settings icon
share icon
Swali

Ni wapi Agano la Kale linatabiri kuja kwa Kristo?

Jibu


Kuna unabii wingi wa Agano la Kale kuhusu Yesu Kristo. Baadhi ya wakalimani waweka idadi ya utabii wa Masihi katika mamia.Ufuatao ni ule ambao ukuchukuliwa wazi na muhimu zaidi.

Kuhusu kuzaliwa kwa Yesu -Isaya 7:14: "Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli” Isaya 9:6: "Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume, na uweza wa kifalme utakuwa juu ya mabegani mwake. Naye ataitwa jina lake Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani." Mika 5:2: "Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katiaka Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.”

Kuhusu huduma ya Yesu na kifo Zakaria 9:9: " Furahi sana, Ee binti Sayuni; piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazam, mflame wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwana-punda, motto wa Punda” Zaburi 22:16-18: "Kwa maana mbwa wamenizunguka; kusanyiko la waovu wamenisonga; wamenizua mikono na miguu. Naweza kuihesabu mifupa yangu yote; wao wannitazama na kunikodolea macho. Wanagawanya nguo zangu, na vazi langu wanlipigia kura.”

Uwezekano wazi unabii kuhusu Yesu ni sura nzima ya 53 ya Isaya. Isaya 53:3-7 haifasiriwi kimakosa: "Alidharauliwa na kukataliwa na watu, mtu wa huzuni nyingi ajuaye sikitiko; Na kama mtu amabye watu humficha nyuso zao. Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika amehachukua masikitiko yetu, amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa. Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu. Alichubuliwa kwa maovu yetu; adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake. Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Sis sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na BWANA ameweka juu yake Maouvu yetu sisi sote. Alionewa, lakini alinyenyekea; wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kindoo apelekwaye machinjioni; Na kama vile kondoo anyamazavyo mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufnua kinywa chake.”

Unabii wa “Sabini na saba” katika Daniel sura ya 9 alitabiri tarehe sahihi kwamba Yesu, Masiya, "atauwawa.” Isaya 50:6 kwa usahihi inaeleza kule kumpiga ambako Yesu alivumilia. Zekaria 12:10 anatabiri "kule kuchomwa mkuki" Masihi, ambako kulitokea baada ya Yesu kufa juu ya msalaba. Mifano mingine mingi zaidi inaweza tolewa, lakini hii inatosha. Agano la Kale dhahiri zaidi inatabrii kuja kwa Yesu kama Masihi.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni wapi Agano la Kale linatabiri kuja kwa Kristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries