settings icon
share icon
Swali

Ukanaji Mungu ni nini?

Jibu


Ukanaji Mungu ni mtazamo kuwa Mungu haishi. Ukanaji Mungu sio jambo geni. Zaburi 14: 1, iliyoandikwa na Daudi karibu mwaka 1000 kabla Yesu azaliwe wataja ukanaji Mungu: “Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu.” Takwimu za hivi karibuni zaonyesha ongezeko la idadi ya watu wanaodai kuwa wao ni wakanaji Mungu, kufikia asili mia 10 ya watu ulimwengu mzima. Kwa hivyo ni kwa nini watu wengi wanaendelea kuwa wakanaji Mungu? Je! Ukanaji Mungu kwa kweli ni msimamo wa kimantiki vile wakanaji Mungu wanavyo dai?

Ni kwa nini ukanaji Mungu upo? Ni kwa nini Mungu hajidhihirishi Yeye mwenye kwa watu, kuthibitisha kuwa ako hai? Kwa kweli kama Mungu atatokea hivi tu, fikirio litakuwa, kila mtu atamwamini! Shida hapa ni kwamba, sio mapenzi ya Mungu kuwathibitishia watu kuwa anaishi. Ni mapenzi ya Mungu kuwa watu wamwamini kwa imani (2 Petero 3:9) na kukubali kwa imani kibaji chake cha wokovu (Yohana 3:16). Mungu kwa uwazi alidhihirisha uewepo wake mara nyingi sana katika Agano la Kale (Mwanzo 6:9; Kutoka 14: 21-22; 1 Wafalme 18:19-31). Je! Watu waliamini kuwa Mungu anaishi? Naam. Je! Waligeuka kutoka kwa njia zao za dhambi na kumtii Mungu? La. Ikiwa mtu hayuko tayari kukubali kuwepo kwa Mungu kwa imani, basi huyo mtu hayuko karibu kumkubali Yesu Kristo kama mwokozi kwa imani (Waefeso 2:8-9). Thamanio la Mungu ni watu wawe kama Kristo, sio wakanaji Mungu (wale wanaoamini kuwa Mungu anaishi).

Bibilia inatuambia kwamba uwepo wa Mungu lazima ukubalike kwa imani. Waebrania 11:6 yasema, “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.” Bibilia inatukumbusha kuwa tumebarikiwa wakati tunamwamini Mungu kwa imani: “Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki”’ (Yohana 20:29).

Uwepo wa Mungu lazima ukubalike kwa imani, lakini hii haimanishi kuwa imani katika Mungu ni ile isio na mantiki. Kunayo pingamizi nyingi nzuri sana juu ya kuwepo kwa Mungu. Bibilia inatufunza kwamba kuwepo kwa Mungu kunaonekana katika ulimwengu (Zaburi 19:1-4), katika uumbaji (Warumi 1:18-22), katika mioyo yetu wenyewe (Mhubiri 3:11). Kwa hayo yote yamesemwa, uwepo wake Mungu hauwezi thibitika; lazima ukubalike kwa imani.

Kwa wakati huo huo, inagharimu imani kubwa sana kuamini ukanaji Mungu. Kufanya habari ya kijumla “Mungu haishi” ni kufanya tangazo kuwa kila kitu chastahili kujua kujua juu ya kila kitu, na kwa vile ako kila mahali katika ulimwengu na baada ya kushuhudia kila kitu kinachostahili kuonekana. Ingawa hakuna mkanaji Mungu atakaye fanya hili tangazo. Ingawa hasa hiyo ndioyo wanasema wakati wanasema kuwa kamwe Mungu haishi. Wakanaji Mungu hawawezi kuthibitisha kuwa Mungu haishi, kwa mfano, maisha katikati mwa jua, au chini ya mawingu ya Jupita, au kaitka umbali wa jamii ya nyota nyingi sana za umbali. Jinsi mahali papo ni zaidi ya utazamo wetu, haiwezi thibitika kuwa Mungu haishi. Inagharimu imani kubwa sana kuwa mkanaji Mungu.

Ukanaji Mungu hauwezi thibitika, na uwepo wake Mungu lazima ukubalike kwa imani. Kawaida, Wakristo wanaamini kwa dhati kuwa Mungu anaisi, na kukubali kuwa kuwepo kwake Mungu ni jambo la imani. Kwa wakati huo, tunaikataa hoja kuwa kuwa na imani katika Mungu ni sio ya kimantiki. Tunaamini kuwa uwepo wa Mungu unaweza kuonekana, kwa umakini unaweza kuhisika, na kuthibitka kuwa wa muimu kifalsafa na kisayansi. “Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake. Mchana husemezana na mchana, Usiku hut0lea usiku maarifa. Hakuna lugha wala maneneo, Sauti yao haisikilikani. Sauti yoa imeenea duniani mwote, Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu, Katika hizo ameliwekea jua hema” (Zaburi 19:1-4).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ukanaji Mungu ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries