settings icon
share icon
Swali

Tunawezaje kupata uhuru wa kweli katika Kristo?

Jibu


Kila mtu anatafuta uhuru. Hasa katika Magharibi, uhuru ni maadili ya juu zaidi, na inatafutwa na wote ambao ni, au wanajiona kuwa ni, waliodhulumiwa. Lakini uhuru katika Kristo sio sawa kama uhuru wa kisiasa au kiuchumi. Kwa hakika, baadhi ya watu waliodhulumiwa sana katika historia wamekuwa na uhuru kamili katika Kristo. Biblia inatuambia kwamba, kusema kiroho, hakuna mtu aliye huru. Katika Warumi 6, Paulo anaelezea kuwa sisi wote ni watumwa. Sisi ni watumwa labda wa dhambi au watumwa wa haki. Wale ambao ni watumwa wa dhambi hawawezi kujiokoa wenyewe, lakini mara tu sisi tunaokolewa kutoka kwenye adhabu na nguvu za dhambi kupitia msalaba, tunakuwa aina tofauti ya watumwa, na katika utumwa huo tunapata amani kamili na uhuru wa kweli.

Ingawa inaonekana kama kinyume, uhuru wa pekee wa kweli katika Kristo huja kwa wale ambao ni watumwa Wake. Utumwa umekuja kumaanisha kushusha hadhi, dhiki, na kutokuwa sawa. Lakini kielelezo cha kibiblia ni uhuru wa kweli wa mtumwa wa Kristo ambaye hupata furaha na amani, matokeo ya uhuru wa pekee wa kweli tutakaojua katika maisha haya. Kuna matukio 124 katika Agano Jipya la neno doulos, ambalo linamaanisha "mtu ambaye ni wa mwingine" au "mtumwa asiye na haki za umiliki wake mwenyewe." Kwa bahati mbaya, matoleo ya kisasa ya Biblia, pamoja na King James Version, mara nyingi hutafsiri doulos kama "mtumishi" au "mtumishi wa utumwa." Lakini mtumishi ni mmoja anayefanya kazi kwa ajili ya mshahara, na ambaye, kutokana na kazi yake, anastahili kitu kutoka kwa bwana wake. Mkristo, kwa upande mwingine, hana chochote cha kumpa Bwana kwa malipo ya msamaha wake, na yeye amemilikiwa kabisa na Bwana ambaye alimnunua yeye kwa damu Yake iliyomwagika msalabani. Wakristo wanunuliwa kwa damu hiyo na ni milki ya Bwana na Mwokozi wao. Hatukuajiriwa na Yeye; sisi tunamilikiwa na Yeye (Warumi 8:9). Hivyo "mtumwa" ni tafsiri pekee sahihi ya neno doulos.

Mbali na kudhulumiwa, mtumwa wa Kristo kwa kweli ni huru. Tumeachiliwa huru kutoka kwa dhambi na Mwana wa Mungu ambaye alisema, "Ikiwa Mwana atakuweka huru, utakuwa huru kweli" (Yohana 8:36). Sasa Mkristo anaweza kusema kweli, pamoja na Paulo, "Kwa sababu sharia ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sharia ya dhambi na mauti" (Warumi 8:2). Sasa tunajua ukweli na ukweli huo umetuweka huru (Yohana 8:32). Kwa fumbo, kwa njia ya utumwa wetu kwa Kristo, tumekuwa pia wana na warithi wa Mungu Mkuu (Wagalatia 4:1-7). Kama warithi, sisi ni washiriki wa urithi huo-uzima wa milele-ambayo Mungu huwatunukia watoto wake wote. Hii ni fursa zaidi ya hazina yoyote duniani ambayo tunaweza kurithi, wakati wale walio katika utumwa wa dhambi wanarithi tu kifo cha kiroho na milele katika Jahannamu.

Kwa nini, basi, Wakristo wengi huishi kana kwamba bado wako katika utumwa? Kwa jambo moja, mara nyingi tunaasi Bwana wetu, kukataa kumtii Yeye na kushikilia maisha yetu ya zamani. Tunashikilia juu ya dhambi ambazo zilitufunga hapo awali kwa Shetani kama bwana wetu. Kwa sababu asili yetu mpya bado inaishi katika asili ya zamani ya kimwili, bado tunavutwa kwa dhambi. Paulo anawaambia Waefeso kuwa "kuvua" mtu wa zamani na udanganyifu wake na rushwa na "kuvaa" mtu mpya na haki yake. Kuvua uongo, na kuvaa ukweli. Kuvua wizi, na kuvaa manufaa na kufanya kazi. Kuvua uchungu, ghadhabu, na hasira, na kuvaa fadhili, huruma, na msamaha (Waefeso 4:22-32). Tumewekwa huru kutoka utumwa wa dhambi, lakini mara nyingi tunaruhusu minyororo kurudi kwa sababu sehemu yetu inapenda maisha ya zamani.

Zaidi ya hayo, mara nyingi hatujui kwamba tumesulubiwa na Kristo (Wagalatia 2:20) na kwamba tumezaliwa upya kama viumbe vipya kabisa (2 Wakorintho 5:17). Uzima wa Kikristo ni moja ya kifo kwa nafsi na kufufuka "kutembea katika upya wa uzima" (Warumi 6:4), na kwamba maisha mapya yanajulikana na mawazo juu ya Yeye ambaye alituokoa, si mawazo juu ya mwili uliokufa ambao umesulubiwa pamoja na Kristo. Wakati tunapoendelea kufikiri juu yetu wenyewe na kuifanya mwili katika dhambi ambazo tumeachiliwa huru, kimsingi tunabeba maiti, yenye imejaa uovu na kifo. Njia pekee ya kuizika kikamilifu ni kwa nguvu ya Roho ambaye ni chanzo pekee cha nguvu. Tunaimarisha asili mpya kwa kuendelea kudumisha Neno la Mungu, na kwa njia ya maombi tunapata nguvu tunayohitaji kuepuka tamaa ya kurudi kwenye maisha ya zamani ya dhambi. Halafu tutafahamu kuwa hali yetu mpya kama watumwa wa Kristo ni uhuru wa pekee wa kweli, na tutaita nguvu Zake "basi, dhambi isitawale ndini ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake" (Warumi 6:12).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Tunawezaje kupata uhuru wa kweli katika Kristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries