settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inasema nini kuhusu malaika Gabrieli?

Jibu


Malaika Gabrieli ni mjumbe ambaye aliaminika kuwasilisha ujumbe kadhaa muhimu kwa niaba ya Mungu. Gabrieli anaonekana angalau kwa watu watatu katika Biblia: kwanza kwa nabii Danieli (Danieli 8:16); mwingine kwa kuhani Zekaria kutabiri na kutangaza kuzaliwa kimuujiza kwa Yohana Mbatizaji (Luka 1:19); na hatimaye kwa bikira Maria kumwambia kwamba atakuwa na mimba na kuzaa mwana (Luka 1:26-38). Jina la Gabrieli linamaanisha "Mungu ni mkuu," na, kama malaika wa kutangaza, yeye ndiye aliyefunua kwamba Mwokozi angeitwa "Yesu" (Luka 1:31).

Mara ya kwanza tunamwona Gabrieli, anaonekana kwa Danieli baada ya nabii huyo kuwa na maono. Jukumu la Gabrieli ni kuelezea maono kwa Danieli (Danieli 8:16). Mwonekano wa Gabrieli ulikuwa ule wa mtu (Danieli 8:15; 9:21). Wakati Gabrieli alimtembelea Danieli mara ya pili, alikuja kwake "akirushwa upesi,alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni" (Danieli 9:21). "Kurushwa" kwa Gabrieli kunaweza kupendekeza mabawa, lakini mabawa hayatajwi. Pia ni wazi kwamba kuonekana kwa Gabrieli kulikuwa wa kutisha, vile Danieli alianguka kwa uso wake mbele yake (Danieli 8:17) na alikuwa mgonjwa kwa siku baada ya uzoefu wake na malaika na maono (Danieli 8:27).

Katika Danieli 10 tunaona mwingiliano mwingine kati ya nabii na "mmoja mfano wa watoto wa wanadamu" (mstari wa 16); hata hivyo, hakuna jina linalopewa mjumbe huyu. Malaika anasema amekuja kumsaidia Daniel kuelewa maono yake, hivyo inawezekana sana kwamba kifungu hiki pia kinamaanisha malaika Gabrieli. Kutoka kwa lugha katika kifungu, inawezekana pia kwamba kuna malaika wawili na Daniel-mmoja akizungumza naye na mwingine kumtia nguvu ili apate kujibu (Danieli 10:16, 18). Malaika pia anarejelea vita vinavyotokea katika uwanja wa kiroho. Malaika huyu, ambaye tunaweza kudhani ni Gabrieli, na malaika Mikaeli walikuwa wanaohusika katika vita na mfululizo wa wafalme wa pepo, ikiwa ni pamoja na wale walioitwa mkuu au wafalme wa Uajemi (mstari wa 13) na mkuu wa Uyunani (mstari wa 20 ).

Gabrieli anasema kwamba alitumwa kutoka mbinguni na jibu maalum kwa sala ya Danieli. Gabrieli alikuwa ameondoka ili kuleta jibu mara tu Danieli alianza kuomba (Danieli 10:12). Lakini Gabrieli alikumbana na shida njiani: "Lakini mkuu wa Ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja" (Danieli 10:13) na kwa kweli akamzuia kuja kwa Danieli kwa haraka iwezekavyo. Hapa tuna mtazamo wa mara moja katika ulimwengu wa kiroho na vita vinafanyika nyuma ya jukwaa. Malaika watakatifu kama vile Gabrieli wanafanya mapenzi ya Mungu, lakini wanakabiliwa na viumbe wengine wa kiroho ambao wanataka tu uovu duniani.

Ujumbe wa Gabrieli kwa kuhani Zakaria, baba ya Yohana Mbatizaji, ulitolewa katika hekalu vile Zekaria alikuwa akitumikia mbele ya Bwana. Gabrieli alionekana kwa upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia (Luka 1:11), ishara ya sala, na akamwambia Zekaria kwamba sala yake ilisikilizwa (mstari wa 13). Mke tasa wa Zakaria, Elisabeti, alikuwa anaenda kushika mimba na kuzaa mwana; mtoto huyu wa ajabu angeitwa Yohana, na angetimiza unabii wa kuja kwa Eliya (mstari wa 17, tazama Malaki 4:5). Ujumbe wa Gabrieli ulikutana na kutoamini, hivyo Gabrieli alimshitua kuhani mwenye shaka asiweze kusema hadi siku ya mtoto kutahiriwa (Luka 1:20, 59-64).

Kuonekana kwa Gabrieli kwa Maria kulikuwa kutangaza kuzaliwa bikira kwa Bwana Yesu Kristo. Mama ya Masihi alihakikishiwa neema yake na Mungu (Luka 1:30) na akamwambia Mwanawe atatimiza Agano la Daudi: "Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho"(mistari 32-33). Kwa kujibu swali la Maria juu ya jinsi hili lingeweza kutokea, kwa kuwa alikuwa ni bikira, malaika Gabrieli alisema mimba itakuwa matokeo ya kazi ya Roho Mtakatifu ndani yake, na kwa hivyo "kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu "(mstari wa 35).

Katika maonyesho yote matatu, Gabrieli alikutana kwa hofu, na alikuwa anaanza mazungumzo yake kwa maneno ya faraja na furaha kwa Danieli, Zekaria, na Maria. Inawezekana kwamba Gabrieli pia alikuwa malaika aliyeonekana kwa Yusufu katika Mathayo 1:20, lakini hili si hakika, kwa kuwa malaika huyo hajaitwa jina katika Maandiko. Tunachojua ni kwamba Gabrieli ni mmoja wa malaika wa Mungu mzuri na mtakatifu. Ana nafasi nzuri kama malaika ambaye "anasimama mbele ya Mungu" (Luka 1:19), na alichaguliwa kuwasilisha ujumbe muhimu wa upendo wa Mungu maalum na neema kwa watu waliochaguliwa kuwa sehemu ya mpango wa Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inasema nini kuhusu malaika Gabrieli?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries