settings icon
share icon
Swali

Agano la Edeni ni gani?

Jibu


Agano la Edeni ni agano ambalo Mungu alifanya na Adamu katika Bustani mwa Edeni. Agano hili wakati mwingine linaitwa “Agano la Matendo” na ni agano la kwanza ambalo Mungu alifanya moja kwa moja na mwanadamu.

Katika Maandiko tunaona aina mbili tofauti za maagano ambayo Munug hufanya na watu. Baadhi ni maagano yasiyo na masharti, ambayo Mungu atayatimiza pasi matendo ya mwanadamu. Mengine yana masharti kwa kuwa watu lazima watii masharti ya agano ili kupokea ahadi zinazohusiana na agano hilo. Agano la Edeni ni mfano wa agano lenye masharti kwa sababu Adamu alitakiwa kutii masharti ya agano ili asipate madhara ya kulivunja.

Agano la Edeni, au Agano la Matendo, linaweza patikana katika sura za kwanza kwanza cha kitabu cha Mwanzo ambapo Mungu anatoa ahadi za masharti kwa Adamu. Agano la Edeni haliitwi kwa wazi agano katika kitabu cha Mwanzo; ingawa, baadaye linarejelewa kuwa agano katika Hosea 6:7, “Wamevunja Agano kama Adamu: huko hawakuwa waaminifu kwangu.”

Ingawa baadhi ya wanatheolojia wataorodhesha majukumu sita hivi tofauti ambayo Adamu alipaswa kutunza, kiini cha Agano la Edeni ni amri ya Mungu kwa Adamu kuwa asikule kutoka “matunda ya mti wa kujua mema na mabaya” (Mwanzo 2:16-17). Amri hiyo inaonyesha wazi ahadi ya Mungu na vile vile adhabu ikiwa Adamu ataasi.

Katika Agan la Edeni, Mungu alimwahidi Adamu uzima na baraka, lakini ahadi hiyo ina masharti ya kadri jinsi Adamu atakavyo tii amri ya Mungu ya kutokula tund la mti wa kujua mema na mabaya (Mwanzo 2:16-17). Adhabu ya Adamu ya kutotii ingekuwa kifo cha kimwili na cha kiroho pamoja na laana juu ya ardhi ili Adamu afanye kazi kwa bidi zaidi katika kukuza mimea. Mojawapo ya matokeo ya dhambi ya Adamu ilikuwa kwamba angelazimika kula kwa jasho siku zote hadi kifo chake (Mwanzo 4:17-19).

Agano hili lina sehemu muhimu katika kufunuliwa kwa mpango wa Mungu wa ukombozi, vile linavyoenyesha udhaifu wa mwanadamu wa kutunza uhusiano unaofaa na Mungu hata wanapokuwa katika paradiso ya kidunia ambayo Mungu aliwaumbia.

Dhambi ya Adamu ilivunja agano hili la masharti na Mungu na kuwaacha wanadamu katika hali ya kuanguka, lakini Mungu karibuni alifanya agano la pili lisilo la masharti la ukombozi kwa Adamu na Hawa (Mwanzo 3:14-24). Kama Agano la Edeni, hili hili haliitwi moja kwa moja agano katika Mwanzo, lakini ni ahadi ya muhimu ambayo Mungu aliifanya kwa wanadamu. Ni ahadi ya kwanza ya ukombozi na ahadi ya kwanza ya ujio wa Kristo (Mwanzo 3:15). Ni sura tatu tu za hiki kitabu cha ajabu ambapo Mungu tayari ametupa tumaini la Mkombozi. Mwanzo 3:15 wakati mwingine hurejelewa kama injili ya kwanza, tangazo la kwanza la injili katika Maandiko. Ahadi ya Mungu kwa Hawa kwamba uzao wa nyoka utauma uzao wa Hawa kisigino na uzao wa Hawa utauponda uzao wa nyoka kichwani, ni utabiri kwamba Shetani angemjeruhi Kristo msalabani, lakini Kristo angemshinda Shetani katika msalaba huohuo.

Maagano yote, la Edeni na la lile linalofuata la Ukombozi ni ya maana kwa sababu nyingi. Kwanza, yanaanzisha utaratibu wa kurudiwa katika Maandiko yote: 1) mwanadamu anatenda dhambi 2) Mungu anahukumu dhambi, na 3) Mungu hutoa neema na huruma kwa kutoa njia ya kukomboa mwanadamu na kurejesha uhusiano wa mwanadamu na Mungu. Pili, agano linatuonyesha kwamba daima dhambi ina madhara yake. Kuelewa maagano hayo tofauti katika Agano la Kale na uhusiano kati ya maagano hayo ni jambo la muhimu katika kuelewa uhusiano wa agano la Mungu na watu wake waliochaguliwa pamoja na mpango wake wa ukombozi kama vile ulivyofunuliwa katika Maandiko.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Agano la Edeni ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries