settings icon
share icon
Swali

Je, kuna aina tofauti za mapepo?

Jibu


Biblia haisemi mengi kuhusu aina tofauti za mapepo. Lakini, kwa miaka mingi, waandishi mbalimbali wa kazi za kitheolojia wameazisha uainishaji mbalimbali kwa mapepo na pia habari zingine kuwahusu. Mojawapo ya zamani ambayo ni bandia ni Agano la Suleimani. Wakati wa Umri wa Kati, kazi zilizoandikwa kushughulikia mapepo ziliongezeka, na mapepo mara kwa mara yaliainishwa kulingana na ile dhambi yalikuwa yanakuza au kazi zingine walishiriki. Kwa mfano, kila moja ya “dhambi saba mbaya sana” ilisemekana ilikuwa na pepo maalum nyuma yake.

Bibilia ndiyo chanzo chetu cha pekee madhubuti ca habari kuhusu mapepo, na habari iliyo nayo kuhusu mapepo ni chache. Bibilia haisemi chochote moja kwa moja kuhusu uainishaji au aina za mapepo. Yesu anataja “aina” ya kipekee ya roho ya pepo katika Marko 9:29, lakini hakuitaja aina yake. Habari nyingi tuliyonayo kuhusu pepo imetambuliwa kwa urahisi kutoka kwa vifungu vya kibiblia ambavyo vinajukumika. Huduma za wakristo ambazo zinazingatia katika ukombozi kutoka kwa mapepo wanaweka mkazo zaidi kwao kuliko vile Biblia inafanya.

Somo la kina na la kubahatisha kuhusu mapepo limechipuka katika baadhi ya makundi ya kikristo na yenye mvuto. Roho za mapepo mbalimbali zimepewa jina kama “yezebeli,” “chatu,” “Dalilahs,” “nguva,” “Absalomu,” na kadhalika. Hakuna kati ya haya ni ya kibiblia. Maandiko hayatoi sababu ya kuamini kwamba kuna aina maalum ya mapepo au kwamba Wakristo leo hii wana kipawa cha kuzikemea au kuzifukuza. Kuvumbua aina hiyo ya elimu ya visasili ya kisasa ni kinyume na njia za Kristo.

Pengine maelezo ya pana zaidi kuhusu vita vya kiroho katika Angano Jipya, Waefeso 6:10-18 (kuhusu silaha kamili ya Mungu), inataja kwamba ”kwa maana kushinadana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya kuu wa giza hili, juu ya ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho” (mstari 12). Hata hivyo, sizitizo hapa ni kwa silaha Mungu anapeana kwa ushindi; hakuna ujuzi umetajawa wa kufunga au kufukuza nguvu za mapepo. Wakati wengine wanaona viumbe vimetajwa (wafalme, mamlaka, nguvu za giza na majeshi ya mapepo) ni kama ni uainishaji tofauti wa mah, hii ni kusoma tu ujumbe zaidi ya vile unatuambia.

Kutoka ushahidi wa kibiblia, tunatambua kwamba pepo ni malaika walioanguka ambao walimfuata Shetani wakati aliasi. Ufunuo 12 inasema kwamba joka (Shetani) alichukua thuluthi moja ya nyota kutoka mbinguni. Hata hivyo, asili ya pepo iko mbali na bayana, na hitimisho kwamba ni malaika walioanguka inapingwa na wengine. Katika Ufunuo 12:9, tunasoma, “Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.” Vile vile, katika Matayo 25:41, Yesu anasema kwamba katika Siku ya Hukumu Yeye atasema kwa watu wengine, “Ondokeni kwangu, ninyi mliolaaniwa, nendeni kwenye moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya ibilisi na malaika zake.” Hii inaweza maanisha kwamba mapepo ni malaika walioanguka wakati Shetani alianguka, au inaweza maanisha kwamba wapepo wanaitwa “malaika” kwa msingi kwamba ni “wajumbe” wa Shetani (maana halisi ya neno malaika).

Kwa uhakika tunaeza sema kwamb mapepo ni wajumbe au wafuasi wa Shetani. Neno pepo halijatumika katika Agano la Kale (ingawa roho za pepo zimetajwa), lakini kufika wakati wa Agano Jipya, wanatheolojia wa Wayahudi walikuwa wamefanya kisio nyingi kuwahusu. Dhana ya pepo au roho za pepo ilikuwa ya kawaida katika mafundisho mengine ya kikristo kwa wakati huo. Injili inaonekana kusadiki kwamba yale yalikukwa yamefundishwa kuhusu mapepo kwa wakati huo ni ukweli. Tunaona Yesu akifukuza mapepo (kwa mfano, Mathayo 8:28-33), na tunaona zinahusika kusababisha magonjwa ya kimwili, ambayo kwayo Yesu aliyaponya kwa kukemea mapepo (kwa mfano, Mathayo 9:33). Paulo anatuambia kwamba pepo ndio chanzo cha ibada ya miungu ya kikafiri na kwamba dhabihu kwa sanamu kwa kweli ni dhabihu kwa pepo (1 Wakorintho 10:19-20).

Wakati wowote kuna pengo katika elimu yetu, ni kawaida kutaka kuzijaza. Hata hivyo, katika mfano wa elimu ya mapepo, “vijazo” vingi vya habari havina msingi na wakati mwingine uvumi chefuchefu. Tunajua ya kwamba mapepo ni roho wabaya ambao, kwa pamoja na kufuata maagizo ya Shetani, vita dhidi ya Mungu na binadamu. Ni sahihi kuyafikiria kama wenza wa malaika watakatifu ambao wanahudumia watu kwa niaba ya Mungu. Tunajua kwamba wameshindwa katika kanuni na Kristo katika msalaba na kwamba hatima yao ya mwisho itakuwa masononeko ya milele katika mahali pametayarishwa kwa ajili yao (Mathayo 25:41).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kuna aina tofauti za mapepo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries