settings icon
share icon
Swali

Je! adhabu ya kibiblia kwa uzinzi ni ipi?

Jibu


Kabla ya kujibu swali hili, ni muhimu kufafanua tofauti kati ya Agano la Kale na Agano Jipya. Chini ya sheria ya Agano la Kale, iliyotolewa kwa Israeli ya kale chini ya utawala wa makasisi, adhabu ya uzinzi ilikuwa kifo (Walawi 20:10). Katika Agano Jipya, Yesu alileta sheria mpya katika matumizi. Mshahara wa dhambi bado ni mauti ya milele (Warumi 6:23), lakini uzinzi haubebi tena hukumu ya kifo kulingana na sheria. Wakristo wa kisasa hawaishi chini ya utawala wa makasisi kale na hawajaamriwa kuwadhuru wale wanaotenda dhambi.

Sheria ya Agano la Kale inaorodhesha idadi ya tabia ambazo ziliadhibiwa kwa kifo, ikiwa ni pamoja na uzinzi. “Ikiwa mtu atazini na mke wa mtu mwingine, yaani mke wa jirani yake, wazinzi hao wawili lazima wauawe” (Walawi 20:10). Ni muhimu kutambua kwamba adhabu ilikuwa sawa kwa wote wawili waliohusika. Hakukuwa na mapendeleo yaliyotoa udhuru kwa mapenzi ya kiholela ya mwanamume; aliadhibiwa pamoja na mwanamke aliyepatikana naye. Sheria hii na zinginezo kuhusu usherati katika Walawi 20 zimefunganishwa na hitaji lakutenganishwa kabisa kwa maadili ya Israeli na mataifa mengine. Wakanaani walikuwa wamejulikana kwa uasherati wao, miongoni mwa mambo mengine, na Mungu alitaka Israeli wawe watakatifu, au “kutengwa,” kutoka kwao (mistari ya 22-24). Tena, sheria hii ilitolewa kwa Israeli kama sehemu ya Agano la Musa. Kanisa si Israeli, na sisi hatuishi chini ya Agano la Kale.

Leo hii, Biblia haipendekezi adhabu yoyote kama hiyo kwa uzinzi. Hata hivyo, tendo la uzinzi hubeba adhabu yake yenyewe. Dhambi ya ngono ni kosa linalotendwa dhidi ya mwili wa mtu mwenyewe (1 Wakorintho 6:18). Kitabu cha Mithali kinaonya juu ya matokeo ya uzinzi: kupoteza heshima na nguvu (Mithali 5:9-11), sifa iliyoharibiwa (Mithali 5:14), utumwa na kifo (Mithali 5:22-23), kujiangamiza (Mithali 6:32), na kisasi cha mume mwenye wivu (Mithali 6:24). “Je, mtu aweza kuchotea moto kwenye paja lake bila nguo zake kuungua? Je, mtu aweza kutembea juu ya makaa ya moto yanayowaka bila miguu yake kuungua? Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa mwanaume mwingine; hakuna yeyote amgusaye huyo mwanamke ambaye hataadhibiwa” (Mithali 6:27-29).

Mithali pia inaelezea tabia ya mzinzi: anaitwa mjinga na mpumbavu (Mithali 7:7) na kulinganishwa na mnyama aliyenaswa katika mtego na kuchinjwa (Mithali 7:22-23). “Lakini mwanaume aziniye na mwanamk
afanyaye hivyo hujiangamiza mwenyewe” (Mithali 6:32). Hatimaye mwandishi wa mithali afikia mkataa huu wa kuhuzunisha sana kuhusu uzinzi: “Aliowaangusha ni wengi; aliowachinja ni kundi kubwa. Nyumba yake ni njia kuu iendayo kaburini, ielekeayo chini kwenye vyumba vya mauti” (Mithali 7:26-27).

Kusoma maonyo haya katika Mithali kunapaswa kuleta hofu katika moyo wa mtu yeyote. Jinsi sheria ya Agano la Kale inavyoonekana kuwa kali kuhusu adhabu ya uzinzi, matokeo ya kiroho ni mabaya zaidi. Jambo la kushukuru ni kwamba dhambi ya uzinzi hajawachwa nje ya ahadi ya Yesu ya msamaha. Inatubidi tu kutazama hadithi katika Yohana 8 kuhusu mazungumzo wa Yesu na mwanamke mzinzi aliyekamatwa katika tendo lile lile na kuburutwa mbele zake na Mafarisayo-ili kuona moyo wa Mungu kwa yule aliyenaswa katika mtego wa dhambi. Mafarisayo wako tayari na wana hamu ya kutoa adhabu isiyo na huruma juu ya mwanamke (bali si mwanaume), na Yesu anawakemea kwa kuwakumbusha kwamba wao ni wenye dhambi kama yeye. Kisha, wakati wote wameondoka kwenye eneo hilo, Anamuuliza kwa upole, “Wako wapi wale waliokuwa wanakuhukumu kuwa mwenye hatia?” Yule mwanamke akajibu, “Hakuna hata mmoja Bwana… Nenda zako, kuanzia sasa usitende dhambi tena” (Yohana 8:10-11)

Yesu amejawa neema na kweli (Yohana 1:14). Anamwambia mwanamke aache uzinzi, naye anamsamehe. Hii ni picha ya ajabu ya Yohana 3:17: “Kwa maana Mungu hakumtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu, bali kupitia kwake ulimwengu upate kuokolewa.” Adhabu ya uzinzi, au kwa dhambi nyingine yoyote, inafutwa tunapokubalia Kristo kuchukua adhabu hiyo kwa ajili yetu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! adhabu ya kibiblia kwa uzinzi ni ipi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries