settings icon
share icon
Swali

Kwa nini siwezi koma kutenda dhambi? Tafadhali nisaidie?

Jibu


Kila muumini, kwa wakati mmoja au mwingine, ameomboleza kutokuwa na uwezo wa kuacha kutenda dhambi. Wakati tunajiribu kufikiria, shinda inatokana na udhaifu wetu, kukosa uwezo wa kuacha kutenda dhambi kwa kawaida inaonyesha kasoro katika ufahamu wetu wa nguvu za Mungu. Wakati hatufahamu uwezo Wake wa kuokoa, kusamehe, na kututakaza kutoka njia sisizo adilifu (1 Yohana 1:9), tunaweza patikana katika mzunguko wa uharibifu wa dhambi, hatia, na hofu, ambayo inaleta ukosefu wa raha katika wokovu wetu, ambayo inaleta dhambi zaidi.

Katika Zaburi 51:12, Daudi anamsihi Mungu, “Unirudishie furaha ya wokovu wangu; Unitegemeze kwa roho ya wepesi.” Aliandika haya baada ya kuanguka katika dhambi mbaya sana ya uzinzi na mauaji. Inavutia kutambua kwamba anamuuliza Mungu kumrudishia furaha ya wokovu wake. Furaha ni ufunguo katika ushindi wetu juu ya dhambi. Ni muhimu pia kufahamu kwamba Mungu anatutegemeza “kwa roho ya wepesi.” Mungu huiona furaha katika kutuokoa, na sisi tunakuwa na furaha katika kuokolewa.

Mungu ametuokoa kwa kupenda, ili kudhihirisha neema, upendo na uwezo Wake. Wokovu wetu hautegemei kiwango tumefanya dhambi, kiwango tunainjilisha au kutubu au kufanya kazi nzuri, jinsi tunavyopenda au kutopenda, au kitu chochote kingine kutuhusu. Wokovu wetu ni uzao kabisa wa neema, upendo, na lengo la Mungu (Waefeso 2:8-9). Ni muhimu kufahamu hili, kwa sababu (kinaya) kuamini kwamba tuna jukumu la kutii sheria inayoongoza hadi hali ya kwa kutokuwa na uwezo wa kuacha kutenda dhambi.

Paulo anafafanua hili katika Warumi 7:7-10. Wakati tunafahamu sheria, kama vile “usitamani,” asili ya dhambi yetu inaasi kabisa dhidi ya sheria hiyo, na tunatamani. Hii ni hali ya binadamu—kwa urahisi hivyo ndivyo tilivyo. Sheria inakuza asili ya dhambi yetu. Neema ya Mungu inaweza kufanya kile sheria haiwezi kufanya kamwe: kututakaza kutoka kwa dhambi.

Kwa hivyo, njia ya kuacha kufanya dhambi sio kuongeza kanuni zaidi. Mungu alijua hili. Kwa kweli, alitupa sheria ili tuweze kutambua dhambi zetu na kumrudia Yeye (Warumi 3:19-20; Wagalatia 3:23-26). Sheria ni nzuri. Ni ishara ya asili ya Mungu na ukamilifu Wake. Lakini hatukupewa kwa wokovu wetu. Kristo alitutimizia sheria (Mathayo 5:17).

Wakati tunakosa kuelewana na Mungu na kushikilia fikra kwamba lazima tutimize sheria, tunapoteza furaha yatu katika wokovu na kujitenga kwa kushindwa kwetu wenyewe. Tunang’ang’ana chini ya mzigo mzito. Tunahisi kushinikizwa kufanya kitu ili kupata wokovu, lakini, wakati huo huo, asili ya dhambi yetu inatuacha bila uwezo wa kutii sheria. Tunapozingatia sheria zaidi, asili ya dhambi yetu inaasi zaidi. Asili ya dhambi yetu inapoasi zaidi, tunakuwa na hofu zaidi kwamba hatujaokolewa. Tunapokuwa na hofu zaidi na kukosa furaha, ndivyo ahadi ya furaha ya dhambi inavyotuvutia zaidi.

Njia pekee ya kuvunja mazoea na kuacha kutenda dhambi ni kukubali ukweli kwamba hatuwezi kuacha kutenda dhambi. Hii inaweza kuonekana kinzani, lakini ikiwa mtu hataacha kujaribu kijiokoa mwenyewe, hawezi kupumzika katika ufahamu kwamba Mungu amemwokoa. Furaha ya wokovu inatoka katika kukubali ukweli kwamba neema ya Mungu imetufunika, kwamba atatubadilisha na kutufananisha na mfano wa Kristo, na kwamba ni kazi Yake, sio yetu (Warumi 8:29; Wafilipi 2:13; Waebrania 13:20-21). Mara tu ukweli huu umeshikwa kwa kweli, dhambi inapoteza nguvu yake. Hatuhisi tena msukumo wa kurudi kwa dhambi kama njia ya msaada ya muda kutoka kwa wasiwasi, kwa sababu wasiwasi na shinikizo zimetulizwa kwa ukamilifu na Kristo (Waebrania 10:10, 14). Basi, kazi njema tunazokamilisha katika imani zinafanyika kwa sababu ya upendo na furaha badala ya hofu au wajibu.

“Uchungu wa mauti ni dhambi na nguvu ya dhambi ni sheria. 57 Lakini ashukuriwe Mungu, yeye atupaye ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, simameni imara, msitikisike, mzidi sana katika kuitenda kazi ya Bwana, kwa maana mnajua ya kuwa, kazi yenu katika Bwana si bure” (1 Wakorintho 15:56-58).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini siwezi koma kutenda dhambi? Tafadhali nisaidie?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries