settings icon
share icon
Swali

Je, kuna uwezekano kwamba vitabu zaidi vinaweza kuongezwa kwa Biblia?

Jibu


Hakuna sababu ya kuamini kwamba Mungu anatoa ufunuo zaidi wa kuongezea neno lake. Biblia huanza na mwanzo wa binadamu -Mwanzo - na kuishia na mwisho wa binadamu vile sisi tunajua -Ufunuo. Kila kitu kalioko hapo kati kati ni kwa faida yetu kama waumini, kwa kuwa uwezo na ukweli wa Mungu katika maisha yetu ya kila siku. Tunajua hili kutoka 2 Timotheo 3:16-17 , "Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema."

Kama vitabu zaidi viliongezwa kwa Biblia, Hiyo itakuwa sawa na kusema kwamba Biblia tunayo hii leo haijakamilika - kwamba haituambii kila kitu tunahitaji kujua. Ingawa inatumika tu moja kwa moja kwa kitabu cha Ufunuo, Ufunuo 22:18-20 inatufundisha ukweli muhimu kuhusu kuongeza kwa neno la Mungu : "Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika ktiabu hiki. Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atmwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu..."

Tuna kila kitu ambocho tunahitaji katika vitabu 66 vya Biblia. Hakuna hali hata moja katika maisha ambayo haiwezi kushughulikiwa na maandiko. Kilicho anzishwa katika Mwanzo hupata hitimisho katika Ufunuo. Biblia kabisa imekamilika na ya kutosha. Mungu anaweza kuongeza Biblia? Bila shaka Anaweza. Hata hivyo, hakuna sababu , kibiblia au kiteolojia, kuamini kwamba Yeye anaenda kufanya hivyo, au kwamba kuna haja yoyote Yeye kufanya hivyo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kuna uwezekano kwamba vitabu zaidi vinaweza kuongezwa kwa Biblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries