Unabii huu ulitimizwa, na hiyo ni sababu ya kutosha kudhani kwamba Mungu ataendelea katika siku zijazo kikawaida kutimiza neno lake. Postimilenia inashindwa kwa kuwa hutafsiri unabii wa Biblia kiudhanifu na inashikilia kwamba ufalme wa milenia utaimarishwa na kanisa, si Kristo mwenyewe.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kipindi baada ya utawala wa miaka elf moja nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries