settings icon
share icon
Swali

Mbingu mpya, nchi mpya ndio gani?

Jibu


Watu wengi wako na dhana potovu juu ya mbinguni itakuwa kama nini. Ufunuo mlango wa 21-22 yatupa kiupana picha kamili ya mbingu mpya na nchi mpya. Baada ya matukio ya nyakati za mwisho, mbingu ya sasa na nchi ya sasa zitatolewa na zibadilishwe na mbingu mpya na nchi mpya. Mahali pa kukaa milele pa Wakristo patakuwa katika nchi mpya. Nchi mpya ni “mbinguni” mahali ambapo tutakaa milele yote. Ni katika nchi mpya Yerusalemu mpya, mji mkuu wa mbinguni utakuwa. Utakuwa katika nchi mpya ambapo milango yake na njia zake zitakuwa sha dhahabu

Mbingu- na nchi mpya- ni mahali panapoonekana, ambapo tutaishi na miili ya utukufu (1 Wakorintho 15:35-58). Hoja kwamba mbinguni itakuwa katika “mawingu” ni jambo lisilo la kibibilia. Dhana kuwa tutakuwa “roho zinazo elea mbinguni” pia sio la kibibilia. Mbingu ambayo watakatifu wataiona itakuwa sayari mpya na kamilifu ambapo tutaishi. Nchi mpya haitakuwa na dhambi, uovu, magonjwa, mateso na kifo. Itakuwa sawa na nchi hii ya sasa, au pengine nchi iumbwe upya lakini isiwe na laana yoyote au dhambi.

Je! Na mbingu mpya? Ni muhimu kukumbuka kwamba wazo la kale, “mbinguni” ilimaanisha mawinguni ya juu kabisa ambapo Mungu anakaa. Kwa hivyo wakati Ufunuo 21:1 yazungumzia mbingu mpya, kuna uwezekano kuwa inamaanisha kuwa sayari mpya itaumbwa- nchi mpya, mawingu mapya, na sayari ya juu kabisa mpya. Inaonekana kana kwamba mbingu ya Mungu itaumbwa upya pia, kukipa kila kitu ulimwenguni “mwanzo mpya,” hata kama ni mwili au kiroho. Je! Tutapata ruhusa ya kuingia mbingu mpya milele yote? Labda, lakini tutangoja tuone. Tafadhali wote tuliruhusu neno la Mungu lichonge uelefu wetu wa mbinguni.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mbingu mpya, nchi mpya ndio gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries