settings icon
share icon
Swali

Ni unabii gani wa biblia uliotimizwa kitika mwaka wa AD 70 (baada ya Yesu kuzaliwa AD70)?

Jibu


Mengi ya muhimu yalitukia Israeli katika mwaka wa AD 70, na wengi uhusisha matukio ya wakati huo na unabii katika Biblia. Katika kulipekua swala hili, ni vyema kukumbuka kwamba unabii hauelezei wakati ujao njia sawia na vile historia inavyoelezea kale. Ndio maana kunazo aina tafauti za tafsiri ya unabii wa kibiblia. Utabiri unaohusu nyakati za mwisho, ni aina inayojulikana kama eskatolojia (tawi la theolojia linalojishughulisha na kifo, hukumu, pepo na jahanamu), ni ya kuvutia kwa watu wengi. Miongoni mwa Ukristo wa kisasa, wingi wa majadaliano haya yanatilia mkazo ni lini tukio litatokea na wala sio ni matukio gani yanatabiriwa. Joha ya wastani ya kurejelea kwa mitazamo hii ni umuhimu wa mwaka wa AD 70, wakati Ufalme wa Kirumu uliiharibu hekalu ya Kiyahudi.

Kwa bayana tafsiri zote za Kikristo za unabii wa kibiblia zinakubaliana kwamba wingi wa unabii ulitimizwa katika au kabla ya mwaka wa AD 70. Yesu alitabiri kuharibiwa kwa hekalu (Luka 21:6; Matayo 24:2) na wengine wanatoa hoja kuwa pia alitabiri mauaji ya halaiki ya Wayahudi mikononi mwa Rumi (Luka 23:27-31). Kihistoria, matukio haya yanaambatana vizuri sana na kauli ya Yesu. Kuna upana wa makubaliano miongoni mwa tafsiri za Kikristo kwamba nabii hizi zilitimizwa mnamo mwaka wa AD 70.

Kuna mjadala kuhusu ikiwa unabii wa ziada, kama vile ule unaopatikana katika Danieli mlango wa 9, Matayo mlango wa 24 na 25, na Ufunuo mlango wa 6-18 pia ulitimizwa katika mwaka wa AD 70 au bado haujatimizwa. Wale wanaoamini kuwa unabii huo ulitimizwa kabla au wakati wa mwaka wa AD 70 na wale wanaoamini kuwa unabii wote umetimia hata ule wa ujio wa Yesu Kristo, wote wanashikilia kwamba, ikiwa sio matukio yote ya unabii yalikamilika takribani mwisho wa karne ya kwanza, wingi wao basi ulitimia kabla ya mwaka wa AD 70. Wale wanao shikilia kuwa Agano la Kale na Agano Jipya zote zinafasiriwa kwa tafsiri ya kisarufi-kihistoria, wanakanuni kwamba uharibifu wa hekalu pekee na pengine mauaji ya halaiki yote yalitimia katika mwaka wa AD 70 na kwamba unabii uliosalia wote utatimizwa mbeleni wakati wa kipindi cha dhiki.

Kwa mujibu wa ushahidi wa kihistoria, kuna uhaba kuwezesha kufanya kauli ya njia moja au nyingine. Matukio ya AD 70 yanaweza kufanywa yaingiane na madai fulani ya unabii, hii ikitegemea mtazamo wa mtu. Bila shaka, ikiwa mtu yuko tayari kutumia kiwango cha juu cha tafsiri ishara, unabii wowote unaweza kufanywa kuenda na takribani tukio lolote. Lazima ikumbukwe, hata hivyo wengi wa wale wasioshikilia tafsiri kuwa unabii wote umetimia hata ule wa ujio wa Yesu Kristo, kitabu cha Ufunuo lazima kiliandikwa kabla ya mwaka wa AD 70, hatua ambayo wadadisi wengi wa theolojia hawaungi mkono.

Matatizo makubwa katika kudai kuwa unabii wote ulitimia mwaka wa AD 70 ni tatizo la kitheolojia. Hasa, wanaoshikilia kauli kuwa unabii wote wa biblia ushatimizwa au sehemu ya unabii haijatimizwa bado, unahitaji muktadha wa maandiko, wahitaji kutafsiriwa kwa mtangamano wa maana halisi na lugha ya kimafumbo. Mtu lazima atafsiri maneno, mistari na vifungo ambavyo vinaonekana katika masingira, au hata ibara moja, lakini kwa dhana tofauti ya kielezi-tamathali.

Tafsiri bora ni kuwa mauaji ya halaiki na uharibifu wa hekalu ni unabii uliotimia katika mwa wa AD 70, na matukio mengine ambayo yameelezewa katika Danieli, Mathayo, na Ufunuo bado hayajatokea. Hakika ni utabiri wa nyakati za mwisho.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni unabii gani wa biblia uliotimizwa kitika mwaka wa AD 70 (baada ya Yesu kuzaliwa AD70)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries