settings icon
share icon
Swali

Biblia inafundisha nini juu ya utatu?

Jibu


Mungu ni mkubwa kuliko sisi na tusitarajie kumuelewa katika kila jambo. Utatu ni jambo gumu kulieleza kwa kina. Hakuna mwanadamu anayeweza kulielewa kwa undani zaidi. Biblia inafundisha kuwa Baba ni Mungu, ya kuwa Yesu ni Mungu na pia Roho mtakatifu ni Mungu. Biblia pia inafundisha kuna Mungu mmoja tu. Ijapokuwa tunaweza kufahamu uhusiano tofauti tofauti wa sehemu za utatu huu ni vigumu kuelewa kwa akili ya kibinadamu. Hii haimaanishi kuwa si kweli au si maagizo ya Biblia.

Utatu ni Mungu mmoja katika nafsi tatu. Aya za biblia zifuatazo zitatumika kufafanua neno hili.

1) Kuna Mungu mmoja: kumbukumbu la torati 6:4; wakorintho wa kwanza 8:4; wagalatia 3:20; Timotheo wa kwanza 2:5.

2) utatu una nafsi tatu: mwanzo 1:1; 1:26; 3:22; 11:7 Isaya 6:8; 48:16; 61:1; Mathayo 3:16-17; Mathayo 28:19; wakorintho wa pili 13;14. Katika mwanzo 1:1 neno la wingi “Elohim” linatumika. Katika mwanzo 1:26; 3:22; 11:7 na Isaya 6:8, neno la wingi “sisi” limetumika. Kwa hivyo neno “Elohim’ na “sisi” kumaanisha zaidi ya mmoja halina pingamizi.

Katika Isaya 48:16 na 61:1, Mwana azungumza huku akihusisha Baba na Roho Mtakatifu. Fananisha Isaya 61:1na Luka 4:14-19 kuona Mwana akizungumza. Mathayo 3:16-17 inaelezea ubatizo wa Yesu. Anayeonekana hapa ni Mungu Roho mtakatifu akimshukia Mungu Mwanahuku Mungu Baba akitangaza furaha yake katika Mwana. Mathayo 28:19 na wakorintho wa pili 13:14 ni mifano ya nafsi tatu katika Mungu mmoja.

3) Nafsi hizi tatu zinatambulika katika maandiko. Katika agano la kale “ BWANA” linatofautishwa na “Bwana” (mwanzo 19:24; Hosea 1:4). “BWANA” ana “Mwana” (zaburi 2:7, 12; Methali 30:2-4). Roho anatofautishwa na “BWANA” (hesabu 27:18) na pia kutoka “Mungu” (zaburi 51:10-12). Mungu mwana atofautishwa na Mungu Baba (zaburi 45:6-7; waebrania1:8-9). Katika agano jipya, Yohana 14:16-17 ndipo Yesu anazungumza na Baba juu ya kuleta Msaidizi, Roho mtakatifu. Hii ina maana ya kuwa Yesu hakujichukulia yeye mwenyewe kuwa Baba wala Roho Mtakatifu. Katika kila mahali ndani ya agano jipya Yesu alipozungumza na Mungu Baba alikuwa akizungumza na nafsi moja wapo ya Utatu – Baba.

4) kila nafsi katika utatu huu ni Mungu: Baba ni Mungu: Yohana 6:27; warumi 1:7; petro wa kwanza 1:2. Mwana ni Mungu: Yohana 1:1, 14; warumi 9:5; wakolosai 2:9; waebrania 1:8; Yohana wa kwanza 5:20. Roho mtakatifu ni Mungu: Matendo ya mitume 5:3-4; wakorintho wa kwanza 3:16 (anayedumu ndani ni Roho mtakatifu –warumi 8:9; Yohana 14:16 –17; Matendo ya mitume 2:1—4).

5) Katika mpangilio ndani ya utatu huu: maandiko yanaonyesha kuwa Roho Mtakatifu humtumikia Baba na Mwana na Mwana humtumikia Baba. Huu ni uhusiano wa ushirika wao wala hupunguzi uungu wa nafsi yoyote ile. Kuhusu Mwana tazama: luka 22:42; Yohana 5:36; Yohana 20:21; Yohana wa kwanza 4:14. kuhusu Roho Mtakatifu tazama Yohana 14:16; 14:26; 15:26; 16:7 na hasa Yohana 16:13-14.

6) Majukumu ya kila nafsi katika utatu: Baba ndiye aliyesababisha kuwako kwa 1) ulimwengu (wakorintho wa kwanza 8:6; Ufunuo wa Yohana 4:11), 2) ufunuo wa kimungu (Ufunuo wa Yohana 1:1) 3)wokovu (Yohana 3:16-17); Matendo ya kibinadamu ya Yesu ( Yohana 5:17; 14:10). Baba anaonekana kwanza katika haya yote.

Mwana ni wakala ambaye Baba humtumia kufanyia haya: 1) Kuumba na kustawisha ulimwengu (wakorintho wa kwanza 8:6; Yohana 1:3; wakolosai 1:16-17); 2) ufunuo wa kimungu (Yohana 1:1; Mathayo 11:27; Yohana 16:12-15; Ufunuo wa Yohana 1:1); na 3) wokovu ( wakorintho wa pili 5:19; Mathayo 1:21; Yohana 4:42). Baba alifanya mambo haya yote kupitia Mwana anayetenda kazi kama mwakilishi wake.

Roho Mtakatifu ndiye anayetumiwa na Baba kufanya haya: 1) uumbaji na ustawishaji wa ulimwengu (mwanzo 1:2; Ayubu 26:13; zaburi 104: 30); 2) ufunuo wa kimungu (Yohana 16:12-15; waefeso 3:5; petro wa pili 1:21); 3) wokovu (Yohana 3:6; Tito 3:5; petro wa kwanza 1;2); na 4) matendo ya Yesu ( Isaya 61:1; Matendo ya mitume 10;38). Haya yote Baba ayatenda kupitia Roho Mtakatifu.

Baba, Mwana na Roho si vipande vya Mungu bali kila nafsi ni Mungu. Mungu asiyeonekana na macho hawezi kuelezwa kwa usahihi na mwenye kuona na macho ya kibinadamu akaeleweka. Lakini katika hali zote tazama Mungu kama nafsi tatu zisizogawanyika kuwa Miungu mitatu bali Mungu mmoja tu. “jinsi zilivyo kuu utajiri wa hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani! Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana?” 9 warumi 11:33-34)

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inafundisha nini juu ya utatu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries