settings icon
share icon
Swali

Alama ya mnyama (666) ni nini?

Jibu


Kifungu kuu katika Biblia ambacho kinataja "alama ya mnyama" ni Ufunuo 13:15-18. Marejeo mengine yanaweza kupatikana katika Ufunuo 14: 9, 11, 15:2, 16:2, 19:20, na 20:4. Alama hii hutumika kama muhuri kwa wafuasi wa Mpinga Kristo na nabii wa uongo (msemaji wa Mpinga Kristo). Nabii wa uongo (mnyama wa pili) ndiye ambaye husababisha watu kuchukua alama hii. Alama hasa huwekwa katika mkono au paji la uso na sio kadi mtu atabeba.

Mafanikio ya hivi karibuni katika teknolojia ya matibabu ya kuwekewa sakiti changamano ya elektroniki imeibua hisia kwa alama ya mnyama ambaye inasungumziwa katika Ufunuo sura ya 13. Inawezekana kwamba teknolojia sisi tunaiona leo hii inawakilisha hatua ya mwanzo wa kile hatimaye kinaweza kutumika kama alama ya mnyama. Ni muhimu kutambua kwamba matibabu ya sakiti changamano ya elektroniki si alama ya mnyama. Alama ya mnyama itakuwa ni kitu kimepatiwa wale tu ambao huabudu Mpinga Kristo. Kuwa na matibabu au fedha ya sakiti changamano ya elektroniki kuingizwa katika mkono wako wa kulia au paji la uso si alama ya mnyama. Alama ya mnyama itakuwa nyakati za mwisho kitambulisho cha Mpinga Kristo kinachohitajika ili kununua au kuuza, na kitapewa tu kwa wale ambao wanamwabudu Mpinga Kristo.

Wafafanuzi weengi wazuri wa Ufunuo hutofautina sana kwa asili kamili ya alama ya mnyama. Licha ya mwilini kuwa na sakiti changamano ya elektroniki, kisio lingine ni pamoja na kitambulisho cha, sakiti changamano ya elektroniki, ambayo ni chale katika ngozi, au alamatu ya kubainisha kama mtu ni mwaminifu kwa ufalme wa Mpingamizi. Mtazamo huu wa mwisho unahitaji angalau uvumi, tangu haina kuongeza taarifa yoyote zaidi kwa kile ambacho Biblia inatupa. Kwa maneno mengine, yeyote mambo hayo yanawezekana, lakini wakati huo huo mwingine hayo yote ni kisio. Tusichukue muda mwingi kudadisi juu ya maelezo sahihi.

Maana ya 666 ni siri pia. Baadhi ya uvumi kwamba kulikuwa na uhusiano na mwezi wa 6, 2006-06/06/06. Hata hivyo, katika Ufunuo sura ya 13, namba 666 hubainisha mtu, si tarehe. Ufunuo 13:18 inatuambia, "Hapa ndipo penye hekima. Yeye mnyama huyo; maan ni hesabu ya sita, sitini na sita." Kwa namna fulani, namba 666 humtambua Mpinga Kristo. Kwa karne silizopita watafsiri wa Biblia wamekuwa wakijaribu kutambua baadhi ya watu wenye 666. Hakuna kubaliano kamili. Hiyo ndio sababu Ufunuo 13:18 inasema namba hii inahitaji hekima. Wakati Mpinga Kristo atafunuliwa (2 Thes 2:3-4), itakuwa wazi yeye ni nani na jinsi ya namba 666 humbainisha yeye.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Alama ya mnyama (666) ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries