settings icon
share icon
Swali

Je! Mwanzo wa watu wa rangi tofauti ulitoka wapi?

Jibu


Bibilia kwa ukamilifu haituelezi mwanzo wa “rangi” au rangi ya ngozi tofauti ya mwanadamu. Kwa ukweli, kuna kizazi kimoja cha mwanadamu. Katika kizazi cha mwanadamu kuna utafauti wa rangi ya ngozi na hali za nche zinazoonekana. Wengine wanadhania kuwa, wakati Mungu alichanganyisha lugha katika mnara wa Babeli (Mwanzo 11:1-9), pia aliumba rangi tofauti. Inaweza wezekana kuwa Mungu alifanya ubadilisho kidogo ili awawezeshe wanadamu kuishi katika anga mbalimbali, kama vile ngozi nyeusi kwa Afrika, kwa chembe chembe za damu ziwawezeshe kukaa mahali kuna joto nyingi sana Afrika. Kulingana na mtazamo huu, Mungu alichanganyisha lugha, kuwafanya wanadamu kutawanyika kilugha, na hapo akaumba chembe chembe za damu tofauti kulingana ni wapi kikundi fulani kitaishi. Kwa kuwa na uwezekano kuwa hakuna msingi wa kibibilia wa mtazamo huu. Kizazi/rangi ya ngozi ya mwanadamu hakuna mahali zimetajwa katika Bibilia kuambatana na mnara wa Babeli.

Baada ya gharika wakati lugha tofauti zilianza kuwepo, kikundi ambacho kilizungumza lugha moja kilijitenga mbali na wengine waliozungumza lugha moja. Kwa kufanya hivyo, chembe chembe za damu zikashuka pakubwa sana kwa vile hicho kikundi hakikupata kujumlika na wengine. Uzao wa karibu ulifanyika na baada ya muda tabia fulani zikazingatiwa katika hivi vikundi tofauti. Uzao ulipoendelea zaidi katika vizazi, ule utofauti wa chembe chembe za damu ulipungua zaidi, hadi kiwango kwamba watu wa lugha ya familia moja wote walikuwa na tabia moja.

Maelezo mengine ni kwamba Adamu na Hawa walikuwa na chembe chembe za damu na kuzaa rangi nyeusi, na nyeupe (na kitu chochote hapo katikati). Hii inaweza kuwa sawa na vile kizazi kina changanyika na kuzaa watoto walio na rangi tofauti. Jinsi Mungu alikusudia mwanadamu awe na sura tofauti, inaleta maana kwamba Mungu huenda aliwapa Adamu na Hawa uwezo wa kuzaa watoto wa rangi tofauti. Baadaye, waliobaki pekee baada ya gharika mahali ambapo Nuhu na bibi yake, watoto wake watatu wa kiume na wake zao, watu nane kwa jumla (Mwanzo 7:13). Ingawa wakwe wa Nuhu walikuwa wa rangi tofauti. Pia inaweza wezekana kuwa mke wa Nuhu alikuwa wa rangi tofauti mbali na ile ya Nuhu. Pengine wote nane walikuwa wa rangi tofauti, ambayo yaweza maanisha kuwa, walikuwa na chembe chembe ambazo zingeweza kuzaa watoto wa rangi tofauti. Elezo lolote lile litakapokuwa, cha muimu katika swali hili ni kwamba wote ni watu wa kizazi kimoja, wote tumeumbwa na Mungu mmoja, wote tumeumbwa kwa lengo moja-kumtukuza Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mwanzo wa watu wa rangi tofauti ulitoka wapi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries