settings icon
share icon
Swali

Je! Ni makosa kwa mume na mke kuwa na akiba tofauti za benki?

Jibu


Kwa sababu tofauti, wanandoa hutaka akiba tofauti za benki. Pesa ndiyo chanzo kikuu nambari moja cha mabishano katika ndoa, na kwa sababu suala la fedha ndio chanzo kikuu cha mabishano katika ndoa, wanandoa wanohusika watafanya vyema ikiwa watachukua muda wao kuamua jinsi mambo hayo yatakavyotatuliwa kabla ya kuingia kwenye ndoa. Biblia inazungumza kwa uwazi sana kuhusu kuunganishwa kwa mwanamume na mwanamke (Mwanzo 2:24; Mathayo 19:5; Waefeso 5:25-33), na mistari hiyo yote inaonyesha kwamba hao wawili watakuwa kitu kimoja, na mwanamume kama kiongozi wa kiroho na mwanamke katika kunyenyekea kwake. Hii ndiyo kanuni ambayo inapaswa kuzingatiwa katika suala la fedha kwa ujumla na akiba tofauti za benki.

Wanandoa ambao kwa kweli ni “mwili mmoja” watakuwa kitu kimoja katika nyanja zote za ndoa yao. Muhimu zaidi, watakuwa na nia moja kuhusu mambo ya kiroho. Lakini umoja huu wa roho unapaswa tena kuwa na nia moja na moyo mmoja. Hii ina maana kwamba fedha ni mali inayoonekana kuwa ya washirika wote wawili kwa uswa. Hakupaswi kuwa na toafuait kati ya “pesa yangu na pesa yako.”

Mnashiriki yote kwa usawa katika ushirikiano wa kweli, na hakuna ushirikiano unaotoshana na ule wa watu wawili kuunganishwa katika Kristo. Kwa hivyo, hakuna sababu ya kuwa na akiba tofauti za benki. Kawaida hali ya akiba tofauti za benki hutokea wakati kuna shida ya shauku, na katika hali hiyo kuna matatizo makubwa zaidi katika ndoa kuliko mahali pesa imewekwa. Ukosefu wa uaminifu ni hatari kwa ndoa, na ikiwa upo, maombi ni muhimu kutafuta hekima ya Bwana (Yakobo 1:5) juu ya jinsi ya kutatua hili.

Biblia inaseam kwamba sisi ni mwili mmoja na wenzi wetu wa ndoa, na hivyo tunapaswa kuamua kuonyesha umoja huu kwa watoto wetu, marafiki zetu, kanisa letu, na ulimwengu unaotutazama. Mahali ambapo mzozo wa pesa upo, kuna fursa ya kukua katika upendo na muhimu zaidi katika kuaminiana kuleta pamoja familia nzima kwa kusudi la Mungu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni makosa kwa mume na mke kuwa na akiba tofauti za benki?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries